Bernard Membe na Philip Marmo kutinga mahakamani wiki ijayo.


Ng'wanza Madaso

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2008
Messages
2,278
Likes
100
Points
160
Ng'wanza Madaso

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2008
2,278 100 160
Mtikila kuwaburuza mawaziri wa JK kortini
Na Beatrice Shayo
28th February 2010

Mtikila(11).jpg

Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia (DP), Mchungaji Christopher Mtikila.

Mawaziri wawili wanatarajiwa kufikishwa kortini wiki ijayo kwa ajili ya kujibu mashataka yanayowakabili dhidi ya kuvunja Katiba na sheria ya nchi kinyume na utaratibu uliopangwa.

Mawaziri hao ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo.

Akizungumza na gazeti hila jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, alisema kuwa kwa sasa mawakili wake wanamalizia utafiti wao.

Mtikila alisema kesi hiyo imechelewa kufikishwa mahakamani kutokana na mawakili kuwa na kazi nyingi. Hata hivyo, alisema pamoja na mawakili wake kuwa na kazi nyingi, wamefanikiwa kufanya utafiti wao kwa umakini na kwa kina ili itakapofika mahakamani wawe na taarifa zote muhimu.

Alisema utafiti wa kesi hiyo unafanywa na mawakili wanne na kwamba kufunguliwa kwa kesi hiyo kutatoa fundisho kwa viongozi wengine kwa kuacha tabia ya kutoa maneno ya ajabu na hatimaye kuvunja katiba na sheria ya nchi.

Kwa mujibu wa Mtikila, viongozi hao watapandishwa kizimbani kutokana na kauli zao walizotoa kwa nyakati tofauti kuwa suala la mgombea binafsi haliwezi kutekelezwa katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Alisema suala hilo liilitakiwa lijadiliwe na wananchi kwa ajili ya kura za maoni na sio viongozi hao kusema hakutakuwa na mgombea binafsi katika uchaguzi mkuu.

"Utaratibu wa kuwasimamisha kizimbani Marmo na Membe kwa kuvunja Katiba na sheria kwa kuthubutu kuifanyia jeuri na dharau mahakama ya nchi uko palepale tena mwishoni mwa wiki mawakili wangu wanamalizia utafiti na hivyo msione kimya," Mtikila alisema.

Mtikila alisema hoja ambazo zimekuwa zikitolewa na mawaziri hao pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Rajab Kiravu, ni za porojo na haziwezi kuathiri utendaji wa mahakama.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 

Forum statistics

Threads 1,236,267
Members 475,050
Posts 29,252,161