Benki tatu hatarini kufungwa kutokana na mtikisiko wa uchumi

mwambojoke

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
1,081
646
Benki tatu hatarini kufungwa kutokana na mtikisiko wa uchumi
-Benki ya wanawake 'TWB'
-Ecobank Tanzania
-Efatha Bank

[HASHTAG]#MWANANCHI[/HASHTAG] NEWSPAPER 4th May 2017

=======

Dar es Salaam. Hali ya mtikisiko wa uchumi uliozikumba taasisi nyingi, hasa za fedha sasa unazinyemelea benki tatu ambazo zinaweza kuwekwa chini ya uangalizi maalumu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kama ilivyokuwa kwa Twiga Bancorp.

Twiga Bancorp, ambayo kwa sehemu kubwa inamilikiwa na Serikali, imewekwa chini ya uangalizi wa BoT baada ya madeni yasiyolipwa (NPL) kuzidi kiwango kinachotakiwa kisheria.

Hali hiyo inazinyemelea taasisi nyingine tatu za fedh; Benki ya Wanawake (TWB), ambayo pia inamilikiwa na Serikali, Ecobank Tanzania na Efatha Bank, ambayo inahusishwa na taasisi ya kidini ya Efatha, kwa mujibu wa uchambuzi wa The Citizen ambalo ni gazeti dada la Mwananchi.

Benki hizo tatu zimelimbikiza kiwango cha NPL kinachozidi asilimia 50 ya jumla ya mikopo iliyotolewa, huku kiwango cha Efatha kikifikia asilimia 63.

Wataalamu wa benki wanaamini kuwa kiwango cha NPL kinachozidi asilimia 15 ya jumla ya mikopo yote ya beki za biashara, kinaashiria uwezekano wa kuanguka.

Katika toleo la tisa la Hali ya Kiuchumi Tanzania, Benki ya Dunia ilitahadharisha kuhusu kukua kupita kiasi kwa kiwango cha NPL, ambacho kilifikia asilimia 9.5 mwaka 2016 kutoka asilimia 6.4 mwaka 2015.

Ripoti hiyo iliitaja TIB Development Bank ambayo kiwango chake cha NPL kilikuwa asilimia 38 katika robo ya kwanza ya mwaka 2017.

Hata hivyo, taarifa za fedha za benki za biashara za robo ya kwanza mwaka 2017 zinaonyesha hali ni mbaya zaidi kwa Efatha, TWB na Ecobank Tanzania.


Chanzo: Mwananchi
 
Hapo labda EcoBank ndiyo ya kuiulizia, TIB ilikuwa lazima ife tu, wale ma director wamechota hela na kuanzisha miradi bila kurudisha mikopo yao, kama kawaida yetu, kupenda kukopa lakini watata kurudisha..
Hizo zingine sidhani hata kama zina sifa zakuwa benki aise...wataalam watakuja

Halafu mkuu si ana akaunti Ecobank??
Nakumbuka mwanzoni alishtukiza kwenda kuchukua mpunga pale
 
Na TIB pia? Kweli Hali ngumu. But nini tafsiri ya hii Hali ya mabenki mengi nchini kutikisika?
Ni Mtikisiko mpya wa mdororo wa uchumi duniani,hii imeanzia china lakini Tanzania tunaumia zaidi pia inaongezewa na uwezo wa wafanyabiashara na wafanyakazi kushindwa kurudisha mikopo kutokana na hali ya uchumi nchini kudorora.
 
Ni Mtikisiko mpya wa mdororo wa uchumi duniani,hii imeanzia china lakini Tanzania tunaumia zaidi pia inaongezewa na uwezo wa wafanyabiashara na wafanyakazi kushindwa kurudisha mikopo kutokana na hali ya uchumi nchini kudorora.
Mkuu sidhani ni mdororo wa uchumi duniani.

Ukiangalia hizo benki zina mtandao wa local bank- Efatha ni benki - ya hapa hapa .

TWB- hii ni benki ya wamama na wengineo, ambayo imejikita kwa mikopo ya wafanyabiashara wa chini akina mama.

ECOBANK - hii ni benki ni kutokana na mabadiliko ndani ya bank yenyewe, hata huko nje ya nchi wamefunga matawi mengi.

Sasa nataka niongelee TWB + EFATHA

Hizi benki zimeathiriwa hali ya uchumi inavyoendelea hapa nchini. Mzunguko wa pesa ni mdogo, au kwenye maeneo machache. Hasa baada, ya serikali kupunguza matumizi na kutumia kwenye maeneo machache kama miundo mbinu.

Kwa upande mwingine, hizi benki kama TWB au EFATHA, utaona hayana mtandao mkubwa wa matawi.
Biashara ya benki kama deci fulani... wateja wasio na kazi na hela wanapeleka hela bank... halafu wao wanazikopesha kwa wenye mahitaji... Endapo benki hazina matawi, basi makusanyo yao yanakuwa madogo sana.. Na watu wasipoenda kukopa , basi ndio benki hazipati hela kabisa.

Kufuatana na hali ya siasa za uchumi hapa nchini, serikali haifanyi biashara na sekta binafsi.. Wanapendelea kufanya biashara wao kwa wao... Mfano biashara ya ndege, wafanyakazi wa serikali na taasisi, mashirika, wanapokuwa kwenye safari za kikazi kutumia ATCL tu ... Hapa kuna watu chungu nzima wanatolewa kwenye biashara.

Angalia mambo ya bima , kama hapo juu, makampuni ya serikali yapeleke bima kwa NIC tu... Sasa unapofanya namna hizo kuna biashara nyingi sana , unawatoa kwenye mzunguko... agent, brokers na hata insurance company.

Kwa hiyo, huu ni mwanzo wa sector binafsi na biashara nyingi kuporoka na kufungwa .... Sera za uchumi, zinasababisha biashara nyingi kufungwa ni suala la muda.
 
Back
Top Bottom