Belle9 sio wa nchi hii, hakuna kama yeye bongo

sonofobia

JF-Expert Member
Jun 21, 2015
1,054
4,062
Hakika uwezo wa Bellenine ni wa juu sana.
Kijana hana skendo wala mbwembwe ila muziki wake na talent yake ndio inambeba.

Wcb wametoa nyimbo mia maskendo na promo. Benpol kajianika utupu wake. Kiba kaja na remix tatu mara record label. OmmyDimppz anadanga nje ya nchi. Wote wamebuma.

Kijana wa watu mtaratibu asiye na makuu Bellenine akawapa kitu kimoja tu Ma Ole na amewafunika wote.

Anakwambia suadina nampenda suadina suadina suadina mama yake namjua alafu anamalizia una maole una maole my one and only yani utakubali tu hii talent ya ukweli

Hakika Belle 9 ni kipaji cha nchi za mbele sio wa nchi hii.
 
Back
Top Bottom