BEEF: Canibus VS LL Cool J

BEEF: Canibus VS LL Cool J

Infopaedia

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2011
Posts
1,231
Reaction score
1,495
download (2).jpg
Mambo vp wadau. Mara kwa mara nimekuwa nikisikia mivutano ya wasanii wetu hapa Bongo, Hasa Kiba na Chibu. Hii mivutano yao imenisukuma kuandika japo kidogo kuhusu beef ama ugomvi wa msanii nguli wa Hip hop, Ladies Lover Cool James a.k.a ‘LL Cool J’ na bwana mdogo mmoja mbishi sana….Canibus a.k.a Canabis a.k.a Bis. Vichwa vyote hivi viwili ni vya New York City. Hii beef ilikuwa ni kama Daudi na Goliath kwa kweli. Hebu fikiria baada ya beef kukolea, LL alipiga bit hadi redio zote za NYC hakuna kupiga truck za Canibus, mtu huyo alikuwa na power kiasi gani!!!. Lakini dogo bado alijaribu kupenya. Katika historia ya beef za wasanii wa music hapa duniani, LL V/S Bis ni moja kati ya beef ambayo ilitoa one of the best dis truck katika ulimwengu wa Hip hop. ‘Second round knockout’ ya Canibus, hii ni dis truck ambayo wachambuzi wa beef mpaka leo wanapata taabu kuamini alichokifanya bwa mdogo Canibus. Lakini ni moja kati ya beef ambazo chanzo chake ni cha kipumbavu kabisa. Kitu kilichopelekea the whole beef kuto-make sense kabisa.

NANI NI NANI!

Kati ya mwaka 1985 mpaka mwaka 1996 LL Cool J tayari alikuwa ni legendary na mkongwe kwenye game ya hip hop. Akiheshimika na kila mtu kwenye tasnia ya muziki na entertainment kwa ujumla. Alikuwa na awards kibao tu, kagonga platinum+ za kutosha, alikuwa mpaka na TV show. Yaaani kuhusu fan base…… kwa LL ndo ilikuwa ‘usibonyeze’ kabisa. LL Cool J alikuwa ni kipenzi cha kina dada na akipanda jukwaani akivua shati daaaah!!!!....demu wako lazima apagawe. LL ndiye aliyebadili Hip hop ikawa sweet kivile. Jamaa alikuwa bishoo by default yaani mpaka machizi wanazima fegi. Alikuwa ni icon flani hivi ambaye akitimba lazima heshima ichukuwe mkondo wake. By that time LL alishakuwa na beef na kuwakalisha wajanja kama kina Cool moe Dee na Ice T. Hata Mc Hammer mwenyewe alichezea vitasa vya lyrics toka kwa LL………hivi inawezekana kweli, “Ndo hivyo ishatokea mwana”.

Kipindi hicho LL tayari alikuwa na album kama sita hivi, 'Radio' ya mwaka 1985, 'Bigger and Deffer' mwaka 87, 'walking with the Panther' ya mwaka 89, 'Mama said knock you out' ya mwaka 90, '14 shots to the dome' ya mwaka 93, 'Mr Smith' ya mwaka 95. Kwa ufupi LL alikuwa amesheheni, tayari ni role model mkubwa tu katika kipindi hicho. Jamaa alikuwa na kilakitu, yaani money, power, respect. The guy was ‘’heavy weight”. Reginald Noble a.k.a Redman anasema, “LL is a beast”.

Na katika kipindi hichohicho cha miaka ya 1996, Canibus alikuwa kijana mdogo tu. Ndio kwaaaanza anahangaika atoke vp. Canibus alikuwa chini ya Wyclef Jean (kama unawakumbuka Fugees). Wyclef alikuwa akiheshimika na machizi mtaani walikuwa wakimpa ‘shanazi’ flani hivi. Aliweza kuongea na watu wakubwa tu. Wyclef akamu-introduce Canibus kwa LL Cool J na kumwambia "huyu dogo ni 'nyoko' bro". Canibus mwenyewe katika moja ya interview zake, anasema alikuwa anamkubali sana tu LL. Na siku aliyo kutanishwa naye kwa karibu alijua ‘this is my time’. Canibus alikuwa akitafuta mtu ambaye angeweza kumbeba na kumuweka mbele ya hadhira, balaa lililobaki Canibus angelifanya yeye mwenyewe kwa mkono wake kwa kutumia mic, style yake na mistari yake plus confidence yake. As matter of fact dogo hakuwa na ramani yoyote wala historia yoyote kwenye game. Mara nyingi alikuwa aki-hang na machizi wa Def squad, Molly G, Keith Murry, Redman….. wana-battle na kufanya yao mtaani. Na Squad walikuwa wanamkubali dogo, yaani ‘kimbwambwa!!!!’.


IKAANZAJE BEEF SASA!!

Mkubwa LL alikuwa na kawaida ya kuwatoa ma-mc wadogo. Au tuseme Def Jam walikuwa na project za kuchukuwa underground Mcs na kumbebesha LL ili awatoe. Kwenye album zake alikuwa akiandaa truck na kuwashirikisha underground mcs ili wafanye yao nao watoke kivyao. Mwaka 1997 LL alimkumbuka dogo Canibus. Akamvutia uzi Wyclef ‘ebana-eee, hebu mlete yule dogo tuone inakuweje’. Kwenye album yake ya Phenomenon ya mwaka 1997, LL aliandaa truck inayoitwa '4,3,2,1’. Kwenye hii truck DMX alipewa shavu, Redman alipewa shavu, Methodman alipewa shavu, na Canibus nae pia alipewa shavu. Ebana-eeee……si kitoto huo mzigo, coz jamaa wote hao walikuwa ni vichwa vya kufa mtu, Plus hawana ramani flani inayosomeka kiviiile. Hasa DMX ndo alikuwa bado kabisa. So kilamtu alitaka sifa kwenye hii ngoma na kila mtu aliitendea haki hii ngoma. Ila mzee mzima LL nae ilibidi akaze kwenye hii ngoma. Yaani angelemaa kidogo tu, madogo ilikuwa wanampa mitama ya kushtukiza halafu inakuwa siyo kabissa. To be honest, for the first time nilim-feel LL. Ngoma ilitoka kali sana. Moja kati ya ngoma ninazosikiliza mpaka kesho. Kwenye plan ‘A’ Master P ilikuwa awepo kwenye hii ngoma. Lakini sijui kwanini haku-appear.

Lakini amini usiamini, beef ya LL na Canibus ndiyo ilianzia hapo kwenye hii truck ‘4,3,2,1’. Wakati wanaandika michano ya ‘4,3,2,1’, kwenye verse yake Canibus akasema ‘’Yo L, is that a mic on your arm? Let me borrow that’’. LL Cool J amechora tattoo ya mic kwenye mkono wake wa kulia kama anavyoonekana hapo down. Canibus alikuwa ana-refer tattoo ya LL kwenye mkono.

image002.jpg

LL ali-mind kinomanoma huo mstari wa Canibus kuhusu mic yake. Tho KRS ONE alijaribu kuelezea why LL ali-mind, lakini mi mwenyewe mpaka leo sijaelewa why ali-mind. Kilichomkera Zaidi LL ni fact kwamba Canibus alikuwa bwana mdogo kwenye game lakini alikuwa na vi-atitude flani hivi. Dogo alikuwa hana ‘shanapa’ na mtu. Yaani uwe nani,,,,,,sijui baba yako nani . . . Canibus don’t give a ‘shikamoo’. Na kaka mkubwa yeye tayari ana ‘empire’, anapenda kulambwa nyayo. Sasa kuna nini tena hapo, Canibus lazima achezee za mbavu tu, hakuna namna. Kumbuka kama nilivyokwambia hapo juu, LL alikuwa na kilakitu……money, power, respect. Nyuma ya LL kulikuwa na label ya Def Jam na LL ndio kilikuwa kichwa kinachotegemewa pale Def Jam. If you mess with LL you mess with Def Jam, you mess with ‘masadali’, unaponaje sasa kwa mfano!!!?.

Canibus anasema yeye alipigiwa simu aende studio akafanye kazi kwenye ‘4,3,2,1’ ambayo ilikuwa ni truck kwenye 'phenomenon', album mpya ya LL. Hiyo ilikuwa 1997 kwenye August hivi. Anakumbuka alipofika, pia alimkuta DMX yupo studio. DMX na yeye waliingiza vocals zao siku hiyohiyo. Mchizi akamaliza mzigo, ‘flengo'……'flengo', akatoa ‘gwala’…kum…kum… ‘akasepetuka’. Baada ya siku mbili tatu akapigiwa simu kwamba LL ame-change plan inabidi arudi akabadilishe verse yake. Bis akaona siyo case, ‘mi mwenyewe tena msitu wa vina’. Canibus alipofika studio ndo akaambiwa kwamba LL ameamua abadilishe mistari yake. Kama Bis nae anataka aendelee kuwepo kwenye truck, na yeye hanabudi abadilishe verse yake, aondoe maneno kuhusu tattoo ya kipaza kwenye mkono wa LL. Canibus akasema 'poa ka mkubwa, haina noma’. Wakakubaliana kwamba wote watabadilisha. Yaani LL atabadili verse yake, na Bis nae ata-change verse yake. Ikumbukwe kwamba LL ali-rewrite verse yake baada ya kusikiliza verse ya Canibus. Baadae akaona hapana, lazima nimuonyeshe dogo mimi ni mbavu nene. LL akatumia ujanja zaidi, ndio akamshurutisha Bis abadili verse yake kwa ahadi kwamba na yeye atabadili. Canibus akabadilisha mistari na kuondoa maneno kuhusu mic tattoo ya LL. Canibus alifuta kiroho safi tu asijue kumbe mwenzake bado ‘amekunja kimbwambwa’. LL alifanya opposite, hakubadilisha verse yake wala nini. Mpaka ‘4,3,2,1’ inatoka na kuingia kitaa, verse ya LL ‘anamkandya’ Canibus ipo. Maana yake nini!!, maana yake two mcees beefing in the same truck ya kishkaji. Ndio maana watu wanaona chanzo na sababu ya hii beef ni ridiculous kabisa.

Mstari ambao Bis alishurutishwa kuutoa na akautoa unasema:

’Yo L, is that a mic on your arm? Let me borrow that’’

Redman anasema, “Bis alikuwa ni kijana mpole sana na alikuwa msikivu kwa kilamtu. Ila ni dogo asiyependa ‘mashauzi’ kabisa”. Redmen anasema kwamba Bis hakuwa na maana mbaya, aliposema L amuazime ile mic kwenye mkono. Ilikuwa ni njia ya kuonyesha heshima kwa LL, kumshukuru kwa kumpa ‘dodo’ kufanya kazi na vichwa vigumu kama Redman, Dmx na LL mwenyewe. Lakini waliposikia LL ameandika upya verse yake. Wakajua enheee….kimenuka.

Kwenye verse yake LL anamjibu Bis direct, anasema:

“The symbol on my arm is off limit to challengers,

you hold the rusty swords I swing the Excalibur”.


Then mbele akaendelea tena, kum-punch Canibus

“Now let’s get back to this mic on my arm,

If it ever left my side it’d transform into a time bomb,

You don’t wanna borrow that, you wanna idolize,

And you don’t wanna make me mad nigga you wanna socialize”.


Dah! LL alimchana Canibus, alim-dis canibus mwa-mwe. Sijui jamaa alikuwa na kisasi gani na huyu mtoto.

Ukiangalia kwenye hii truck, wote watano wame-dis na ku-brag a lot (ndio kawaida ya ma-mc). Lakini since hakuna mtu aliyetajwa, dis zote zinakuwa kama kutupa jiwe gizani vile. LL alikuwa mjanja sana, technically aliona kwamba kama opening lines kwenye verse ya Canibus zimeelekezwa kwake. Basi dis lines zote zinazofuata zitakuwa zinamlenga yeye. Hata kama Canibus hakumaanisha hivyo, lakini hadhira ingeelewa hivyo. Hata logically ni hivyo tu haiepukiki. Hata Redman alipoulizwa alisema yeye alikuwa anajua kwamba Bis alikuwa anamlenga LL. Lakini hakujua kama itakuwa serious to that extent.

Hivyo LL akaona no way, akamshurutisha Canibus “dogo futa mistari hiyo!”. LL alichangia sana kudugisha career ya Canibus kwasababu ya beef yao. Canibus alikuwa ni hatari, alikuwa ni scientific lyricist, alikuwa na sauti, alikuwa na style, na Bis alikuwa muandishi mzuri. Canibus alihesabika kama Rakim mpya wa enzi zake. Mitaa ilimuelewa lakini kwenye main stream hakuweza kupenya vizuri kama alivyostahili sababu ya LL.

Kimsing LL alimchezea foul Canibus. Kwenye '4,3,2,1' LL alijibu mistari ya Bis ambayo Bis alikubali kuifuta na aliifuta. Bis yeye hakuisikiliza ngoma kabla haijatoka. Alikuja kusikia verse ya LL ngoma tayari ikiwa meachiwa mtaaani. Bis hakupendezwa, akajaribu kuongea nae lakini LL akadai hakuna mtu angejua kwamba verse yake ni dis kwa Bis. Kibaya Zaidi LL alimtosa Canibus kwenye video ya ‘4,3,2,1’. Na wala LL hakumshirikisha kwenye show za ‘4,3,2,1’ japokuwa wengine wote walikuwa wakishirikishwa vizuri tu, mpaka kwenye ma-interview.

image003.jpg

Redman, Methodman, DMX, na LL upande wa kulia amekatwa. Baada ya kuhojiwa na mtangazaji wa MTV, wakiwa wametoka kwenye show.

‘4,3,2,1’ ilipoingia mtaani, mingong’ono ikaanza kusambaa kwamba verse ya LL ilikuwa ni dis kwa Canibus. Kibaya zaidi original track kabla Bis hajarekebisha verse yake nayo ilivuja mitaa ya NYC, watu wakaipata. Pia ikaja ikagundulika kwamba Bis aliandika 46 bars lakini kwenye ‘4,3,2,1’ zilitumika 16 bars tu, of course bila consultation au consent ya Bis. Canibus akaanza kupata pressure from kila kona….’’inakuwaje unakubali kufanyiwa
?, yaani panya road unakubali kuzinguliwa na bishoo wa ‘Sengerama’!!!!”. Masela wakawa wanaendelea kumtia chumvi mwana. Kwa heshima na taadhima Bis haku-disclose chochote related na dadhia yote hiyo. Ila kwavile issue ilishasanuka ‘kishakunaku’ flani…na Bis hakutaka kupoteza nafasi aliyopewa na LL, Ukae ukijua kwamba balaa alilolifanya Bis kwenye ‘4,3,2,1’ si la nchi hii. Yaani maskani zote ikawa zogo. Machizi wanaulizana “hivi huyu ni dogo gani kawatimulia masela kivile!!”. Kwenye ‘4,3,2,1’ Canibus alijipambanua kwenye angle zote, ilikuwa fire. Bis mwenyewe alijuwa nimeshatoboa. Ukiweza kutoboa NYC kuna nini tena!! Ni kama vile ukitoboa na kuwa supernyota DSM mjini, by default wewe ni nyota TZ nzima. Asikudanganye mtu weweee!!!, barabara zote zinazojengwa Tz mchongo mzima ni kuleta wepesi wa kufika DSM mjini. Turudi New York!!!!!...Canibus alijaribu sana kumsihi kaka mkubwa haya mambo wayamalize kishkaji tu. Coz alijua this is my time kutoka and I don wanna blow this opportunity. Ilikuwa ni kama vile Chibu alivyomuokota Chinga from nowhere, halafu Chinga amletee mbavu Chibu……..Kwangwalu isinge-exist. Chinga angeendelea kulamba reli mwa-mwe to date. Tuachane na Bongo. Bis alimuomba LL hata wafanye underground track tu ili ‘kuipelemba’ mitaa kwamba issue ziko ‘mswano’, then waendelee na ‘pelaso’ zao, dah!!. Lakini LL Cool J…..Kaka mkubwa….King of New York…..Bishoo…...Greatest Of All Time, alikaza, akakaza na akamkazia Canibus. Na kipindi chote hicho Bis alikuwa very humble, lakini mchizi LL akasema…NOOOOH, "Mimi sijaribiwi”

Issue ya kupigwa ngumi ya kuviziwa ilimuuma sana Canibus ila alijikaza kisabuni tu, atafanyaje!!!!. Ni kama vile waswahili tunavyosema ‘mkubwa hakosei’. Kwenye ‘mbilinge’ lote hilo mambo ma5 yalikuwa ni dhahiri shahiri kwa Bis. Mosi: hakukusudia kum-dis LL wakati anaulizia ile tattoo. Pili: LL alimchezea rafu kwa kumuhadaa abadili lyrics zake. Tatu: alipokwa tonge mdomoni. Nne: Alijaribu kila njia yaishe, na Tano: Lyrically ana uwezo wa kumnyuka LL within a split second. Maji yakawa yamemfika shingoni.

Canibus akaona nough is enough!! akaamuwa kufanya maamuzi magumu. Officially akaanzisha BEEF na LL Cool J. Yalikuwa ni maamuzi magumu coz by that time watu walikuwa wanachukulia beef very serious. Uki-lose beef battle you lose your career and is the end of your story. Canibus akamvaa LL Cool J, akamvaa ile 'kimbwambwa'!!!!

DAH! Beef ndio kwanza imeanza, lakini inabidi tupumzike kidogo. ITAENDELEA!!
 
Niliifuatilia sana hii beef endelea kuna mengine nitakuongezea
 
Umenikimbusha mbali sana, sana umefanya nilisikilize 4,3,2,1 dah indelea bwana...
 
Nakumbuka The legendary 2pac Amaru..alikua hampendi LL mno...akilalamika kwamba LL alikua anaringa....
 
Dogo Alichemka maana si lazma kukaa new york kwa miaka ile angehamia Cali...na Angetoka au angeshikwa mkono na malegendary..kama KRS One, Rakim au hata ICE T
 
Dogo Alichemka maana si lazma kukaa new york kwa miaka ile angehamia Cali...na Angetoka au angeshikwa mkono na malegendary..kama KRS One, Rakim au hata ICE T
Dah!!! ni kweli lakini ilikuwa ni ngumu kidogo. Coz kipindi hicho watu walikuwa wana-move toka maeneo mengine kuja NYC kutafuta mafanikio.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom