Hili la kutumia muda zaidi kwa issue za Kenya ni kweli hasa kwenye amka na BBC.
Sasa ninyi mnataka BBC itangaze nchi yenu (TZ) au habari?
Mkiwa na habari mtatangazwa! Vinginevyo watatangazwa wanyarwanda, wakenya na hata waganda; kama majukumu yao yanatengeneza habari.
Men, be accountable; acha kulalama! Sidhani iwapo Karume au Vuai wanazo habari kwa ajili ya BBC kutangaza, labda waendelee kugombea mafuta yatakayopatikana Zanzibar mwaka 2500 na kuchimbwa mwaka 3000!
Kama una malalamiko au unamapendekezo watumie ujumbe wa maandishi kwa email. Ni kweli kama hakuna habari hawawezi kutangaza. Ni kweli pia Kenya kuna reporters wengi kuliko TZ na habari nyingi hupatikana. TZ kuna reporters wachache ama waliopo pia wanatumia muda mwingi kufanya kazi zao badala ya kutafuta habari. Pia BBC hawatangazi habari za umbea ambayo hawajaweza kuthibitisha upande wa pili au source yake. Je lini mmesikiliza TBC mara ya mwisho?