BARAZA la Wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA), limesema kuwa linaunga mkono tamko la Makamu Mwenyekiti wa chama hicho John Heche, la kupinga uchaguzi mkuu wa 2025 na kueleza kuwa uchaguzi huo ni batili.
Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 20 Desemba 2025, Sharifa Suleiman, Mwenyekiti wa Bawacha -taifa amesema kuwa uchaguzi huo mbali kuwa hakuwa na uhalali uligubikwa na matukio ya uvunjwaji wa haki za binadamu “Wanawake walikuwa waathirika wakubwa wa matukio hayo ya kihalifu walikuwa wanawake”.