BAVICHA Waongeza Nguvu Mtwara

BAVICHA Waongeza Nguvu Mtwara

Chademakwanza

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2014
Posts
6,346
Reaction score
1,872
Baraza la vijana wa CHADEMA (BAVICHA ) Wameelekea Mkoa wa Mtwara hii leo,wakiongozwa na Katibu Mkuu wa BAVICHA Julius Mwita,Naibu Katibu Mkuu bara Getrude Ndibalema na Katibu Mwenezi wa BAVICHA Taifa Edward Simbeye.

Watafanya mikutano sita ya hadhara,kuhamasisha uandikishaji wa wapiga kura katika Daftari la kudumu la wapiga kura.
Pamoja na hayo watakagua uhai wa Chama na kufanya mafunzo ya Uongozi kwa viongozi wote wa CHADEMA.

Leo kuanzia saa kumi jioni,kutafanyika mikutano miwili katika kata ya Mwena jimbo la Masasi,tarafa ya Chikundi na Mkutano wa mwisho utafanyika Ruangwa mjini Jimbo la Ruangwa.

Mungu Ibariki BAVICHA,Mungu ibariki CHADEMA Mungu ibariki Tanzania.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
....hujitambua weye! mvuto ndiyo nini? MACCM wana mvuto? Kwenye lipi ikiwa kila kitu nchini ni shakalabaghala? Elimu doro, ajira doro, matibabu doro, deni la Taifa doro, thamani ya shilingi doro, uchumi doro, usafiri wa angani, barabarani na majini doro, mishahara inayokidhi gharama halisi za maisha doro na bado mnaimba usiku na mchana eti MACCM ni nambari one!? Nambari one kwenye nini!? labda kuliangamiza Taifa na kupokea rushwa.

Bavicha imepoteza mvuto
 
Makamanda wameshaingia Masasi mjini hapa, kesho saa 8 mchana wanapiga shoo eneo la uwanja wa fisi nyuma wa stendi kuu
 
Makamanda wameshaingia Masasi mjini hapa, kesho saa 8 mchana wanapiga shoo eneo la uwanja wa fisi nyuma wa stendi kuu
Tutaendelea kuwapa habari za Chadema mara kwa mara

Cc. Tumaini Makene, Kurugenzi ya Habari, Molemo, Chademakwanza, Greenwhich, crashwise, Standalone, Mwanahabari Huru
 
BAVICHA ilikuwa ya Heche hawa wasasahivi bora liende wasakatonge tu hawana lolote wababaishaji chadema inakufa mikononi mwao mwaka huu
 
BAVICHA ilikuwa ya Heche hawa wasasahivi bora liende wasakatonge tu hawana lolote wababaishaji chadema inakufa mikononi mwao mwaka huu
Mfumuko wa bei umeongezeka kwa 4.5% ndani ya wiki 2 hizi. Acha Bavicha wapulize Dawa
 
Baraza la vijana wa CHADEMA (BAVICHA ) Wameelekea Mkoa wa Mtwara hii leo,wakiongozwa na Katibu Mkuu wa BAVICHA Julius Mwita,Naibu Katibu Mkuu bara Getrude Ndibalema na Katibu Mwenezi wa BAVICHA Taifa Edward Simbeye.

Watafanya mikutano sita ya hadhara,kuhamasisha uandikishaji wa wapiga kura katika Daftari la kudumu la wapiga kura.
Pamoja na hayo watakagua uhai wa Chama na kufanya mafunzo ya Uongozi kwa viongozi wote wa CHADEMA.

Leo kuanzia saa kumi jioni,kutafanyika mikutano miwili katika kata ya Mwena jimbo la Masasi,tarafa ya Chikundi na Mkutano wa mwisho utafanyika Ruangwa mjini Jimbo la Ruangwa.

Mungu Ibariki BAVICHA,Mungu ibariki CHADEMA Mungu ibariki Tanzania.

Wakimaliza Ntwara waingie Lindi kwa Bi Mkubwa maana huko watu wamelala bado. Kusini kuchele
 
Tukisema ACT inawapa watu presure nyie mnakataa
 
chadema mna tatizo sasa mtwara mmekwenda kuzungu mzia matatizo ya wananch lakini ajabu mnaweka na porojo ACT wanahusika vipi?
Kwakua unapata ruzuku ya ccm unaona fisi tu hapo ulipo
 
Back
Top Bottom