WanaJF,
Kuna msemo niliwahi kuusoma zamani, 'mimi sio nyoka kwa sababu baba yangu hakuwa nyoka'...
Pia, wengi wetu (sio wote) ni wakristo au waislamu kwa sababu wazazi wetu ni wakristo au waislamu. Au kwa sababu tumelelewa kwenye mazingira hayo.
Hali hiyo imewakuta wengi linapokuja suala la ufuasi wa vyama hasa kwa vijana ambao wazazi wao walikuwa au ni viongozi wa ccm. Ukiangalia vijana walio kwenye baraza la vijana la chadema na wale walio kwenye umoja wa vijana wa ccm utaona hilo. Hata wale ambao umri umesogea kidogo na sio vijana tena.
Hapa nitatoa mifano michache;
1. Ridhiwani Kikwete
2. January Makamba
3. Nape Nnauye
4. William Malecela
5. Hussein Mwinyi
6. Abdulla Mwinyi
7. H. Kawawa
8. Mboni Mhita
Hawa ni baadhi ya wengi ambao kuwa kwao CCM ni dhahiri kumetokana na malezi na sio kwa kutaka kwao. Ndio maana wanafuata dini na makabila ya wazazi wao. Wamelazimika pia kufuata 'uanachama' wa wazazi wao.
Swali linabaki inawezekanaje wakawa na lolote jipya? Je wana uwezo kiasi gani kuwa na mawazo binafsi? Itawezekanaje wajivue gamba walilozaliwa nalo?
Kuna watu kama kina Makongoro Nyerere waliwahi kwenda tofauti lakini baadae tena wakarudi walikotoka.
Freeman Mbowe ni mmoja wa watoto wa makada wa CCM ambae ameweza kusimama na kubaki kwenye upinzani daima. Je ni kutokana na kutokuwa na njaa? Ni kutokana na yeye kuweza kufanya biashara zake bila kutegemea mzazi hivyo kuweza kuwa na mawazo binafsi? Au ni influence ya Mzee Mtei?
Kikubwa zaidi ni kwamba hakuna mtoto wa kiongozi wa ccm anayeweza kuthubutu kwenda kinyume na baba au mama yake. Kwa nini? Uoga na unafiki!
Unafiki unawasumbua hao! CCM ina wenyewe muulize Bashe Hussein Bashe
Adam na Eva walikuwa wana wa Mungu hapo Mwanzo. Walipotaka kuwa kama Baba yao yaani Mungu, ndiyo mwanzo wa mauti, taabu, shida, chuki, udini, ukanda, ukabila n.k ambavyo tumerithi mimi na wewe.
"Mtoto amuleavyo ndivyo akuavyo". Binafsi sioni kwa nini wote uliowataja wasiwe wanasiasa na viongozi. Ni haki yao kikatiba ni hii nchi ni yetu sote.
cdm nayo ina wenyewe muulize zitto kabwe
Uko hivyo ulivyo kwa sababu kadhaa na miongoni ni hizi zifuatazo:
1. Wazazi wako
2. Sehemu na wakati ulikozaliwa
3. Shule ulizosomea, ikiwa ni pamoja na fani yako
4. Exposure yako
5. Unafanya nini na ni zipi jitihada zako juu ya hali ulionayo
5. Ndoto na chaguo la maisha yako
6. n.k
Wako watu wengi wamezaliwa familia za hali ya chini sana, lakini wameibuka na kufanikiwa aidha kwenye medani za siasa, elimu, biashara, muziki n.k
Pia wako watu wengi sana wa watu waliokuwa mashuhuri na wasomi wakubwa lakini wameishia kuwa wavuta bangi na walevi wakubwa.
Rai yangu: Akina Nape, January, David, Hussen n.k tutakuwa hatuwatendei haki tunapowasema vibaya juu ya success yao katika medani za siasa hapa nchini. Ebu soma profile ya Mh. January kwenye website yake, uone alivyo smart...Ukweli, ata lile wazo la kupost profile yake kwenye mtandao ni kuonyesha inajibidiisha. Fuatilia kwa umakini ata mawazo na posting za watu hapa JF utaona baadhi yetu tuko weak kwenye mijadala. Soma rambirambi za Mh. Zitto kwa aliyekuwa M/Kiti wa CDM Shinyanga, utaona Mh. Zitto ata asingekuwa Mbunge bado mchango wake kwa jamii ungeonekana tu. VIJANA TUJIBIDIISHE POPOTE TULIPO NA TUENDELEE KUFANYIA KAZI NDOTO ZETU KWA UMAKINI, ONE DAY YES!
Una maana gani kwa hili swali lako la pili? si umesema mwenyewe kuwa Freeman Mbowe ni mmoja wa watoto wa kada wa CCM?