Mimi ni mwanaCDM ila bila kutafuna maneno Tabora ni pagumu sana,tuingie Igunga siyo kwa ajiri ya kushinda bali kukijenga chama kwanza alafu ushindi baadae
Nayasema haya si kwa unafiki wala kwa kubahatisha,mfano1 ni pale Dr.Slaa alipokuja Tbr mwezi wa 4 akiwa na akina Mpendazoe,tuliona kama wameelewa somo lakini wiki1 baadae mpaka leo navyoongea si rahisi kuiona bendera ya CDM kama zinavyoonekana za CCM na CUF,si soko kuu,si bus stand,si mtaani,si kokote pale ni vigumu sana
kwahiyo kwa sasa tukubali kwanza kufanya yafuatayo:tuwape dozi ya kutosha ya elimu ya uraia na pili,tuwafanye wawe na ujasiri wa kujisimamia kwa maana Wanyamwezi ni waoga mno mno mno,wanawaogopa watawala kuliko bomu la nyuklia