Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Watu wawili wamefariki dunia baada ya basi la Kampuni ya Mallesa walilokuwa wakisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda mkoani Geita kugongana na lori la mizigo katika Kijiji cha Rumasa, Wilaya ya Chato mkoani Geita.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Safia Jongo, amezungumza na TBC Digital kwa njia ya simu na kuthibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Watu walioshuhudia ajali hiyo wamesema imetokea majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo, Oktoba 7, 2025.
Lori la mizigo lililogongana na basi hilo lilikuwa limebeba vifaa vya ujenzi na lilikuwa likisafiri kutoka mkoani Mwanza kuelekea wilayani Kibondo mkoani Kigoma.