LIM ni bus zuri sana..wana semi luxury ambayo ni uhakika..
Abood na BM luxury zao wanaingizaga hiyo route in case yale manganga yao yameroga..
Maana Abood na BM route zao main ni Dar - Moro ndo wanakopeleka gari zao Luxury..
So dandia LIM chap kwa 25k tu..
Ukitaka kufika salama raha mstarehe, kiyoyozi na kelele za muziki - BM
Ukitaka kufika ukiwa hoi bin taaban, joto kali na upepo wa moto, kejeli na vijembe toka kwa wahudumu wa bus - Abood Bus
Ukitaka kulala popote njiani au kuhamishiwa kwenye mabasi mengine (kufaulishwa) - Hood
Yapo mengine nayaona - ila nenda Msanvu stand kajifunze juu ya huduma zao kwa kusikiliza kauli na mapokezi kwenye booking office zao ndipo utapata picha ya safari itakavyokuwa