Bashe, Zitto, waibuka wabunge bora 2015/2016

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,400
Nyota ya wabunge vijana Hussein Bashe wa Nzega Mjini, na Zito Kabwe wa Kigoma Mjini wamekuwa wabunge waliofanya vizuri katika bunge hili kwa hii mikutano 3 (tokea November mwaka jana).

Hayo yamasemwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya kufatilia mienendo ya kibunge kwa nchi za madola Ndg. Melkiory Tungaraza (CMPTSA). Mkurugenzi huyo kasema baada ya kufatilia kwa makini, jinsi ya kuibua mijadala, uwezo wa kujenga hoja, kukosoa kwa hoja, Bashe na Zito wameibuka kidedea. Huku Bashe akipata alama 8/10,Zitto alama 7.8/10, na Tundu Lisu alama 7/10.

Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa taasisi hiyo kasema kitendo cha bunge kutoonyeshwa Live sio sawa kwa wananchi, huku asilimia 89.3% wakilaani kitendo hicho. Na pia, Mkurugenzi huyo kaonyesha hali ya wabunge wengi hasa vijana kuathiriwa na hatua hiyo.
 
Yaani mbunge apimwi kwa kutekeleza ahadi katika jimbo lake na kuwatumikia wananchi, kuibua mijadala na kujenga hoja bungeni ni bora kuliko wananchi maskini ambao wanaendelea kugonga nyundo kwa machozi, jasho na damu huku wakisubiri majibu ya ahadi.

Kuna mahali hatutumikishi usomi wetu vyema na ndio maana hizi sinema hazitoisha na wananchi wanahitaji 50 more years kupiga hatua Zaidi.
 
Kuna taasisi fulani (jina nimelisahau) wametoa chati ya wabunge bora katika kipindi cha kuanzia Nov mwaka jana hadi June mwaka huu. Wabunge bora kwa mujibu wa taasisi yao ni: 1. Goodluck Mlingwa 2. Agnes Marwa 3. Lusinde Livingstone (Kibajaji)
 
Back
Top Bottom