Bashe: Mazao ya Mkulima sio mali ya Umma, Waachwe wauze popote

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Nov 8, 2022
7,382
8,437
Hello mabibi na mabwana.

Serikali imesisitiza kwama Mazao ya Wakulima ni Mali Yao na Waachwe Wauze Popote kwenye soko.

Waziri wa Kilimo amesema kulikuwa na dhana kwamba mazao ya Mkulima ni Mali ya Umma na hivyo kumpangia utaratibu wa kuuza mazao yake, utaratibu huo Sasa umekomeshwa maana Kwa mda mrefu umemfanya mkulima kuwa maskini.

Asante sana Waziri Bashe na sie tunaendelea kuwakumbusha wale walalamishi wa bei kupanda kwamba Mvua zinanyesha waende shambani.

Tukutane Sokoni baada ya mavuno,

IMG_20230122_153935_176.jpg
Kama mnadhani mtaendelea kula jasho letu basi subirini awamu ya mataahira ndio waje wafunge mipaka na walifanya hivyo tutaacha kulima ziada Ili tuone mtakula nini huko Mjini..

Bashe Kanyaga twende tuko pamoja 👇

========

"Tuondokane na dhana ambayo imekuwepo miaka mingi ya kugeuza mazao ya mkulima kuwa mali ya umma, Mazao ya Mkulima ni mali yake ana haki ya kuchagua sehemu ya kuuza na sisi Serikali tutamruhusu mtu yoyote kutoka popote kununua mazao ya kilimo.

Sisi Serikali kama tunayataka tutaenda kuyanunua kwa bei ya soko pia tutachukua hatua kuhakikisha analindwa. Kwa muda mrefu nchi yetu imewafanya wakulima kuwa masikini kwa manufaa binafsi."

Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo akizungumza na wanahabari kuhusu maendeleo ya kilimo, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 
Hakuna tatizo na mkulima.

Tatizo linatokana na Serikali yenyewe. Kwa hiyo asilifanye hili kuwa ni jambo jipya.

Serikali haiwezi hata siku moja kujiondoa katika shughuli yoyote inayofanywa na wananchi wake.

Huo ni uongo, ni kutafuta sifa za kijinga.
 
Bashe hapo tu ndio Huwa nakukubali. Kuzuia mkulima kuuza mazao anavyotaka iliondoa morali ya kilimo kwa watu wengi sana na ndio maana vijana wapo tayari wauze hata pipi mjini kuliko kujishughulisha na kilimo. Pambania hapo kwenye pembejeo tu mh. Bashe. Utaleta mageuzi makubwa kwenye kilimo. Waliomjini wanaosubiria mkulima alime waje wanunue kwa bei wanayotaka wewe waache tu watajifunza
 
77455E4F-0D47-4566-8A4B-2CA4BC012FED.jpeg



Hakuna serikali inayotaka kuumiza watu wake hasa wananchi ambao gdp per capita ni chini ya $1000.

Ndio shida ya watu waliokariri badala ya kuelewa hata kwenye free market serikali inajukumu la kumlinda mlaji.


Ni watu ambao hawana huruma na wananchi wanaowaongoza, na elimu ya kukariri.

Anyway baadhi ya watu walishaonya toka akiwa back bencher awamu ya tano. Huyo bwana ni mropokaji tu siku akipewa nafasi na kuruhusiwa kufanya anayohubiri ataumiza wenye kipato kidogo.

Uwezi kukopi sera na nchi zenye gdp per capita $20000 plus bila ku amend kwa mazingira yako utaumiza watu na hata wao free market hawazui food import ili kulinda wakulima. Wewe ata chakula kuagizwa utaki.

Katika mawaziri wote January Makamba pekee ndio alie elimika not necessarily ana elimu kubwa (still bozo). Hila zwazwa huyu kwenye shida jamii ikimwambia huko siko anapima merit za hoja na ku tweak approach yake.

Sio huyu Bashe jitu kama robot mjomba watu wanaumia na bei za chakula do something aelewi somo.
 
Hakuna tatizo na mkulima.

Tatizo linatokana na serikali yenyewe. Kwa hiyo asilifanye hili kuwa ni jambo jipya.

Serikali haiwezi hata siku moja kujiondoa katika shughuli yoyote inayofanywa na wananchi wake.

Huo ni uongo, ni kutafuta sifa za kijinga.
Amesema Serikali inajiondoa kwenye kukandamiza wakulima na si vinginevyo
 
Mkulima Gani anayenufaika na ongezeko la bei...?! Wakati walanguzi humulangulia mkulima pindi avunapo Kwa bei cheese.....! Aende vijijini akaulize kama kuna mkulima mwenye akiba hata ya debe mbili alizolima yeye.......
Kwani mlanguzi umesikia akilangua zile bei za awamu ya 5 za 20,000-30,000?

Acha walangua maana wakija na bei ndogo kabisa msimu wa mavuno ni 40,000-70,000 kutegemea na bei ya soko la zao husika huko Sokoni..

Halafu miaka hii kuna mawasiliano ya simu na Barabara Vijijini kote hakuna unaeweza mlalia bei kama zamani.

Mwisho wakulima sio wajinga kama zama zile nao wanauza kiasi na wanaweka kusubiria bei,mfano Mimi mkoani kwangu mazo Hadi daikika hii mipunga Inatoka Vijijini kuja mjini na ni hao hao walanguzi wa kati ndio wanaleta Sasa unadhani wanalangua Kwa bei za hovyo kama za awamu ya 5?
 
Ruzuku kwenye pembejeo mfano mbolea ya ruzuku inapingana na kauli yake. Pesa ya umma ikitumika popote hukigeuza kitu husika kuwa partly mali ya umma kwa uwiano wa pesa iliyowekwa.
Amesema Serikali inajiondoa kwenye kukandamiza na kuwafukafisha wakulima badala yake inajikita kwenye kuwainua Kwa mbolea ya ruzuku nk..

Na hapa ndio kuwalinda nyie walafi wa Mjini vinginevyo ingeacha wakulima wangelima msosi wao tuu harafu nyie mkome huko Mjini Kwa bei kupaa mara mbili ya Sasa.
 
Suala la Chakula linahusu moja kwa moja Usalama wa Taifa, sasa ngoja waletee siasa tu.
Mwaka huu, wakulima walifurahia kuuza mahindi kwa mia 500 kilo, wakati huu ndio haohao wanaolalamikia bei ya unga 2000.

Kupanga ni Kuchagua.
 
Amesema Serikali inajiondoa kwenye kukandamiza wakulima na si vinginevyo
LOOoooh!

Kwa hiyo kuna raia wanakandamizwa na Serikali? Hao wakulima ndiyo leo wamegunduliwa kuwa wanakandamizwa?

Kwa hiyo, hawa raia wengine watakaoshindwa kupata mlo kwa kutoweza gharama wanazozitaka wakulima, na wao wajihesabu kukandamizwa na serikali, au siyo?

Sasa sijui wao wafanyeje?
 
Mkulima Gani anayenufaika na ongezeko la bei...?! Wakati walanguzi humulangulia mkulima pindi avunapo Kwa bei cheese.....! Aende vijijini akaulize kama kuna mkulima mwenye akiba hata ya debe mbili alizolima yeye.......
Hata kama ingekuwa kweli kuwa wakulima ndo wanauza mazao, haifai mazao yauzwe nchi za nje bila mkakati wowote. Anafikiri kwa nini ngano ya Ukraine haiuzwi kiholela licha ya nchi kuwa vitani?
 
Back
Top Bottom