Tahadhari mnaosubiri barua za utumishi kwani nimekutana na issue 2 live.
Kwanza: kuna jamaa 2 walishinda interview wakaambiwa wasubiri wiki2. Baada ya wiki wakaenda kwenye ile taasisi wakajitambulisha. Aliyewapokea akasita baadae akaamua kuwasaidia baada ya kuangalia barua za utumishi zilizotumwa kwao na akawatolea nakala. Kwa mshangao wakakuta majina ni yao ila anwani sio zao. Application zao zilikuwa na anwani za shinyanga ila barua zilikuwa na anwani za Arusha ikimaanisha barua zisingewafikia kabisaaaa. Baada ya wiki 2 waliripoti lakini walipigwa danadana mpaka jamaa 1 akawaambia ukweli kuwa nafasi hizo zilikuwa na wajamaaa ndani ya taasisi ila walishindwa interview hivyo wakala njama na utumishi ili jamaa wasiripoti.
Ujumbe: hakiki anwani waliotumia kukutumia barua utumishi na ulikopangiwa. Usilale kusubiri kwenye sanduku.
Mbona sisi wa weight and measures agency tulipigiwa simu na kwenda pale utumishi kuchukua barua then tukariport kwa mwajiri? Jaribu kwenda utumishi kama uko dsm
Hata mimi nilipita kwenye sanduku la posta nililoandika la home sikukuta barua ingawa waliandika tayari zimetumwa, nikampigia jamaa wangu mmoja pale sekretatiat ya ajira akaniambia bora niifuate kule kule nisisubiri kwenye s.l.p na kweli nimeshachukua na kureport kwa mwajiri. Kwa kweli fuateni ushauri uliotolewa na wadau humu ndani zifuateni kule ofisi zao maktaba wakuu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.