Barua ya Wazi kwa Uongozi wa Baraza KUU la CUF Taifa

5525

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
5,412
6,279
BARUA YA WAZI KWA UONGOZI WA BARAZA KUU LA CUF TAIFA.

Waheshimiwa, uongozi wa Baraza Kuu CUF Taifa kwa heshima kubwa kabisa Amani iwe juu yenu.
Barua hii ya wazi inatoka kwa wapenzi na wanachama wa CUF visiwani Zanzibar badala ya kusoma na kusikiliza maazimio ya chama kutoka kwa viongozi Wakuu wa Chama Cha Wananchi CUF Juu ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar kutangaza uchaguzi wa marejeo March 20, 2016.


Kwa kweli tuna huzuni, majonzi na mskikitiko makubwa juu ya dhulma inayofanywa na inyoendelea kufanyika juu Haki ya wazanzibari walioiamua Dec 25, 2015 kuporwa.

Madhumuni hasa ya barua hii ni kama ifuatavyo:-

1. Kutokana na maamuzi ya tamko la Baraza Kuu la CUF Taifa lililotoka leo tarehe 28.1.2016 likiwa ni pamoja na CUF kutoshiriki uchaguzi wa marejeo March 20 mwaka huu, Je ni vipi mustakabali wa Wazanzibari na haki yao ile ya maamuzi Dec 25, 2015? Katika tamko lenu hatukuona ata mstari mmoja unaosomeka ni nini CUF itafanya kudai Haki hiyo kwa vyovyote vile.

2. Tunaelewa kwamba uchaguzi wa marejeo ni uchaguzi haramu na CUF kwa mujibu wa tamko la Baraza Kuu haitashiriki ni upi mustakbali wa CUF iwapo CCM Zanzibar watapiga uchaguzi na kuzoa viti vyote vya uwakilishi na udiwani Zanzibar?.

3. Baraza kuu CUF limezingatia kiasi gani iwapo wawakilishi kwenye Baraza la Wawakilishi wote watakuwa ni CCM baada ya kuwatangaza washindi wa uchaguzi huo wa marejeo? Vipi kuhusu sheria za nchi na Katiba itafumuliwa kiasi gani pale Baraza la Wawakilishi ilenge maslahi ya CCM na KUUA UPINZANI KWA MIAKA YOTE YA MBELE IJAYO.

4. Kama CUF haitaishiriki uchaguzi ni Wazi Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoongozwa CUF itakuwa haipo madarakani vipi hili mbona hatukuona mustakbali wa jambo hili muhimu?

5. Wakati wa kampeni za uchaguzi tuliwasikia viongozi mbali mbali wa juu wa CUF wakisema endapo CUF itashinda na CCM wakajaribu kupora ushindi wa CUF nguvu ya Umma itatumika kwa mujibu wa hili tamko la leo kwanini hatukuona hili azimio kuhusu nguvu ya Umma hapo baada mazungumzo kukwama na sasa baada ya kuwa na uhakika kwamba haki yetu inaelekea kuporwa.

6. UKAWA tulishirikiana kwenye mbio za kampeni Tanzania nzima ni kwanini Ukawa hakuna tamko la pamoja la kuunganisha nguvu ya umma kudai haki ya Wazanzibari kwa vile CUF ilishinda Uchaguzi Zanzibar na CUF ikiwa ni mdau mkubwa wa Ukawa? Kwanini Baraza Kuu la CUF katika matamko yenu hatukisikia mukigusia hili angalau tukapata mwanga kuhusu haki ya wazanzibari na watanzania kwa ujumla.

7. Baraza kuu la CUF kwanini hamukueleza kuhusu kufungua kesi Mahkamani kuzuia uchaguzi badala yake mumelani uchaguzi wa marejeo lakini mbona hamukuonyesha hatua ambazo mutazichukua kuzuia uchaguzi haramu na Wazanzibari kupata haki yao.

8. Pia tunapenda kueleza baada ya tamko la Baraza kuu la CUF watu wengi baada ya kusoma hili tamko wamevunjika moyo sana kwa hatua za viongozi zilipofikia hatukuona muelekeo kwa wananchi nini wafanye au kuwe na msimamo gani badala ya kuwataka wasishiriki uchaguzi wa marejeo. Watu wana wasiwasi mkubwa sana na hofu kila siku za uchaguzi zikikaribia kwanini Baraza Kuu CUF hamukueleza hatua ili kuona matumaini ya Wazanzibari walio wengi yanarudi na Haki yao inapatikana kwa garama yeyote ile.

Ni matumaini yetu makubwa sana barua hii itawafikiwa walengwa na kupata majibu ya maswali haya kwa niaba ya Wazanzibari mapema iwezekanavyo.

Tunatanguliza shukurani.

Wabillahi Tawfiq.
 
Back
Top Bottom