Abdul Nondo7
Member
- Feb 22, 2017
- 9
- 25
Ni muda mrefu sasa Tanzania tumekuwa tukipiga sarakasi juu ya suala la ajira kwa vijana tumekuwa tukitengeneza sera nyingi juu ya masuala ya vijana bila kutekelezeka (policy implementation gap) leo Naomba kuweka wazi juu ya uhamnazo tulio nao ndani ya taifa hili na viongozi wake.
Kwa mujibu wa taasisi ya integrated labour force survey mwaka 2014,inasema asilimia 57.3,ya popoulation nchini Tanzania ni nguvu kazi ya vijana ambao wengi wao hawana ajira, na hii imekuwa ikiongeze mwaka hadi mwaka, Jambo kubwa la kushangaza ni kuwa viongozi wetu wamekuwa wazito na wasio na mikakati ya weledi kupambana na suala la ajira kwa vijana ni taifa la viongozi wa kutunga sera, kuitekeza wenyewe na kujitathimini wenyewe (self monitoring and evaluations).
Bahati mbaya wamekuwa wakitengeneza sera nyingi zenye kukata matawi na sio shina la tatizo la ajira kwa vijana, suala la ajira kwa vijana ni (problem tree) lazima Shina na mizizi yaondolewe sio Matawi Kama ambavyo mmekuwa mkifanya ,sera ya mwaka 2008,ya ajira haikujibu, hata hii pia rasimu yake inakata matawi sio Shina la tatizo la ajira kwa vijana. Na viongozi wapo tuu bila kuwa na
Mikakati yeyote endelevu, na yenye kuzaa matunda kwa vijana.
*hatutaweza kutatua tatizo la ajira bila kutumia njia hizi*
1.tunapaswa turekebishe mfumo wa elimu yetu, elimu yetu inamtengeneza mhitimu awe tegemezi wa kuajiriwa sababu Hana kanuni za kujiajiri,pia kutokukidhi katika soko la ajira sababu ya ujuzi unaokinzana (skills mismatch),hii ni kwa Mujibu wa baraza la vyuo vikuu afrika mashariki(interuniversities council for east Africa). Tanzania asilimia 61 ya vijana waliohitimu Chuo hawawezi shindana katika soko la ajira, hii ni hatari saana, pia wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne ni wengi wanaoanguka na kubaki mtaani huku Elimu walioipata kutowapa ujuzi wa kujiajiri, tulipofikia tunahaja ya kurekebisha mfumo wa elimu yetu.
2.tatizo la kodi nchi hii haina mipango yeyote kwa vijana Faraja ya kodi hata kwa kijana ambaye anaanza kujiajiri, tunatambulika kimataifa kuwa Tanzania tuna utitiri wa kodi, nchi Kama China huwa inatoa tax holiday kwa vijana ambao wanaanza kujiajiri ndani ya miaka 3,hii inafanya vijana ventures zao kukua na kufikia malengo, ila Taifa hili linaubiri kujiajiri bila mkakakati matokeo yake hutoza kodi hata kwa vijana wanaoanza hivyo ventures/bussines zao kufa lazima tutoe msamaha wa kodi hata kwa miaka mitatu kwa wanaoanza biashara ili tuvune biashara zao zikiimarika ni faida kwao hata kwa serekeli kuendelea kupata kodi baada ya miaka hiyo mitatu ya msamaha.
3.lazima tuige mfumo uitwao *A working career shift or caree change* katika sector za umma hata binafsi mtu aajiriwe baada ya miaka 10 au 15 atoke akajiajiri yeye mwenyewe huu ni mfumo uliopo ujermani,
hii hufanya mtu ajue kujiwekea akiba ya kujiajiri baada ya kuajiriwa, pia tayari anakuwa na maarifa, na mtaji hivyo hurahisha ambao hawana ajiraa kuchukua nafasi.,na wenyewe hufanya wakijua watatoka huu ni mfumo imara wa kutatua tatizo la ajira, lakini waliopo serekali na katika ajira hawatapenda kulisikia hili, kila mtu ni interprenuer in nature sababu utastaafu, Hapa tuu mfumo huu ni bora zaidi. Kuliko mtu kuzeekea akiwa ameajirwa huku akipiga kelele *vijana changamkieni fursa*huku hazuonekani
4.tuachane na mambo ya uzoefu au experience,tuige mfumo wa *job training*,tuwaajiri tuwape mafunzo wakiwa kazini hii itasaidia saana kuondokana na kisingizio cha experience (uzoefu),suala la internship /volunteerism (kukuza ujuzi) ndio iwe kipimo cha kumuajiri mtu,impact aliyoleta ktk internship hiyo sasa hivi internship na ajira havina mahusiano watu wanafanya tuu,report will never be considered .mfano. *Cambridge development initiatives*huu ni mradi wa wanafunzi wa chuo cha Cambridge ambao huwa wanakuja Tanzania dar, hujanya miradi minne kwa mwaka ambapo inatathiminiwa na report huchukuliwa ndio inayotumika kuwaajiri ktk taasisi za umma hata binafsi kwa kile walichofanya katika jamii ya Tanzania ,sisi tumekaa bila mikakati yeyote.
5.tuwe na baraza litakaloratibu masuala yote ya vijana sio baraza la vijana wa chama baraza la utekelezaji masuala ya vijana ndani yake tuwe na idara ya kusaidia vijana wenye mawazo (ideas) , mfano. Uingereza wanalo baraza linaitwa national youth council ndani yake wana *the young change makers* (YCM), ambapo vijana wote wenye mawazo hupewa msaada kuendelezwa, na kufikia malengo yao Tanzania tuna vijana wangapi Wenye mawazo, ya kufanya mambo makubwa lakini hawaendelezwi, na uwezo wao kufa. Na ndoto zao kupotea sababu hawajui waende wapi.
Na hii hufanya hata fursa za ajira ktk nchi bilatateral au multilateral zisijulikane sababu Hakuna chombo cha kuonganisha vijana, Rwanda imerasimisha kiswahili kuwa lugha ya taifa, Hakuna wizara yeyote inayohusika inayopiga debe wahitimu wakiswahili wakafundishe, na vijana wanajiuliza waende Wapi kiswahili kinafundishwa na wakenya,. Ukienda wizara ya mambo ya ndani nenda wizara ya elimu wizara ya elimu unaambiwa Hakuna hilo tangazo yaani nchi tupo tupo.
6.suala mikopo kwa vijana, ni mambo ya kushangaza serikali kuu kupiga kelele halmashauri itenge fedha makusanyo asilimia 5 kwa vijana, ndugu zangu halmashauri utoaji wa fedha hizi ni mgumu sababu hutegemea makusanyo ya fedha makusanyo yakiwa madogo asilimia 5,ya vijana haitolewi sababu ya itaathiri shughuli za maendeleo ile asilimia 60 ,mfano kutokana na makusanyo inaweza patikana mil. 5 haitoshi kwa vijana woote hivyo, mkono wa serekali kuu unahitajika, pia halmashauri *ziitumie mifuko ya hifadhi ya jamii* kwa kuweka hiyo fedha ya vijana alafu mifuko hiyo itakuwa ikizungusha fedha zao na kuwapa mikopo, Kwa faida.
7.tusiwadanganye vijana kusubiri viwanda kana kwamba wanasubiri basi kituoni, hadi sasa kabla ya hivyo viwanda (promised industries), sekta ya viwanda imeporomoka ndani ya mwaka mmoja, uzalishaji viwandani umeshuka, bidhaa zumeshuka ubora na kukosa soko na kusababisha hasara ya $272,ml.tsh, sawa na 600 bilion source *the citizen* hivyo tunapotabiri viwanda tuangalie na hali tulionayo ili kuchukua hatua maridhawa kwa vijana juu ya ajira. hii kwa sisi tunao soma political science tunaita *trend extrapolation* ambayo inatupa mwanga kutabiri yajayo kutokana na hali iliyopo, kwa kuporomoka hivi uzalishaji na ukilema tulionao katika kuchukua hatua za kibunifu, naona uhaba wa matumaini mbele kwa vijana hatua stahiki zinahitajika, kuokoa jahazi la vijana.
8.tuachane na makundi makundi kwa vijana tuwe formal tuunde Interprisises tupunguze mlolongo mrefu wa usajili wa makampuni hii itasaidia kuondokana na vimakundi makundi unakuta mwaka, miezi mtu anasumbuka kusajili kampuni au interprisises, hadi anakata tamaa.
9.kuwe na taratibu wa kuu wa mikoa wote wa husike kufanya wajibu wa kupunguza tatizo la ajira kwa vijana na sio blaa blaa,
10.serekali isiwe inajifanyia monitoring and evaluation katika sera zake, kuwe na *independent consultants*( watu kutoka taasisi zinazojitegemea) , mfano, twaweza, hakielimu, wakifanya tathmin huwa ipo very critical.
Tukitaatua tatizo la ajira bila kuangalia *retreanchment*(ubanamatumizi na ubinafsi) serikali itafaidi kodi payee ambayo inachangia asilimia 25 ya mapato yote ya kikodi ya serekali,bodi ya mikopo haitatumia ubabe, hii ni ashirio kuwa taifa limekosa viongozi wabunifu.
Shukrani natumai ujumbe utawatawafikia na hatua za lazima zinapaswa kuchukuliwa ili kuokoa vijana na tatizo hili la ajira.
Imetolewa na
*Abdul Omar Nondo*.