Barua ya wazi kwa Rais Magufuli juu ya hali ya gereza la Mjini Bukoba

ANNA PENN

New Member
Feb 15, 2016
3
0
Barua hii imetumwa wazi kwa Mheshimiwa, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu mawasiliano ni marufuku.


Mimi naandika barua hii nikihusianisha na mauaji ya ARNOLD AUGUSTIN katika gereza la Bukoba tarehe 21.2.2016, baada ya kukosa dawa kwa matatizo madogo ya kiafya kutoka hospitalini.

Arnold Augustin sio mhanga wa kwanza aliyefariki katika hali hii, bali ata wafungwa wote waliobaki maisha yao yapo katika hali ya hatari dhahiri, baada ya uongozi wa magereza kukataa wahanga kupata dawa na matibabu, bali baada ya kuzidiwa sana, hupelekwa hospitali kuepusha kigezo cha lawama kwao, kuwa ndio wamepelekea vifo hivyo.

Kwa makadilio vijana wadogo (17) walifariki kwa tatizo hili mnamo mwezi wa pili 2014 katika gereza la Bukoba tu. Na wengine tofauti wamepoteza maisha yao katika magereza mengine nchini Tanzania kutokana na mfumo huu wa viongozi hawa wa magereza.

Wakuu ya magereza huulizwa kwanini wahanga hawapatiwi dawa na matibabu mapema, bali upelekwa hospitali wakiwa mahututi zaidi. Jibu lao ni kuwa misaada ya kimataifa kwa Tanzania imekataliwa. Kauli kama hii ni ushaidi tosha wa mauaji haya,na inaelezea nia nyuma ya udhuru kwa sababu hospitali zote ya serikali hutoa dawa kwa kuuza. Dawa hutolewa kwa wale wanaowahishwa hospitali mahututi, ni ghali zaidi kuliko kama wange litibiwa kabla ya kulazwa hospitalini.

Alisema baada ya mawazo na maafisa wa magereza kwa ni ugaidi wa kidiplomasia dhidi ya raia, kwa msaada wa kimataifa kama ilivyoelezwa. Misaada hii haiwafikii walengwa hali inayopelekea, mauaji ya makusudi ya wafungwa wa mahabusu kwa kukataa kupatiwa dawa na matibabu, hali inayowafanya kupata hali mbaya zaidi, na kupelekwa hospitali wanapozidiwa sana kama matokeo ya kuepuka kifo gerezani.

Kwa niaba ya watu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, swala hili ni kuletwa mbele ya Mweshimiwa Raisi, kwa ajili ya kuchukuliwa hatua. Tunaomba maofisa wote wa magereza watumiao mfumo huu unao sababisha vifo vya raia wa Tanzania, waadhibiwe kwa ukali mbele ya macho ya Taifa lako, na wale wanaougua magerezani wapelekwe hospitalini mapema, na vyema kupatiwa dawa magerezani.

Maisha marefu na utawala, viwe kwako Mweshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
....misaada ya kimataifa kwa Tanzania imekataliwa. unamaana gani katika hii sentensi!
 
Nina taarifa kuwa wafungwa wengi wanaoishi na ukimwi wanakufa kwa wingi Sana kwa sababu jeshi la Magereza linapata bajeti duni Sanaa ,kuweza kubuni kununua madawa na lishe ,,..Hali ni mbaya Magereza mikoani kiasi imefikia mahala huwezi tofautisha Kati ya Askari na mfungwa ..wote wamechakaaaa......kitambulisho cha Askari ni bunduki yake
Wako Askari ambao Wana miaka mitano hawajapatiwa mgao wa mavazi.....hili tatizo aliloacha jk .....JPM alishughulikie haraka
 
Muandishi jaribu kulirudia bandiko lako maana kuna vitu haviko katika mtiririko mzuri...lakini hiyo sababu walioitoa hao maafisa wa Magereza kama ni kweli hai make sense ..je ni kweli wali address matatizo yao kwa government ikagoma kuwasaidia? Ila kwasasa tunae JPM ni mfuatiliaji atalifanyia kazi hili maana najua anapitia hapa kama sio yeye basi wasaidizi wake
 
Mr president ebuanza n.a. hili kwani damu ya watu wako inamwagika wakati ingeweza tibika,kila lakheri my president
 
Back
Top Bottom