Mwanzoni nilidhani ni utani, ila mpaka nilipokuja kuiona picha ukiwa ndani ya shela na tabasamu kubwa lisilo hata na tone la huzuni moyo wangu uliumia sana. Nikaanza kutafakari toka mbali kwa niliyoyaona na kuyajua mwenyewe achana na yale ambayo nilikuja kusimuliwa, kwa sababu safari ya urafiki wenu imetoka mbali sana ni zaidi ya miaka 11 hivi tangy mlipofahamiana. Nakumbuka mara ya kwanza nakutana na rafiki yako mpenzi, alinisimulia mambo mengi mazuri na yenye kutia moyo.
Ambayo kwa kiasi kikubwa yalinishawishi hata mimi kuitwa mume. Nakumbuka tulisheherekea vizuri sana siku ile ya harusi yangu kwa furaha kubwa na uhakika usiokuwa na chembe ya kwamba hichi ninachokiona kitakuja kutokea. Nikawakabidhi kijiti mlikuwa wawili wewe na rafiki yako wa siku nyingi na pia alikuwepo rafiki yangu mwingine kupitia mke wangu ambao wao kwa heshima kubwa walitimiza ahadi waliyokuwa wameniahidi siku ile ya ndoa yangu. Ila wewe sijui ni nini kilitokea mpaka yakatokea haya.
Katika hili lililotokea kwako naungana na ule msemo unaosema historia haidanganyi, ni kweli historia haidanganyi. Waliokutangulia ndani ya ukoo wenu walishayafanya haya uliyoyafanya wewe. Aliyekutangulia aliacha mume bora, akaolewa na bora mume mwingine kwa sababu ya land lover ya enzi za mwalimu. Baada ya miaka kadhaa nadhani wewe ni shaidi hivi ile land lover bado ipo? Vipi kuhusu yule kaka ambae ukoo mlimuona kajamba nani leo je mafanikio aliyoyapata yanalingana na unabii wenu, wa kibinadamu unaoona leo wala hauyajui ya kesho?
Nayasema haya yote mpaka kurejea mifano hai kutokana na sababu ambayo familia waliitoa kumuhusu rafiki yako mpenzi. Aliyejitoa kwa kila kitu kwa ajili yako kuhakikisha tu unapata yote uliyohitaji, yeye akiamini kuwa hakuna hasara yeyote kumsaidia mke wake mtarajiwa. Kumbe rafiki yako huyu alikuwa anajipatia matumaini hewa ambayo hayapo. Nilijaribu sana kukushauri nini ufanye pale uliponiletea malalamiko kuhusu changamoto uliyokuwa unapitia nikiamini kuwa ulikuwa ni mwanamke shupavu unaeweza kusimama kutetea haki yako.
Masikini mimi nilishindwa kutambua kuwa kumbe tayari ulishakutana na mwajiriwa wa serikali. Mwalimu wa sekondari ambae wazazi wako walikuwa wanamtaka kisa tu ana ajira ya serikari. Walimkataa rafiki yako wa siku nyingi eti kisa yeye si mwajiriwa wa serikari, ni mwajiriwa wa secta binafsi, hivyo muda wowote anaweza kufukuzwa kazi hivyo akageuka kuwa tegemezi kwako.
Inasikitisha sana hii binadamu kugeuka kuwa ni watabiri wa maisha ya watu. Kinachonisikisha zaidi ni kuwa umeolewa na mwalimu kwa shinikizo la wazazi ila si kwa mtakwa yako. Hili maana yake nini? Maana yake ni kuwa hautakuwa na furaha na huyo mume. Kwa kuwa nafahamu hilo na wewe pia unalijua hilo, na hii dhuruma kubwa uliyomtendea rafiki yako wa siku nyingi itakuandama na kukutafuna maisha yako yote. Ipo siku utakuja kuwalaani wote waliosababisha ukaingia kwenye mkataba ambao haukuridhia kutoka moyoni. Waliokushawishi wao kwa sasa ni furaha tupu kwasababu masilahi yao wanayotegemea kuyapata na ambayo kiuharisia hawatayapata wamefanikiwa kuyalinda. Huyu rafiki yako wa siku nyingi yeye kwa sasa Ninachomshauri ni kuwa, akuchukulie kama amekupoteza katika ajari mbaya iliyowakumba, na wewe ukapoteza maisha. Hivyo hana budi kukusahau na kuzoea na hata wewe nakushauri pia umchukulie hivyo hivyo. Ingawa najua huwezi kumchukulia hivyo kwa kuwa umemtenda yasiyostahili. Mwenzako amekutendea mema wewe umemlipa mabaya. Ninayo mengi sana ya kukwambia kuhusu uchungu na masikitiko yangu. Ila najisikia nimechoka kuandika ngoja nipumzike. Ili nisiendelee kukuchosha kwa upuuzi wa masikitiko yangu nakutakia honey moon njema nitakutumia kumbukumbu zetu enzi zile za furaha yenu na yetu pia tulipokuwa na matumaini hewa juu yako.