Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Kwanza nakupa hongera kubwa kwa kuchaguliwa kwako kuwa Rais wa TLS baada ya kuchaguliwa kwako ni wewe tu ndio kiongozi makini na shujaa unaweza kuongoza chama cha upinzani katika harakati ya kukiondoa chama cha CCM madarakani katika uchaguzi ujao. Kwa hali sasa hapa nchini umaarufu wa CCM umeshuka kwa kiasi kikubwa na asilimia kubwa ya watanzania wamekataa tamaa na wanaendelea kukataa tamaa kuendelea kutawaliwa na chama hicho.
Ni wakati muafaka kwa wewe kuanza kutumia hekima yako katika kuunganisha vyama vyote vya siasa ili ifikapo mwaka 2020 tuwe na chama moja makini na chenye nguvu ili kuweza kupambana na CCM, kama ujuavyo CCM ni chama kinatumia mbinu ya kudhoofisha vyama vya upinzani kwa kuvigawa kama unavyoona kinachoendelea chama cha CUF na sasa tunaona ACT Wazalendo inavyotumika kuvuruga uchaguzi wa wabunge wa Afrika mashariki.
Tujifunze kutoka Kenya wakati wa kumuondoa Rais Moi harakati ziliendeshwa na wanasiasa wengi vijana na walitoka kutoka chama cha wanasheria wa Kenya mfano:
1. Marehemu Wamalwa Kijana 2. James Orengo 3. Martha Karua 4; Marehemu Mutula Kilonzo5, Kalonzo Musyoka. Hao niliowataja ni miongoni mwa wanasheria waliotayarisha makubaliano ya kuunganisha vyama vyote vya upinzani chini ya chama cha National Rainbow Coalition matokeo yake Mgombea wa chama hicho aliibuka kuwa Rais Mwai Kibaki na huo ukawa ndio mwisho wa utawala wa KANU wa miaka 30.
Mheshimiwa naona ni wewe kiongozi pekee unaongea na kuonyesha una nia dhabiti ya kuleta mabadiliko hapa cha msingi unatakiwa utoe ushauri kwa chama chako cha CHADEMA kuimarisha demokrasia ndani ya chama, na hakuna haja ya chama kiwe kimbilio ya wanasiasa kutoka CCM ambao ni miongoni mwa viongozi waliyoifikisha nchi hii hapa ilipo, juzi katika mahojiano yako na Mwananchi Media ulitamka kuwa vurugu zinazoendelea ndani ya CUF inaweza kuwa neema kubwa kwa upinzani nakubaliana na wewe kwa asilimia 100 hapo ndipo kuna uwezekano kuzaliwa kwa chama kimoja imara hapa Tanzania bara na Tanzania visiwani.
Mheshimiwa naomba usome waraka wangu huu na ufanyie kazi.