Barua ya wazi kwa Mh.Magufuli : Viiwanda ni nia njema ila watanzania tutakuangusha

EWGM's

JF-Expert Member
Jul 22, 2013
1,521
2,112
Mh. Magufuli natambua una nia njema sana na auchumi wa nchi hii na kutimiza ahadi zote za CCM. Viwanda ni moja ya njia sanifu itakayoweza kukuza uchumi wetu na kupunguza idadi ya wasio na ajira nchini. Marighafi tunazo, maeneo tunayo, sera safi tunazo, fedha tunaweza kukopa, tatizo ni rasilimali watu kwenye nchi hii ndiyo tatizo kubwa na usipokuwa makini tutakuangusha.

Tanzania ina watu zaidi ya Miliomi 45 na asilimia 75 kati hao ni vijana ambao ni tegemeo kwa taifa lolote katika kujenga uchumi wa nchi. Pia tuna idadi kubwa ya vyuo vikuu nchini kwa sasa ambayo inatoa vijana wengi waliohitimu masomo ya elimu ya juu. Mh. Magufuli vijana wetu wana vyeti vizuri sana lakini wenye vyeti wenyewe wanamapungufu makubwa sana kwenye vipawa, ujuzi na uwezo wa uwakilishi wa elimu zao.

Wengine wanasema elimu ya bure mliyowapa ni bure kwelikweli sababu wanashindwa kuwakilisha kile walichokisoma kwenye uhalisia wa uchumi wa dunia ya sasa. Kwangu kikubwa nachokiona ni “ignorance” na “attitude” ya kujiona wana vyeti vya elimu ya juu basi inatosha. Hawajui dunia ya sasa inataka vipawa, ujuzi na uwezo vya uwakilishi wa elimu uliyosoma kwenye uhalisia wa uchumi wa kisasa.

Wakishahitimu na kupata vyeti vyao basi wao ndiyo wao na wanajua kila kitu, ukishakuwa hiyo “attitude” kujiendeleza inakuwa ngumu sana. Vijana wetu ni kama sangara akimwekwa kwenye dimbwi basi tayari na yeye anajiona nyangumi. Kingine Mh. Magufuli ni kuwa wakishatoka kule madarasani basi kiburi na dharau “ignorance” kwenda mbele na bahasha zao za kakhi mitaani, hawajishughulishi na chochote wanachokijua wao kinatosha huku hawafahamu dunia haiku hivyo.

Wasomi wa miaka ya nyuma walikuwa wakihitimuu elimu ya juu na wakiwa na kadi ya uanachama wa TANU au CCM wanakuta ajira inawasubiri tayari. Hali ya sasa ni tofauti kidogo sehemu kubwa ya uchumi wa viwanda unaendeshwa na sekta binafsi. Pia teknoloji imefanya dunia imekuwa kama kijiji na nusu ya idadi ya watu duniani iko kwenye harakati za mizunguko ya kikazi. Kazi ikitangazwa leo Tanzania mtu wa mashariki ya mbali ana uwezo wa kuiona na kutuma maombi dakika hiyo.

Hivyo Mh. Magufuli napenda kumnukuu Nelson Mandela aliwahi kusema hakuna taifa litakalo endelea ikiwa raia wake hawajaelimika. Elimu anayoiongelea Comrade Mandela siyo ile ya bure na kuwa na vyeti tu huku uwakilishi kwenye uhalisia hakuna. Pia mwanarakati mmoja wa India aliwahi kusema “kama elimu haijaingia kichwani mwako na moyoni mwako na kubadili uwezo wako wa kutafakari, kufikiri na kutatua mambo kwa madhumuni na malengo mema basi hiyo elimu haina tofauti na joho ulilolivaa na kulivua siku ya mahafali”

Hivyo Mh. Magufuli kama hautaliona hilo basi kazi na nguvu zote unazoelekeza kwenye viwanda zitakuwa za bure sababu vijana wako watakuangusha. Wako tayari kutumia Mb za mabando yao kukesha kwenye magroup ya Whatsapp and Instagram kuongea yasiyo na maana wala maendeleo ya nafsi zao. Wako tayari kupoteza muda wao kujua kama Mama wa Diamond anajua kingereza au la? Wako tayari kupoteza muda wao kujua leo mwanamuziki gani ana ugomzi (beef) na nani?

Wasomi wetu hawa hawasomi vitabu, hawako tayari kujiendeleza, hawako tayari kufanya utafiti wapo wapo tu kutwa kuongelea ngono, umbeya na mambo yaisiyo na manufaa kwao. Na ndiyo hawa hawa unataka kuwapa dhamana ya viwanda, Mh. Magufuli tafadhali fikiria hilo kwanza sababu vijana wako hawa ni mizigo na haya siyo majipu ni matambazi. Pia wamegawanyika kwenye pande mbili; upande huu magwanda na upande ule nambari wani lakini wameshau kuwa wote ni Watanzania na taifa linawatemea wao.

Vijana wetu wanataka kufanya mambo makubwa wakati hataka madogo tu waliyonayo yanawashinda kufanya kwa ustaha na ufasaha mkubwa. Mh. Magufuli tatizo kubwa la nchi yetu ni rasilimali watu na nyinyi wenyewe mnatuonyesha kwa mifano hawa wasomi wetu tatizo. Mkitaka kujenga barabara injinia mnamtoa China, mkitaka kutibiwa lazima muende India kama hamna imani nao kwenye hayo mtawapa vipi dhamana ya viwanda hawa wasomi (vijana) wetu? Ni sawa na kuwa na gari lako la kasi la kifahari ukataka kuliweka mafuta ya dizeli ni lazima litakufa tu.

Hivyo nakushauri Mh. Magufuli sitisha kwanza viwanda na anza kuwekeza kwenye elimu ya juu mpaka pale itakapoweza kutoa vijana watakaoweza kupambana na ulimwengu wa uchumi wa sasa ndiyo tuanza kufikiria viwanda. Taifa hili haliko tayari kwa viwanda bado wana mengi ya kujifunza kwenye ulimwengu wa sasa na mpaka pale tutakapobadili “attitude” na kufuta “ignorance” katika vichwa vyao ndiyo tufikirie viwanda. Na Mwalimu Nyerere alishawahi kusema “it can be done, play your part”. Hii ndiyo nafasi yangu kuanza kukufungua macho kuwa huku kwenye soko la ajira kuna mabomu na watakuangusha hawa wasomi wa sasa.

Wako mtiifu kwenye soko la ajira Tanzania

S.L.P Dar-Es-Salaam

Kifupi EWGM'S ulichokisema ni changamoto za kujenga viwanda na elimu duni inayotolewa nchini: hayakufanywa maandali ya kutosha kabla ya kuja na wazo la viwanda.

Umesema vijana hawaelemiki ila wanahitimu madarasa. Mfumo mbovu wa elmu unatoa wasomi wenye matarajio kuajiriwa baada ya kuhitimu masomo umeandaliwa na kusimamiwa na nani kama siyo serikali?

Nakushangaa kurundika lawama kwa vijana wenye "bahasha za khaki" wanaoonekana mitaani kutafuta kazi za kuajiriwa. Acha kupotosha watanzania kwa maslahi binafsi. Serikali inafahamu kuwa kla mwaka vyuo vikuu vyetu hutapika wahitimu wa stashada na shahada ilihali hawana elimu ya kujitegemea.
 
MKuu umejaribu kung'ata na kupuliza ila ukweli utabaki pale pale wasomi wa miaka hii ni shida. Wakishakuwa na vyeti wanaona basi inatosha, hawajui kujieleza, hawajui kujiwakilisha, hawana ushawishi, wao wanategemea vyeti tu.

Cheti ni asilimia 40 ya ulichosoma ila asilimia 60 iliyobaki ni mwendelezo wako binafsi wa kila siku ili kukuza vipawa, ujuzi na uwezo. Mwajiri anatazama zaidi hiyo asilimia 60 na uwezi ukalaumu serikali kwa hilo inagawa mfumo wa elimu yetu ni m-bovu.

Hata serikali ikifahamu si ya kulaumiwa tuanze kujilaumu sisi wenyewe kwanza attitude zetu haziko sawa na mahitaji ya soko la ajira nchini. Makampuni mengi sasa ni ya kimataifa na yanataka kuwa na kiwango sawa cha uchapa kazi lakini ikishindwa kumpata afisa masoko nchini watakwenda Kenya, Uganda au Zimbabwe.

Wahitimu hawajiendelezi kukuza vipawa, ujuzi na uwezo , wapo wapo tu kutwa kwenye WhatsApp na Instagram kuongelea mama Diamond na Zari. Pamoja na wingi wao lakini bado hawatoshelezi mahitajia ya soko la ajira la Tanzania. Ndiyo maana tunaona Wakenya, Wazimbabwe na Waganda wanakuja kuchukua nafasi ambazo zingeweza kujazwa na wasomi wetu.

Sasa elimu ya kujitegemea ya nini wakati hawawezi hata kutoshereza nafasi zilizopo kwenye soko la ajira.
 
Kabla ya ku adopt hizo sera tungepitia kwanza dhana za Comperative advantage na competitive advantage.
 
Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100 ila jukumu still linabaki kwa wahitimu wenyewe wa elimu ya juu

Ili ku-adopt dhana ya Comparative advantage then individuals, firms and Nation as whole lazima wawe tayari.

Ila ukitazama Firms za ziko tayari ila ni individuals ndiyo wako nyuma ambao ni wasomi wetu
 
Back
Top Bottom