Barua toka tamisemi inapingana maelekezo na barua ya wizara ya elimu

ibesa mau

JF-Expert Member
Sep 17, 2015
2,109
1,697
Kuna malalamiko toka kwa wakuu kwa wakuu wa shule na walimu wakuu juu waraka uliotolewa hivi karibuni ikiambatanishwa na barua yake iliyotumwa mashuleni. Hizo barua mbili zinapingana. Barua ya awali iliyotumwa na wizara ya elimu inakatza wazazi kuchangishwa michango ya chakula hasa shule za kutwa na michango mingine. Wakati barua toka tamisemi inaelekeza maeneo ambayo serikali itachangia na barua hiyo inakataza wazazi baadhi ya michango huku ikishindwa kueleza wanafunzi wa kutwa chakula watapata wapi.

Mkanganyiko upo kwenye barua hizo mbili , elimu wanakataza mzazi kuchangishwa huku ikieleza michango yote aliyokuwa akitoa mzazi sasa itatolewa na serikali wakati tamisemi wao wameleta barua inayoelezea aina ya michango ambayo serikali itagharamia, katika barua hiyo haionyeshi kama serikali itachangia chakula shule za kutwa . Kuna baadhi ya wakuu wa shule za kutwa wamechangisha michango ya chakula na tayari wameandikiwa barua za demotion wakuu hao. Serikali ielimishe wazazi kwani hali ilivyo hivi sasa mzazi hataki kabisa kusikia habari za michango wanachojua wao ni kumnunulia mtoto viatu , shati, blauzia, suruali, au sketi basi.
 
shule za bweni serikali inatoa tsh. 1500 kwa siku na barua imeelekeza hivyo wakati shule za kutwa haijaeleza chochote .. eneo hilo linaleta mkanganyiko kwa wakuu wa shule na wazazi.
 
Back
Top Bottom