Barua kwa Rais Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

KATASAN'KAZA

JF-Expert Member
Jul 24, 2013
3,097
1,355
Ndg, waheshimiwa.

Wasalam, pole na shughuli nzito ya kuliongoza taifa letu.

Baada ya kuwasalimia naomba nitumie fursa hii ambayo kwangu naamini ndiyo fursa pekee ya kuwafikishia mawazo yangu kama kijana na raia mwema nchi wa nchii ya Tanzania.

Kabla ya yote nianze naomba Ku declare interest kuwa mimi ni muanga wa tatizo la ajira kati ya mamilioni ya vijana nchini na duniani kote.

Nikiwa ni mhimu wa chuo kikuu 2011 mpaka sasa sina kazi kwa maana ya kuariwa na serikali, kampuni au mtu binafsi.

Lengo la barua hii hasa nikutaka kidogo kwa ufupi ujue madhira yanayotupata vijana katika taifa pendwa Tanzania. Na haya ni matatizo yanayomsibu kijana katika nchi hii.

Mosi, Vijana hatuthaminiki na haminiki kwa serikali.

Lipo tatizo la kutothaminiwa sisi kama vijana na serikali, maana yangu ni kuwa muda wote wa uhai wa serikali ya Tanzania tangu tupate uhuru ni wakati wa awamu ya kwanza tu ambapo kijana alikuwa na umhimu kwa taifa. Na pia taifa liliona umhimu na thamani ya vijana katika kujenga taifa, rejea mashamba ya ushirika, viwanda, katika mfumo wa ujamaa mafanio ambayo mpaka leo ndiyo tunayoweza kujivunia tangu uhuru.

Pili, kuna lawama nyingi anatupiwa kijana wa Tanzania kuwa siyo wabunifu, wavivu na mengine mengi, lakini muda huohuo wanashindwa kuangalia mazingira na changamoto ambayo vijana wabunifu wanatakiwa kuishi, mazingira yana jumuisha aina ya elimu wanayopata vijana tangu msingi mpaka chuo kikuu je, inawandaa kukabili mazingira yalipo nchini. Mitaala na silabasi hazi akisi ata kidogo kumwandaa kijana kukabili mazingira. Rejea elimu ya ujamaa na kujitegemea.

Tatu, mfumo hauna sehemu maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya vijana. Hapa kwenye mfumo namanisha kuanzia siasa(maamuzi) sera hazina ushirikishwaji wa mambo mahususi ya vijana, rejea sera ya kazi haibainishi mipango mahususi ya ushughulikiaji masuala ya ajira na uwezeshwaji vijana katika kuchangia maendeleo ya nchi. Pia sera ya vijana nchini ipo katika makaratasi haina utekelezaji wowote wa changamoto za vijana.

Nne, kasumba ya viongozi kuwashambulia vijana bila ata kuwapa fursa ya kuwasikiliza; binafsi huwa najiuliza mnapata wapi ugumu kwa rais na viongozi wengine kutoa fursa ya kuwasikiliza mkaambiwa yanayotusibu kila siku tunasikia rais ataongea na wazee wa mahari fulani na hasa dar es salaam, kwanini msifanye hivyo kwa vijana pia. Tunayo mengi yanayotusibu tunatamani kuwaelezeni.

Tano, nipende kuwakumbusha kwamba hakuna maendeleo tutapata kama vijana tusipo pewa kipaumbele katika kutoa fursa za uwezeshwaji kwa vijana katika uzakishaji, spendi kuwatetea sana vijana wenzangu kwa kubweteka ila pia niseme kwamba wapo vijana walioweza kufanikiwa hasa wale walio kuwa na chanzo/msingi katika kuwekeza ingawa wengi wao ni watoto wa wakubwa ambao ni asilimia ndogo sana ya vijana nchini.

Mwisho nikuombe mh. Rais tusaidie haya yafuatayo kwa kuyapiga marufuku.

TOZO ZA MAZAO YA KILIMO TUNANYANYASIKA TULIOJITOLEA KULIMA.

KODI KWA BIASHARA ZA MITAJI MIDOGO.

UPATIKANAJI WA MIKOPO HASA YA PEMBEJEO, UWEJEZAJI MDOGO MDOGO.

Nilimalizie kwa kuomba tena fursa ya kukutana na mh. Rais na sisi vijana kukueleza madhira yetu kabla ya hatua ya kuanza kutuadhibu bila kutusikiliza.

Nikutakie utekelezaji mwema wa majukumu ya kuongoza taifa.

Wako; kijana wa Tanzania.
 
Safi sana. Mh. Rais ni mfuatiliaji nina hakika ataliona hili. Usikate tamaa nina imani na Rais wa Awamu hii akiahidi kitu atatekeleza. Labda tu wito kwa Waziri mhusika na suala la ajira aandae mkakati wa kutoa fursa za ajira au uwezeshwaji wa vijana katika maeneo mbalimbali!
 
Back
Top Bottom