Barrick wasimamisha mgodi.

Tatizo ni viongozi wetu na wabunge wetu, viongozi wanaandaa mswaada wa sheria bila kufanya study ya kutosha maadamu wanayoyafikiria yawemo kwenye sheria kama vile wao ndio wamekamilika basi huamini imekidhi, na wabunge nao badala ya kujadili wamebaki ushabiki wa vyma tu na kulala bungeni. Huyu Sijui Zambi alikuwemo bungeni na sheria ilipitishwa bungeni leo imeanza kusimamiwa ili itumike ipasavyo imesababisha kero kubwa sana kwa wazalendo. Geita GGM walikuwa na mtafaruku kama huu wakalazimika kumwita afisa wa SSRA naye amekiri kabisa kutokana na utaratibu wa kazi za migodini na makampuni yatowayo huduma migodini (subcontractors) na aina ya mikataba wanayoingia wafanyakazi bado wana lazima ya kuwa na haki ya kujitoa na kuchukua mafao yao kabla ya umri wa kustaafu. sasa ndipo nasema mwanzo hawakufanya utafiti aina ya wadau wa mifuko hii ya Jamii. Angalia hata barua ilioambatanishwa walioiandika.
 

Attachments

Watu wa migodi wamechachamaa lakini huku sector nyingine tumelala usingizi sana!!

Wewe ndio umelala watu wa-telecom wanasainisha petition (i.e Tigo, Airtel na Voda) ya kukataa huu upuuzi
 
naunga mkono, sheria hii ni ya wezi wa mchana ,SSRA ni zaidi ya wabakaji na wafiraji.
 
kamanda acha uoga.....nchi ni yako bado unaishi kwa hofu kiasi kikubwa hivyo.
 

Dizaini umeanza kukutana na wazungu ukubwani.
 
kamanda acha uoga.....nchi ni yako bado unaishi kwa hofu kiasi kikubwa hivyo.

Mhe. Vinci, hii nchi ni ya watu wachache, wengineo tumebaki kama watoto wa kambo hamna dili wala nini. Nilikuwa najaribu kumake point ya kwamba ubavu wa mtu mweusi ni mdogo sana ukilinganisha na mzungu pia kuwapa tahadhari wanamgomo wawe macho wasije shangaa kisago kitakachofuata. Angalia historia ya bara letu la afrika, akina patrice lumumba, samora, biko na wengine wengi tu wamekwishaangamia ktk harakati zao kukabiliana na racism iweje mfanyakazi wa mgodini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…