TUPACified
JF-Expert Member
- Feb 27, 2015
- 1,367
- 604
Mashabiki wa Premier League kwa muda mrefu wamekuwa wakijisifu kwamba ligi yao ni bora kutokana na vigezo kwamba ni ligi yenye ushindani mkubwa na ni ligi yenye followers wengi duniani (hakuna ubishi kabisa). Je ni kweli kwamba ushindani na umaarufu wa ligi ndio unaoifanya kuwa bora? Binafsi sidhani
Nadhani ligi bora ni yenye timu bora, wachezaji bora, mafanikio zaidi ngazi ya vilabu na kimataifa, mvuto wake kwa wachezaji bora, mchango wake katika mpira kwa ujumla n.k. Na La Liga iko far superior kwa vigezo hivyo.Ukizingatia kigezo cha karibu tu ambacho ni michuano ya ulaya (Both UEFA Champions league & UEFA Europa League) ni evidently enough ligi ya Uingereza iko chini kwa sasa kulinganisha na La Liga au hata Bundesliga. Juzi Arsenal wanacheza nyumbani dhidi ya Monaco dhaifu, kutoka 'ligi dhaifu' (Wachezaji watano wa kikosi cha kwanza walikosekana akiwemo captain wao) na wanakuwa hammered kama wamesimama vile. Jana kwenye Europa league, Timu ambazo zipo kwenye kiwango cha hatari kwa sasa katika PL, Liverpool na Tottenham Hotspur wanayaaga mashindano baada ya kushindwa kupita dhidi ya Fiorentina na Besistas ambazo ligi zao ni za kiwango cha kawaida sana.
FIFPRO World XI hakuna mchezaji wa premier hata mmoja, Ballon d'or japo ina mizengwe ila Premier League haikuwahusu, Wachezaji waliofanya mambo World Cup pia hakuna wa premier, TImu ya taifa ya Uingereza kila siku inajikongoja tu, Champions league 2013/14 ilikutanisha vilabu vya Spain fainali na hakuna timu yoyote ya Premier iliyoingia hata nusu fainali, bingwa wa Europa ni kutoka Spain. Wachezaji wanaoonekana wa kawaida La Liga wakija Premier wana-run the show (Kun, Diego Costa, Alexis Sanchez, David Silva, Yaya Toure, Fabregas, David De Gea, to name few). Wachezaji walio Man United, Chelsea, Liverpool, Arsenal wengi ndoto zao ni siku moja kucheza Barca, Real Madrid au Bayern Munchen ya sasa, lakini hakuna mwenye mchezaji wa barca au Madrid mwenye ndoto za kucheza United, Arsenal, Liverpool, Chelsea au hata City.
Ligi ya Uingereza ni kweli kabisa ndio maarufu kuliko zote duniani, ila pia 'El Clasico' ndio the most popular and the biggest football match duniani.
My thoughts.