Baraza la wawakilishi wapitisha hoja kuchunguzwa CUF kuhusika kuchochea ubaguzi ikibainika kufutwa

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,734
Spika20wa20Baraza20la20Wawakilishi20la20Zanzibar20Zuberi20Ali20Maulid.jpg

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), Zuberi Ali Maulidi


WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), wamepitisha hoja binafsi wakitaka Chama cha Wananchi (CUF), kichunguzwe na kikibainika kinahusika na vitendo vya ubaguzi ulijitokeza Zanzibar, kifutwe.

Wajumbe hao hawakuishia hapo pia, wanataka Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad achukuliwe hatua za kisheria.

Hoja hiyo imewasilishwa kwa dharura na Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae Mohamed said Mohamed (Dimwa) na kuungwa mkono na wajumbe baada ya kujadiliwa.

Mbele ya Spika wa Baraza la Wawakilishi (BLW), Zuberi Ali Mouludi hoja ziliibuliwa za kutakiwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuchunguza vitendo vinavyodaiwa kufanywa na viongozi wa CUF baada ya kufanyika uchaguzi wa marudio ambao waliususia.

Hatua ya CUF kususia uchaguzi wa marudio kwa madai haukuwa halali kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar na sheria ya uchaguzi namba 11 ya mwaka 1984, imesababisha kukwama kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK).

Wajumbe watano waliyochagia hoja hiyo na kueleza kuwa hali ya kisiasa ya Zanzibar si shwari kutokana na kasi ya wananchi kubaguana katika nyumba za ibada, misiba, harusi na kunyimana huduma za madukani na ndani ya vyombo vya usafiri kwa sababu ya chuki za kisiasa.

Chimbuko la ubaguzi huo pamoja na kuhujumiwa mali za serikali na wananchi kama utekelezaji wa mpango wa kutomtabua Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na viongozi wote, lilidaiwa ni agizo la Katibu Mkuu wa CUF kwa wananachama wa chama hicho.

Wawakilishi hao wanataka Maalim Seif, achukuliwe hatua za kisheria kwa kuhatarisha amani na umoja wa Wazanzibari kutokana na kampeni zake za kuwataka wananchi kugoma kulipa kodi pamoja na kutoshirikiana na serikali na wana CCM.

Hoja binafsi imesema waathirika wakubwa ni wana CCM ambao wanatengwa katika nyumba za ibada, misiba, harusi pamoja na kupata huduma nyingine za kijamii kama usafiri wa daladala.

Kuelekea Mwezi wa Ramadhani, waumini wanahitajika kufanya ibada pamoja lakini, hali imekuwa tofauti hasa katika kisiwa cha Pemba, ambako ni ngome kuu ya kisiasa ya CUF.

Madhara ya mpasuko wa kisiasa yameanza pia kuathiri Watanzania Bara ambao pia wameanza kutengwa hasa wanaoishi katika nyumba za kupanga wakionekana kama ni sehemu ya wana CCM Zanzibar.

Lakini SMZ katika kupambana na tatizo hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud Mohamed anasema watawanyang’anya leseni za biashara wafanyabiashara watakaopatikana na hatia ya kutoa huduma kwa ubaguzi au kujaribu kufanya mgomo kwa sababu za kisiasa.

Aliwambia wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuwa, SMZ imempiga marufuku Maalim Seif kuzunguka na misafara mirefu ya magari na kufanya mikusanyiko ya watu katika matawi au sehemu anazopita bila ya polisi kuwa na taarifa au kuwa na kibali.

Tayari watu watatu wameripotiwa kujeruhiwa katika vurugu zilizotokea vijiji vya Kivunge, Mkwajuni na Bumbwini baada ya askari wa kutuliza ghasia kutumia mabomu ya kutoa machozi, kuwatawanya wafuasi wa CUF waliojitokeza kumpokea Maalim Seif akiwa katika ziara yake ya kwanza tangu kufanyika uchaguzi wa marudio.

Mpasuko huo uliibuka baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana kwa madai ulikuwa na udaganyifu pamoja na waangalizi wa ndani na nje kudai ulikuwa uchaguzi huru na wa haki.

Baadhi yao ni Umoja wa Ulaya(EU) Jumuiya ya Madola (Commonwealth), Marekani na Uingereza. Uamuzi wa ZEC unapigwa na CUF ambao walisusia uchaguzi wa marudio wa Machi 20, 2016.

Tunajiuliza kwanini wananchi wateswe kwa maamuzi yaliyofanywa na Jecha na kufikia kunyimwa huduma muhimu za kijamii pamoja na kuhujumiwa mali zao yakiwamo majengo na mashamba ya mazao?

Lazima tukumbuke kwamba vitendo vya ubaguzi vinavyoendelea kufanyika Zanzibar hasa kisiwani Pemba havikubaliki katika misingi ya haki za binadamu na utawala bora.

Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana hakuharibiwa au kufutwa na wananchi wa Zanzibar tangazo la kuubatilisha lilitolewa na Mwenyekiti wa ZEC, kwanini waadhibiwe Wazanzibari au Wabara (Watanganyika), wasiokuwa na hatia?

Pamoja na wawakilishi kutaka CUF ichunguzwe na Katibu Mkuu achukuliwe hatua za kisheria si ufumbuzi wa kumaliza mpasuko wa uchaguz mkuu wa Zanzibar.

Unaweza kuifuta CUF lakini watu wanaoiunga mkono huwezi kuwafuta wataendelea kuwepo na kubakia na misimamo yao, cha muhimu ni kutafuta maelewano kwa njia za kidiplomasia na amani badala ya nguvu za dola.

Maridhiano bado ni jambo muhimu katika kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa uchaguzi mkuu wa Zanzibar kwa vyama vya CCM na CUF pamoja na kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa marudio na kuundwa kwa serikali ya awamu ya saba Zanzibar.

Kuwataka wahisani kuongeza vikwazo au wananchi wasilipe kodi hakusaidii, wanyonge ndiyo wataumia kwa ugumu wa maisha kwa kukosa misaada na wala si viongozi wakuu.
 
Mi ninavyomfahamu Mheshimiwa SHEIKH SHEIN ana busara sana hawezi kupenda Cheo huku waja wanaumia. Cheo hakiwezi kuzidi thawabu za baadae?
 
Kama hali ndiyo hiyo naanza kupata uwoga kwa ishara za kutoweka kwa amani
Waislamu sio watu wanaokubali kupelekeshwa ikitumika nguvu kutatokea madhara makubwa
Busara itumike

Na kama mnayataka ayo machafuko basi mmalizane hukohuko msifike uku tanganyika
 
Huyo muwakilishi Muhamed Said na hao wajumbe wa BLW hawaitakii mema znz na tz kwa ujumla.
Ivi kama baba yako au mmoja wa familia yako anaumwa ni busara kumuuwa au kumtibia?
Mm nadhani suala la znz linahitaji umakini na busara zaidi sio mihemuko ya kisiasa.
Kuifuta cuf au kumshitaki katibu wa cuf na kumfunga au kumuadhibu kwa njia yeyote ile sio kumaliza matatizo ya kisiasa znz.
Cuf haikuwepo kabla 1995 lakini znz ilikuwa na matatizo ya kisiasa.
seif kashewekwa ndani miaka kama mitatu hivi lakini akiwa ndani ndio matatizo yalizidi na mpaka leo yanaendelea.
Wazanzibari lazima wajiuluze nini chimbuko la haya yanayo jirudia kila mara.
Si vyema kila kukicha tunajidili migogoro ifike wakati tusahau hizi tofauti zetu tujadili mustakabali wa nchi yetu.
Miaka mitano ya mwisho ya Mh Amani na miaka mitano ya mwanzo ya Mh Sheni tumeshudia amani mshikamano na upendo kwa waznz na wa tz kwa ujumla.
Chakujiuliza tuliwezaje kuishi kwa amanani upendo na mshikamano miaka 10 iliyopita leo tushindwe?
Nafasi ipo bado sidhani kama taifa limekosa wazee na viongozi wenye hekima na busara wa kutufanya tuishi salama kwa amani na upendo.
Tukubali kila mmoja wetu kamkosea mwenzake na tukubali kila mmoja wetu kuwa tayari kuomba msamaha na kila mmoja wetu kukubali kusamehe kwa faida ya nchi yetu na vizazi vyetu.
Hatuwezi kuishi kwa kufukuwa makaburi.
 
Sindano inauma!hapo ndipo mnavuruga,Wamesahau Muungano?Cuf inaoperate bara na visiwani haitawezekana kufanya Kazi upande mmoja kwan lengo la chama cha kisiasa ni kushika dola na ni lazima kiendeshe shughuli zake pande zote,sasa hoja ya kikifuta Cuf Zanzibar labda wavunje Muungano.Ccm watulie wavumilie sindano zinavyouma.
 
Kama Pemba ni ngome kuu ya CUF mbona hawana mwakilishi hata mmoja? Je? Wawakilishi wa Ccm wako barazani kuijadili CUF au kujadili maendeleo ya majimbo yao! Mbona hapa kuna lugha gingana?
 
Back
Top Bottom