Baraza la vijana ni muhimu kwa sasa

Rafa kilenza

Member
Jan 23, 2017
32
30
TUNAHITAJI SASA BARAZA LA TAIFA LA VIJANA

Ni wakati sasa wa vijana wa Tanzania kupata baraza letu ambalo litakuwa na dhamira moja kubwa ya kuwatetea vijana wote wa kitanzania kwa kuweka itikadi za vyama vya siasa pembeni

Vijana ni kundi kubwa sana hapa nchini,Vijana ni wengi sana hapa nchini kwa mujibu wa takwimu mbali mbali zinaonyesha vijana ni zaidi ya nusu wa watu wote hapa Tanzania

Vijana hawana chombo cha kuwatetea,Vijana wanakosa haki zao za msingi katika nchi yao
Umoja wa vijana wa vyama mbali mbali vya siasa navyo vimeshindwa kutetea maslahi ya vijana wenzao zaidi ya kupokea maagizo kutoka kwa wakubwa zao tu tena kwa maslahi ya vyama vyao
Umoja wa vijana wa UVCCM upo kimya sana katika kutetea maslahi ya vijana wa chama cha mapinduzi nadhani taratibu za chama zinawabana
Vijana wengi walipokosa mikopo hata wale wa ccm hakuna tamko lolote kuhusu hawa vijana
Uvccm ya miaka ya nyuma sio hii ya sasa
Uvccm ilikuwa na nguvu kubwa sana ndani ya hii nchi walikuwa wapo makini sana katika kutetea maslahi ya vijana

Umoja wa vijana wa chadema( BAVICHA) upo kimya sana.Bavicha ya miaka ya nyuma sio hii ya sasa,bavicha imekuwa kimya sana inashindwa hata kutoa matamko katika kutetea maslahi ya vijana wenzao wa chadema
Leo hii kijana na mwanachama mashuhuri wa chadema ndugu BEN SAANANE hajulikani halipo kwa zaidi ya miezi miwili sasa lakini bavicha ipo kimya, bavicha haina mpango na be saanane,Tukiacha siasa zetu za vyama ben ni mtanzania mwenzetu na ni kijana mwenzetu kwanini bavicha wapo kimya kuhusu ben? Labda ni maagizo kutoka chadema kuu

Ni muhimu sana kwa sasa vijana wote kuunganishwa kwa pamoja bila kuweka itikadi zetu za vyama vya siasa

Tunaitaji sasa baraza la taifa la vijana ambalo halitakuwa na sura za kisiasa na kazi yake kubwa ni kutetea vijana wote wa kitanzania bila hizi siasa zetu za ccm,cdm,act na cuf,Vijana hatuna nguvu moja,vijana hatuna watetezi, vijana tumebaki yatima tu hatujui kesho yetu kuna nini tumebaki kama gari bovu tu

Leo hii makato ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu yameongezeka kutoka 8% adi 15% na wahathirika wengi ni vijana na sio wazee
Vijana wote wamebaki wanalia lia tu kwenye mitandao hawana cha kufanya,chama cha wafanyakazi wapo kimya, Tughe,Cwt na vyama vyote vya wafanyakazi wapo kimya hawana muda na vilio vya vijana, hata uvccm na bavicha wapo kimya, wanaolalamika ni wanachama wa ccm na cdm pia, nani sasa wa kumsaidia kijana huyu? Ndio maana tunataka baraza la vijana litakaloundwa na vijana kwa maslahi ya vijana

Wabunge wetu vijana waliopo bungeni nao wapo kimya, hawana msaada kwa vijana wa kitanzania, wapo busy na mambo yao.Hawawezi kuwa busy na maswala ya vijana kwa kuwa hawakuchaguliwa na vijana na wao kwanini wasumbuke kwa kutetea vijana wanaolalamika kuhusu makato ya bodi ya mikopo wakati kule bungeni wao take home zao ni 17m..?
Sijaona mbunge yeyote kijana ambaye hili jambo limemgusa wao wapo busy na siasa zao vyama vyao

Kijana mbunge hawezi kupoteza muda kutetea vijana wakati yeye sasa hivi yupo bungeni ana mshahara mzuri sana
Sisi watanzania tuna desturi moja kwamba ukiwa mezani unakula hupaswa kuongea adi chakula kiishe' nadhani kwa sasa wapo mezani wanakula wataongea 2020

Makubaliano ya bodi ya mikopo na vijana waliosaini mikataba ya mikopo ilikuwa ni kukatwa 8% na sio 15%.Fomu hizo zimesainiwa na watu wawili tu, mkopaji na heslb
Kwa mujibu wa sheria za mikataba ya Tanzania na dunia nzima ni kwamba(contract act) mabadiliko yeyote yanayofanyika ndani ya mkataba ni lazima pande zote zilizohusika kukubaliana kwanza kabla ya kufanya hayo mabadiliko. kwanini vijana hawa hawajapewa nafasi ya kushauriana na bodi ya mikopo? Kwakuwa hawana uwakilishi wala hawana watu wa kuwatetea

Hata kama bunge lina mamlaka makubwa kiasi chote hiki lakini walipaswa kwanza kundi hili la wakopaji kukaa mezani na wahusika ndio wakubaliane kuhusu haya makato
Hili swala wabunge wetu wa chadema, act, nccr, cuf na Ccm walilipitisha kwa kugonga mikono mezani na leo hii vijana wanalia hawana msaada

Tunaitaji baraza la vijana sasa ili likatetea maslahi ya vijana na sio ya kisiasa. Kwanini mnatunyima baraza letu? Wabunge vijana mmeshindwa kuwatetea vijana wenzenu lakini kumbukeni ubunge sio kazi ya maisha ni ya muda tu na nyie mtakuja uku mitaani
Vijana wanalalamika sana tena sana kuhusu uwakilishi wao tunaomba waziri anayehusika na wizara ya vijana atuletee baraza letu sasa na sisi tupate wa kutuwakilisha nyie bakini na vyama vyenu

Sisi vijana tuna kesho nyingi sana kuliko Jana

RAPHAEL LUKINDO
 
Sawa kabisa mtoa mada nakuunga mkono hata mm Niko tayari
 
Back
Top Bottom