Mwenyezi MUNGU anayotabia ya kuwatumia wale watu ambao wamekataliwa. MUNGU anayo tabia ya kuwabariki wale watu ambao wamedharauliwa, kuumizwa na kufedheheshwa.
.
MUNGU anayotabia ya kuwainua, kuwapa hadhi na kuwaheshimisha wale walioumizwa vibaya.
.
Hufanya hivyo makusudi kabisa, ili tu, pale utakapofanikiwa, asiinuke mtu awaye yote na kusema kwamba, bila yeye wewe usingekuwepo hapo ulipo.
.
Mwenyezi MUNGU atakubariki ule wakati ambapo hakuna hata mmoja anaesimama na wewe kukusaidia. Ili tu, pale utakapofanikiwa mtu awaye yote asiinuke na kusema mimi nilikusaidia mpaka kufanikiwa.
.
Endapo mtu ataanzisha vita na wewe, endapo mtu atakuumiza, kukufedhehesha na kushushia heshima, hebu furahi maana hiyo ni dalili tosha kwamba, MUNGU ameamua kukubariki.
.
Sijui ni yepi unayoyapitia, ila elewa kwamba, kwa yote yanayokuumiza muda huu hebu kuwa na furaha, wala usioneshe huzuni. Usiwape ushindi wa mezani. Kilima uzuri mbali, karibu kina majuto.
.
You are a candidate for God's next blessing!