Baragumu: Wabunge wanaohama wanakimbia ahadi zisizotekelezeka walizowaahidi wananchi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,957
141,946
Mjadala unaendelea katika kipindi cha baragumu channel ten juu ya hama hama ya wabunge.

Wachangiaji wanasema hadi sasa ni Nyalandu na Mtulia ambao wameutema ubunge kwa kuhama vyama lakini ukienda katika majimbo yao utagundua kuwa hawajafanya lolote la maana.

Wamedai hata wabunge wanaotarajiwa kuhama wengi ni wale walioishiwa pumzi majimboni na ndio maana hutegemei mbunge kama Bashe ahame CCM kwa sababu anatimiza majukumu yake ipasavyo halikadhalika Sugu wa Mbeya.

Source kipindi cha Baragumu channel ten!
 
Wameonesha ni namna gani watanzania walivyo chini kifikra
 
Kabla haujachangia pumba hapa kwanza mnaujuwa mshahara wa mbunge?

Mnazijuwa posho za vikao? Kama mtu hajafanya lolote anashindwa kusinzia tu bungeni na akifika 2020 hachukui fomu na analamba pensheni yake?

Mada kama hizi ndio utagunduwa jinsi Watanzania walivyo weupe kichwani.
 
Unazungumzia marupurupu mbona Rostam aliyaacha akasepa, mbona Zitto aliyaacha akasepa zake?!!! Mkuu ubunge ni zaidi ya marupurupu!!
 
Unazungumzia marupurupu mbona Rostam aliyaacha akasepa, mbona Zitto aliyaacha akasepa zake?!!! Mkuu ubunge ni zaidi ya marupurupu!!
Akili yako ni ndogo sana, Rostam hakufuata pesa kwenye ubunge na Zitto Kabwe alishspiga madili makubwa utawala wa JK ndio maana hata sitting allowance akawa hachukui (Mnafki)
 
Back
Top Bottom