Barabara za jiji la Arusha zinakera sana

Barabara za jiji la Arusha zinakera sana

chingas

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2014
Posts
261
Reaction score
113
Jiji la Arusha ni ndogo ukilinganisha na majiji mengine kuna barabara chache zinazoingia mjini kati na kati ya barabara hizo ziko zinazokera kuzitumia kutokana na foleni zinazosababishwa na daladala kujitawala barabarani kama vile sheria hakuna.

Kwa mfano--barabara inayotoka makao mapya kwenda Posta ya Meru.

Kuna daladala za Ngaramtoni zinaacha kupakilia abiria ndani ya stand ndogo na kupakilia abiria nje barabarani na mara nyingi husababisha foleni ndefu.

Barabara hiyo hiyo ikifika Posta kuna daladala kwa makusudi hupakia abiria kwenye kona na kuzuwia magari mengine yanayotaka kuingia Uhuru road, inakera sana hii.

Barabara inayotoka stand ndogo kupitia Anex kwenda miazini kwa makusudi daladala hupakilia abiria kwenye kona na kusababisha foleni kubwa kwa barabara zote zinazokutana pale.

Barabara ya uhuru kwenda mbauda kwa makusudi daladala hupakia abiria katkati ya barabara maeneo na kusababisha foleni kwa magar yanayowai trafic light za esso.

Ukienda kule kwa morombo ndio kabisaa daladala hupakia abiria katikati ya barabara bila wasiwasi.

Kwa kweli hizi barabara zinakera sana yaani kama uko na mgonjwa kwenye gare anaweza kupoteza maisha ukiwa kwenye foleni hizi zinazosababishwaa daladala.

Hivi yuko wapi mkuu wa trafic Arusha? Mbona hatuoni kazi yako kama wakuu wengine waliokutangulia?Mbona kuna trafic mmoja hapa Arusha anayo maarifa sana ya kuwanyoosha awa madereva wakorofi, kwanini msimuweke huyu askari Malisa atunyooshee hizi barabara?
 
Mkuu daladala nyingi ni zao........na si unajua January ni kesho kutwa..........
 
Kweli kabisa Arusha barabara ni kero kero kero yani inatia hasira ni kama hakuna sheria kwanza Arusha kwa idadi ya magari yaliyopo sasa na kasi ya ukuaji wa mji hakuna barabara labda vichochoro.
 
Umesema kweli..

Halafu sijui wameruhusu machinga kurudini katikati ya mji..

Ni kinyaa
 
Yani utafikiri ulikua town leo kwa jins palivyokua na jam kubwa.yani tumekereka sana kwa sababu unakuta ni dereva mmoja tu wa daladala anahamua kupaki gari njian ili apakie abiria.ole wako umsemeshe.walivyo wababe sasa .utafikiri wameweka serikali yetu mifukoni mwao.
 
Mamlaka husika zichukue hatua stahiki...

Vifodi ni kero kubwa hapa Arusha
 
Daladala ndo zao mkuu hazina ustaarab hata kidogo kwenye matumiz ya barabarani niwasababishaji wazur sana wa ajali ukifuata hapo nyuma yake nilazima umgonge anashika break ghafla katikat ya njia bila hata kuangalia nyuma yake akiona abiria
 
Juzi jumamosi ilinichukua zaidi ya nusu saa ku drive kutoka posta meru mpka makao mapya cafe la aziz, palikuwa na jam ya hatari. Leo mchana barabara zote mpaka za ndani ndani kilikuwa na jam, ilinichukua kama dakika 20 kutoka metropal mpka stanley hotel frends conner.

Arusha barabara nyembamba alafu chache na hakuna njia mbadala, shunghuli nyingi za watu ni mjini tu. Eneo la stand kubwa maduka ya jirani kumejaa watu msimu huu wa sikuu mpaka njia hazipitiki jwa gari
Watu wa mipango miji wana haja ya kuangali mji wa Arusha kwa jicho la pili maana miaka mitano ijayo hali itakuwa mbya sana.
 
Police wengi hasa Trfic ndio wamiliki wa Daladala na ndio maana hazikamatwi.
 
Yote ameleta lema, wakati ule hawa watu walipogoma yeye aliwatetea eti wapaki wapi.!? na barabara mbadala zipo ila watu wamegeuza ni mahali pa kupaki magari yao, wamachinga kufanyia biashara zao yote ni lema ameleta.! yaani jiji limekuwa kama zizi, haohao madereva wanakojoa barabarani hovyo na kupaki ndio kabisaa, magari mengine mabovu hayafai kubebea abiria lakini yapo barabarani, dawa iliyopo ni kuondoa daladala zote na kuweka coaster zifanye kazi kama Dar, kero nyingine ni ungaltd daladala ni shida tupu ukiwa ndani utafikiri uko nje, maana gari limetoboka mtindo mmoja mpaka unaona chini, janga la mwisho ni madereva na makonda ni wachafu kupindukia yaani ni kero na lugha mbaya ajabu, mirungi, viroba kwa kwenda mbele, mkuu wa mkoa na kamanda wa polisi mkoa tunaomba mtutatulie hili tatizo, naomba kuwakilisha hoja.
 
Back
Top Bottom