BABA E's
JF-Expert Member
- Dec 25, 2012
- 354
- 135
Hii barabara sasahivi hali ni mbaya kupita kiasi hasa ukizingatia magari mengi yanatumia hiyo njia. Zaidi ya mwezi sasa viliwekwa vifusi ambavyo mpaka leo havisambazwa mpaka vifusi vingine vimesombwa na mvua, hii nayo imeongeza kero kwenye hiyo barabara. Nashindwa kuelewa kwanini tunapata hii shida wakati Machine zipo zimepaki barabarani zinaonekana zaidi ya miezi miwili na hazifanyi kazi.