Balozi wa Malaysia nchini Korea Kaskazini aitwa nyumbani

Ava Sancez

Member
Jan 27, 2017
33
50
_94736468_3f13e654-be87-4b6d-9789-3b54cc83aab1.jpg

Malaysia imemuita balozi wake nchini Korea Kaskazini kufuatia tofauti zilizojitokeza kati ya mataifa hayo mawili kutokana na kifo cha nduguye Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kilichotokea uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur.

Nchi hiyo pia imesema kuwa imemtaka balozi wa Korea Kaskazini ametuhumiwa na serikali ya Malaysia kutokana na shutuma zake dhidi ya nnchi hiyo wiki iliyopita kutokana na kifo hicho.

Nduguye Rais wa Korea Kaskazini inadaiwa kuwa aliuawa kwa sumu na Malaysia inaendelea na uchunguzi japo kuwa Korea Kaskazini inahitaji kurejeshewa mwili huo na kwamba haihitaji uchunguzi wowote ikiwepo upasuaji kufanyika.

Hata hivyo Malaysia imesisitiza itaendelea na uchunguzi na kwamba ina mamlaka ya kufanya uchunguzi huo kwa kuwa alifia katika ardhi ya nchi yao lazima wafanye uchunguzi na hakuna wa kuwazuia.

Chanzo: BBC/Swahili
 
North Korea wanahusika na mauaji na hiyo nia ya kujihami tu dhidi ya tuhuma.
 
Hii mbegu (damu) ya nduguye aliyoimwaga ardhini hakika itamlilia Kim Jong-Un maisha yake yote. Huu ni mwanzo wa kuanguka kwa utawala wake. Hakuna aliyewainukia wa nyumbani mwake akadumu; hiyo ni kanuni ya asili.
 
Wewe umejuaje kama yeye ndo kamuua ndugu yake?
Kwanini usiseme waliomuua uwezekano Mkubwa kuwa ni maaadui wake kisiasa Nchini mwake,na Nje ya nchi yake...kama Marekani,South korea nk.Kila siku tumeona jinsi CIA Marekani wanavyochukia KIM JONG wa Noth korea asifanye majaribio ya nyuklia na yeye amekuwa akifanya....,pia wapinzani wake wengi ki siasa amekuwa akiwaua,sasa huoni logic tuu hapo?
halafu useme eti yeye mwenyewe ndo kamuua kaka yake hata sikubali 100%.
 
Typical communist/socialist ideology! Huwa mnapenda kutenda maovu halafu mnayakana just through cheap propaganda like what you've brought here. Kwani huyu ni wa kwanza kuuwawa na Kim? Kim ameua hadi viongozi kwenye serikali yake kwa vijisababu vya kijinga kabisa; hapa napo anasingiziwa? Kim Jong-un executes education minister by firing squad for not sitting properly in meeting | Daily Mail Online. Hapa napo? Entire family of Kim Jong-un’s uncle executed in N. Korea – reports. Hebu acha kutetea ushetani kwa hoja nyepesi ndugu; au kwa sababu hayajakufika?
 
Katika hiyo article uliyoweka kuna hii sentensi 'after making an alleged attempt to stage a military coup and dethrone his nephew.' Dogo Kim alifanya sahihi kum-execute
 
You're still proving how intolerable dictators are! Kumbe ni just "alleged"; mbona yeyote akiamua anaweza kumtuhumu yeyote? I thought was found guilty kumbe ni just allegations! Huyo dogo atakufa kifo kibaya sana; and I can see, "ufalme" wa ukoo wa Kim unaishia kwa huyo dogo mjinga. Baada yake taifa la North Korea litaishi maisha ya kibinadamu kama mataifa mengine.
 
Hahaa kakutana na wavutaji wenzie, mpaka wachunguze kwanza ndipo wammpe mwili wa kaka yake, otherways akaushe.
 
Huyo dogo ni mpuuzi alidhani akimuua kaka yake nje ya ardhi yake haitajulikana maana huyu alieuawa alikua anampinga sana mdogo mtu na anaonekana hata kukosa kiti cha ufalme ni kutokua na siasa kali kama za mdogo mtu ingawaje wao walisema alitumia hati feki ya Taiwani kwenda Japani kama nakumbuka vizuri..
 
Wewe umejuaje kama yeye ndo kamuua ndugu yake?
Kwanini usiseme waliomuua uwezekano Mkubwa kuwa ni maaadui wake kisiasa Nchini mwake,na Nje ya nchi yake...kama Marekani,South korea nk.Kila siku tumeona jinsi CIA Marekani wanavyochukia KIM JONG wa Noth korea asifanye majaribio ya nyuklia na yeye amekuwa akifanya....,pia wapinzani wake wengi ki siasa amekuwa akiwaua,sasa huoni logic tuu hapo?
halafu useme eti yeye mwenyewe ndo kamuua kaka yake hata sikubali 100%.
Mkuu hata hukumbuki alivyomdungua mjomba wake na ant-aircraft gun?...Pia unajua kwamba huyu aliyeuawa alikuwa uhamishoni sababu alikuwa akipingana na sera za ndugu yake?...Unataka kunambia ni mara yako ya kwanza kusikia huyu Kim jong un kuuwa mtu anayepingana nae?...Yaani akili zetu zishakuwa lazy sana.Kila kitu kinachotokea kwa maadui wa marekani basi ni marekani kafanya.Hem tutume akili zetu vizuri basi.Usipoagalia kuna siku utaibiwa mkeo alafu utasema ni marekani kasababisha.
 
South Korea propaganda

Hakuna uthibitisho
Hawa south wana propaganda sana

Huyo Kim jong nam alipokufa south walieneza propaganda nyingi za uongo shukrani kwa maofisa wa Malaysia wamewaaibisha south Korea

Kuhusu hiyo kudunguliwa kwa ant craft 100% south propaganda
 
Huwa nashangaa sana, habari za Korea kaskazini eti huwa zinatolewa na Korea kusini tena zile zinazoonyesha ubaya tu, yaani kama wao ndio wasemaji wa serikali Korea kaskazini.
 
King Jong Nam na King Jong Un watoto wa Baba mmoja ila Mama mbalimbali, huyo Kim Jong Nam ndio alitakiwa awe mrithi wa Urais katika nchi ya DPRK hadi pale alipokamatwa akiingia Japan kwa pasipoti bandia, ndio urithi wa kiti cha Urais ukaenda kwa Kim Jong Un. Kim Jong Nam alikua mpinzani mkubwa sana wa nchi kuendeshwa kwa urithi wa kiukoo.
 
Huwa nashangaa sana, habari za Korea kaskazini eti huwa zinatolewa na Korea kusini tena zile zinazoonyesha ubaya tu, yaani kama wao ndio wasemaji wa serikali Korea kaskazini.
Siku ambayo huyu jamaa alikufa media zote za Korea kusini na maofisa walikuwa wanasema spies wa North Korea walimchoma sindano yenye sumu huyo jamaa na walikuwa wanaeleza step kwa step namna alivyouliwa??

Swali la kujiuliza huyu jamaa amefia airport ya Malaysia na polisi wa Malaysia hawakufanya uchunguzi wala kutoa ripoti hawa Korea kusini walijuaje??..yani tukio litokee nchi ya mbali na ripoti haikutolewa wao siku hiyo hiyo wakaanza kutoa ripoti za uongo eti alichomwa sindano yenye sumu na wakataja aina ya sumu

Lakini baada ya uchunguzi kufanyika maofisa wa Malaysia wakasema hakuna sehemu huyo jamaa alichomwa sindano ya aina yeyote ile bali alipuliziwa tu na video ya CCTV imeonyesha tofauti na namna Korea kusini walivyoelezea tukio..wameaibishwa vibaya

Watu pekee waliokuwa wanapaswa kutolea ufafanuzi ni Malaysia ..

Na watuhumiwa wamekamatwa na pasi ya kusafiria ya Vietnam ..

Habari nyingi tu hawa Korea kusini wanatoa za propaganda na nikiona source ya habari ni Korea kusini huwa napuuzia ,.kuhusu hiyo ishu ya ant craft hakuna uthibitisho Bali south wamesema tu na hawa south wana propaganda nyingi na ndio huwapa taarifa CNN

Inawezekana north wamefanya kweli lakini south sio wa kuwaamini na inawezekana spies wa south ndio wameua na kuanza kumfanyia propaganda kim ili azidi kuonekana mbaya sababu tu USA wanawaamini south

Mjomba habari za south ukizitizama propaganda zao za kimiyeyusho Mimi nipo kwenye group moja linalohusiana na north Korea tu humo kuna waandishi wa habari wa kujitegemea na waliofika north ndio nikagundua upuuzi wa south ..

Kim ana madhaifu lakini hawa south hawawezi kuwa reliable source,toka lini panya akaandika ukweli kuhusu paka zaidi ya kumchafua ili USA azidi kumwekea vikwazo na amvamie na propaganda tu..
 
South Korea propaganda

Hakuna uthibitisho
Hawa south wana propaganda sana

Huyo Kim jong nam alipokufa south walieneza propaganda nyingi za uongo shukrani kwa maofisa wa Malaysia wamewaaibisha south Korea

Kuhusu hiyo kudunguliwa kwa ant craft 100% south propaganda
Okey,sasa tuwekee habari toka North korea iliyotangaza kupinga hizo propaganda za south korea.
weka link.
 
Back
Top Bottom