1.
Nimetafakari wasifu wa aliyekuwa Gavana wa BoT Dr. Daudi Timoteo Saidi Balali, na sijaweza kuona sababu ya mtu aliyekuwa na wasifu na kipato kizuri sana (hata kabla ya huo ugavana) kujihusisha na wizi wa aina yoyote.
Mwizi ni mwizi, na kiongozi yoyote asiyekuwa mwizi hujitenga na tuhuma za wizi kwa kusema ukweli tena at the right time, kama Balali hakuwa mwizi alikuwa na kila haki ya kusema ukweli, sasa hivi tayari runajua kuwa kuna hela nyingi sana zilizoibiwa huko BOT kwa ruhusa yake,
Ninazo dataz zote hata alivyojaribu kujiweka sawa kwa kuwapa wabunge wawasha moto hela za bure kutoka huko, ili wanyamaze, mmojawapo akiwa Mzindakaya, ambaye according to the dataz ni kwamba origianlly alikuwa na deni la shillingi billioni 9 toka benki ya Standard, ambazo alishindwa kulipa kabisa wakati ulipowadia wa malipo tena ya kwanza, alipoona wanamjia juu Mzindakaya, akaamua kumfuata Balali, ambaye pamoja na kushindwa kwake kuwalipa Standard bank, Balali akaamua kumlipia anyways deni hilo,
Mkuu wangu hakuna gazeti lolote wala serikali ambayo imewahi kutuambia Mzindakaya alipataje ule mkopo wa BOT, huu ninaouweka hapa ndio ukweli wake na unamhusu Balali period! Je alifanya madudu mangapi huko BOT?
Kwa hiyo mkuu huwezi kutaka wananchi wakaandamane DC nyumbani kwa Balali, halafu hapa unakuja kumtetea kuwa hakuiba hela za taifa letu, sasa mbona unajichanganya mkuu?
2.
Nahisi kuna usaliti aliofanyiwa, na inawezekana siku zote ambazo tulikosa habari zake kuna watu walizizuia kwa makusudi.
Jamani sisi ni watu wazima hapa JF, zimetolewa habari za wizi wa watu wa karibu na rais wetu kama Lowassa, na Karamagi sasa zitakuwa za Balali? Eti kuna watu wamezizuia kwa makusudi? Yaaani hao watu wana nguvu mpaka ya kumzuzia Balali asiongee akiwa nje ya nchi? Usaliti? Alifanyiwa au alijifanyia mwenyewe?
Mkuu ninaamini kuwa una uwezo wa kufikiri zaidi ya hizi hoja finyu za kujaribu kumsafisha Balali, kiongozi yoyote msafi hawezi kuishia kwenye haya mazingara ya Balali, the matter of fact toka tupate uhuru hizi habari zake za sasa ni the best comedy ever, na ni lazima iende kitabu cha record za dunia za historia!