Bahati

Averos

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
788
500
Ewe sheikh ndugu yangu, hii dunia ya Qawi
Utazame ulimwengu, likutakalo haliwi
Ndio kalamu ya Mungu, viumbe hatuijuwi
Bahati yenda kwa muwi, wema wakalia ngoa

Bahati imegeuka, watatu hazidishiwi.
Wa moja afurahika, mbili hazimsumbui
Mkavu wanawirika, mbichi hauchipui
Bahati yenda kwa muwi, wema wakalia ngoa

Wa kisamvu ala nyama, wa samli ala tui
Simba limekuwa ndama, makucha hayapapui
Kieleacho huzama, shina limekuwa tawi
Bahati yenda kwa muwi, wema wakalia ngoa

Wa kilio yuwacheka, war aha hafurahiwi
Wa nyuma wanatukuka, wanena hawarudiwa
Wa mbele wanatihika, wasema hawasikiwi
Bahati yenda kwa muwi, wema wakalia ngoa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom