Hakuna mtu ambaye haipendi nchi yake humu ndani, wote tunaipenda na tunaiombea mema dhidi ya waharibifu.
Ila kuna tofauti kati ya kuipenda nchi na kuipenda serikali. Kuichukia au kuipenda nchi ni tofauti kabisa na kuichukia au kuipenda Serikali.
Kuna wakati kuipenda Serikali iliyopo madarakani sio uzalendo, na kuna wakati kuichukia Serikali iliyopo madarakani ni uzalendo.