Bado ni Chura Kiziwi?

Bado ni Chura Kiziwi?

Kalamu

Platinum Member
Joined
Nov 26, 2006
Posts
19,488
Reaction score
26,109
Ni swala la kumkumbusha yeye na waTanzania kwa ujumla wasisahau ilikuwa kuwaje hadi akaamua mwenyewe kujipa jina hilo bila ya kushurutishwa na yeyote..

Sasa awaeleze waTanzania, huo ukiziwi wake uliinufaisha vipi Tanzania; na kama baada ya kunyang'anya miaka mingine mitano ukiziwi wake utaongezeka maa dufu!

Je, kuna ushahidi wowote ambao waTanzania wanaweza kuutambua kuwa ni faida iliyotokana na ukiziwi wa mtawala wao ambao umewanufaisha na kwamba miaka mitano mingine yenye ukiziwi mkubwa zaidi ya ule wa mwanzo utailetea nchi yao manufaa zaidi?

1. Tutegemee utekaji na uuaji wa waTanzania zaidi?

2. Mikataba ya kuuza raslimali za nchi yetu iwe ni ya siri zaidi; kama ile ya Gesi ya Ntorya ambayo wamepewa wajomba toka Oman? Huu mradi wa Lindi si ndio kitakuwa kiama chetu?

3. Chura kiziwi huyo huyo ndie awe mwamuzi wa kesi mahakamani?

4. Bunge liwe ni la kuendeshwa na kutunga sheria anazotaka Chura Kiziwi?

5. WaTanzania wawe ni watwana tu wa kuwatumikia watu toka nje kwa jina la uwekezaji?

6. Miaka mitano tena, au zaidi, iwe ni ujenzi wa matabaka wa walionacho na wasiokuwa nacho ndani ya nchi yetu hii. Tunaona akina DULA na wengine, sijui akina Mombo, na akina Polisi wa mabilioni tayari tunao ndani ya miaka minne tu; je, itakuwaje ikiwa mika mitano, kumi au hata ishirini? (Museveni ni mfano mahsusi namna ya kudumu madarakani kwenye ukanda huu; bila shaka Chura Kiziwi kajifunza vya kutosha toka kwake).

Na mengi mengine ambayo yanajulikana kuwa ni matokeo ya kuwa na Chura kiziwi kama mtawala wetu.

Nchi hii na Chura Kiziwi, tutasalimika kweli?
 
Back
Top Bottom