Apologise lady
JF-Expert Member
- Sep 16, 2013
- 5,979
- 3,103
Kijana badilika, tena jirekebishe, wakati wewe unatumia muda wako kusubiri ajira na kuwacheka wenzio wanao jaribu kufanya hata jambo dogo ambalo linamuingizia kipato, nakuambia unajipotezea muda na utashia kumuona kila mtu adui kwako
Kamwe hutopata amani, maana utapoteza marafiki kila siku, kwa kuwa kila rafikio anaefanikiwa utamsifia huku roho inakuparama ndani kwa ndani, mwisho utajitenga bila kuaga
Jifufunze kuthubutu bila kuangalia watu watakuonaje, usitake hadi upate fursa kubwa uitendee haki, nakuambia utasubiri sana na utaishia kuwasema vibaya wanaofanikiwa"free mason huyo, kahongwa huyo, alipewa mtaji wa urithi nk "
Wenzio wanafanya jambo la kawaida kabisa lakini wanaingiza pesa, wewe ambae hata kiwanja chamazi huna, unadharau kazi, utasubiri sana na kasi hii ya mchakamchaka wa MAGUFULI wallah!!! Utachuchumaa.
Jifunze kwa waliofanikiwa, fanya maamuzi, chukua hatua.
"usimuulize mtu amegraduate wapi, muulize anaingiza shilingi ngapi"
Mwisho karibu jukwaa la matangazo madogo, ujipatie bidhaa bora kwa bei nafuu.
Karibu nikuvishe