aiseee haya maakuli ni hatari tupu kudos..1)Kunde.... (za kupaaza) kg 1/2
2)pilipili mboga 1/2..
3)kitunguu maji 1/2.
4)kitunguu saumu 1/2teaspoon
5) chumvi kiasi....
6)baking powder/hamira 1tablespoon
7)mafuta ya kupikia
8)kotmiri/giligilani
Namna ya kutaarisha
1)roweka kunde for 4 hours
2)weka kwenye blender ama food processor bila ya kutia maji then weka pilipili mboga,kitunguu maji, saumu na chumvi na kotmiri/giligilani
3)tia baking powder/hamira kwenye mchanganyiko wako
4) weka mafuta kwenye karai na ukaange badia zako kwa kutengeneza viduara vidogo vidogo
5)kaanga hadi ziwe brown..weka moto mdogo mdogo ili ziwive vizuri ndani...
Badia tayari kwa kuliwa....
Hizi ndo tamu, kuliko zile za dengu. Weekend ijayo itakuwa ya kujaribu mapishi yako kadhaa likiwemo hili. Ntakuonjesha mpishi mkuu unipe alama za ufaulu.
Ntajaribu !! au gesi ntawauzia wachina !!!Noo ukiziroweka zinapungua sana gesi..
hizi natengeneza kesho sitaki kupitwa shosti
Mie nnavojua ni badia... za kunde tamu zaidi BAK...kwa chatne ya nazi au hiyo ya embe mbichi weee utamu hadi machoni lol...
Unajua kuna baadhi ya maneno matamshi yake yanatofautiana kati ya Zenj na Tanganyika. Huku Bara tunaziita bajia. Kuna neno kama swali, Zenj ni suali. Sikulielewa swali/suali lako?
Yeah ni kweli ila walau tunaelewana mfano kaimati nyinyi mwaita kalimati........
Unajua kuna baadhi ya maneno matamshi yake yanatofautiana kati ya Zenj na Tanganyika. Huku Bara tunaziita bajia. Kuna neno kama swali, Zenj ni suali. Sikulielewa swali/suali lako?
Upo mamito..eid imetuficha 🙂
Nipo jaan habar za eid vp mkwe wangu alienjoy
Hahha kaenjoy sana na mifuko imejaa saiv zote anaweka kwenye kibubu cha mchumba...lol
Sijaelewa kunde za kupaaza maana yake nini
Besti...bajia kihindi zaidi...lol
Best nafahamu kwamba Badia ni neno la kidindi ambalo limekuwa adopted na Kiswahili kama yalivyo maneno mengine ya kihindi chai, lakini n.k. ila kuna tofauti ya matamshi kati ya bara na visiwani. Visiwani linatamkwa kama wanavyolitamka wenyewe wahindi na bara linatamkwa Bajia. Mzima lakini Best? usipotee hivyo banaaa!?
Mie mzima wa afya nashkuru. Sijapotea kiivyo besti majukumu tuu ...saivi nategemea mahanjumati ya eid yatawekwa sana na jaanu farkhina kwahio tutakutana jikoni. .lol
Senkyuu, nnavyozipenda mie hizi..