Baba kwanini umeniacha hapa?

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,622
Reaction score
167,462
I LOVE YOU!!!! (NAKUPENDA)
Mwezi mmoja baada ya kumaliza elimu yangu ya kidato cha sita 2013 huko jijini Mwanza nilirejea nyumbani kwetu Mbeya.......

Nyumbani kwetu nipakawaida sanaa lakini nashukuru Mungu tulikuwa tunauwezo wa kupata chakula (asubuhi, mchana na jioni)
Nakumbuka siku moja niliwahi kusikia baba yangu akizungumzia kuhusu swala la kuwasaidia yatima.. Wajane pia kuwatembelea wafungwa.......

Nilibahatika kupata kakazi ka kufundisha shule moja pale mtaani kwetu jambo ambalo liliniwezesha kupata hela kidogo ya kujikim.....

Baada ya kulipwa niliwanunulia wazazi wangu zawadi japokuwa ilikuwa ndogo ***** siku hiyo jioni wakati wa Sala mama yangu aliniita faragha na kuniuliza '' mwanangu Mau hivi toka uzaliwe ushaawahi kwenda kuwatembelea watoto yatima? '' nilimjibu mama kwamba sijawahi...... Mama akaniambia basi siku moja jipange twende tukawatembelee '' lakini mama kwa kitu gani hasaa tulichonacho ili tuwatembelee '' nilimjibu mama yangu.........

Mama alizidi kunielewesha kwamba chochote ukitoa kwa Moyo basi hicho ni kikubwa sanaaa kwa Mungu......... Tulizidi kuongea sana hatimae tulifikia muafaka kwamba jumapili tungeondoka......

Jumapili majira ya saa saba tulianza safari yetu mimi, baba na mama....
Tulifika salama na tulipokewa vizur sanaa na mda wa kukutana na watoto pamoja na kuwapa chochote kitu ulifika...............

Ilikuwa ni ngumu sanaa kwangu pale ambapo mtoto mmoja alikuja moja kwa moja kwangu....Mtoto huyu alikuwa kati ya miaka 6 mpaka 7 (Maurine) alipokuja alinirukia '' baba shikamoo.. Kwanini umeniacha hapa??? Leo si tutaondoka wote?? '' Maurine alizidi kuongea huku analia na mimi nililia pia kwa sababu ni wazi kwamba Sina mtoto lakini nilijua fika mtoto yule anamis mapenzi ya wazazi wake na wengine wapo pale hawajui kwamba wazazi wao hawapo tena duniani..........

Kiukweli nililia sanaa baada ya kuona machozi ya binti huyu lakini nililia zaidi kwa kuwa mimi sio baba yake japo sikuweza kamwambia ukweli.......

Tulizidi kupiga story na maswali yake mda wote yalikuwa magumu kwangu '' baba leo si tutaondoka wote? Naomba usiniache!

Nilimwambia nakupenda na sikuachi ***** niliendelea na kuwasalimia watoto wengine lakini Maurine tulipokuwa tunapita aliwaambia watoto wote kuwa mimi ni baba yake na aliwasisitizia kuwa tunaondoka wote!

Upande wa pili nilimuona baba yangu na mama wakiwa wanafurahi pamoja na watoto wengine.... Walipiga picha kadhaa na mimi pia nilijumuika nao..........

Mda ulisonga mbele hatimae muda wa kuondoka uliwadia na watoto waliambiwa warudi ndani kwenda kuoga.......

Ulikuwa ni muda mgumu zaidi kwangu Maurine alilia sanaa kitendo cha mimi kuonyesha ishara za kumuacha nilimpa tsh 10000 nikamwambia '' nakupenda sana mwanangu basi nenda ukaoge uje twende '' na niliahidi nafsi yangu kwamba ningekuja tena siku nyingine.........

Nlimuachia namba yangu ya simu lakini pia anuani yangu.......... Aliondoka akiwa anaamini kwamba atanikuta pale pale ......Mara baada ya kuondoka Maurine safari yetu ilianza lakini roho yangu ilifadhaika sanaaa mda wote hususani nikiyakumbuka Yale maneno......

Mwezi mmoja badae baada ya kupata kale kamshahara kangu nilifunga tena safari kwenda kumuona Maurine........
Nilifika kule na nlipokelewa vizuri sanaaa... Muda kidogo baadae nililetewa barua ya Maurine ambayo ilikutwa kwenye begi Lake....

Sister walinipa taarifa kwamba Maurine alipotea siku moja baadae akiwa ananitafuta mimi. ............. Walitoa taarifa polisi lakini mafanikio yalikuwa F.....

Hatimae siku nne baadae kadri ya maelezo ya sister mwili wa Maurine ulipatikana ukiwa umeharibika sanaaa (amekufa) nililia sanaaaa
Nilikubaliana na Ile hali ndipo nikaamau kusoma Ile barua ya Maurine '' NAKUPENDA SANA BABA.... KWA NINI UMENIACHA?...!''Barua Ile ilikuwa ndefu japo hati yake ilikuwa bado ya kitoto ila niliielewa sana,,,,,,,,,,, sikuamini kwamba niliyoyasikia ni kweli ama ndoto........... won't forget you Maurine...... Huenda ndicho kifo chako ulichopangiwa ila naumia kwamba umekufa ukiwa unaamini mimi ni baba yako
..............
Story hii ni ya kweli ila tu nimebadilisha baadhi ya majina kwa makusudi maalum...........

Nimesukumwa kuandika haya baada ya kuona kwamba wengi tupo tayari kuchangia anasa lakini mambo ya kusaidia wahitaji kama
Wajane
Yatima
Wafungwa
Wagonjwa nk.

Tumeachana nayo ila kuchangia vitu vingine tupo tayari ili yule na yule wakuone na upewe sifa (papaa fulani)........wewe unachangia nini zaid tafakari chukua hatua.....

Je? Tangu umeanza kazi au kupata kipato kidogo, ulishasaidia moja kati ya hayo makundi maalum ya binadamu!, ukipata jibu fikiri zaidi.
 
Bujibuji samahani.......napenda sana kujua umeandika nini ili nami niweze kutoa mchango wangu......lakini ningeomba kama una kasamare au kiaudio unipatie tafadhali........natumaini sijakukwaza.......
 
Last edited by a moderator:
Nimeguswa mno na hii story tumejisahau mnoo dunia inatuhadaa hatujui kuwa tunapita Tu hapa Hua mambo mengi hatujifunzi mpaka yatufike
 
Hii story ilishaletwa hapa hata wiki haijakatika!
 
Bujibuji samahani.......napenda sana kujua umeandika nini ili nami niweze kutoa mchango wangu......lakini ningeomba kama una kasamare au kiaudio unipatie tafadhali........natumaini sijakukwaza.......

nasapoti
 
Heee!, hao watoto Mungu awasaidie. Nikikumbuka ninachokutana nacho kwa watoto kama hao huwa nashindwa lakufanya. Omba sana mtu asije akafa akiwa analitamka jina lako na akikumbuka sura yako kwa hisia. Inauma sana aisee!. Hongera kwa kutuletea ujumbe mzuri sana wa kutukumbusha
 
Jamani, nlishavoluntia kwenye kituo mwaka mzima, cha ajabu nlikuwa na aman sana moyoni na nliwafaam watoto wote 100 kwa majina na sauti... Nlipomaliza muda wangu nkaenda kufundisha shule kadhaa trust me ckuwahi kukumbuka majina ya wanafunzi wangu lkn wale watoto mpaka sasa bado nakumbuka majina yao... Naanza maandilizi pia ya ujenzi wa kituo cha watoto... 2ombeane tu!
 
Hongera kwa kuongozana na wazee wako kwenda kuwaona yatima....we ni jembe.😊
 
kwa kweli watoto hawa wanahitaji Upendo wetu kuliko hats Mali zetu. nilishawahi kwenda na nilitamani kumchukua mmoja lakini kama wakatoliki wanyosema kwenye njia ya msalaba kuwa wanaogopa kutenda mema kwa kuogopa ndivyo nilivyoogopa kumshawishi mwenzangu wa ndoa kwa kuwa nyuma kuna muhitaji mmoja kumsaidia ili let's upinzani lakini nafikiri nahitaji kumtayarisha upya.
 
Bujibuji samahani.......napenda sana kujua umeandika nini ili nami niweze kutoa mchango wangu......lakini ningeomba kama una kasamare au kiaudio unipatie tafadhali........natumaini sijakukwaza.......

Ukipata hako ka summary naomba uniforwadie LOL
 
aisee inatia simanzi yaani mweee

ila nakumbuka nami mwaka jana tulikwenda kuwaona wagonjwa wa saratani ya ngozi pale agakhan ila kwa yatima na wajene bado sijafanya hivyo naona huruma sana
 
Aisee, Mungu nisamehe, nipe muongozo na usahihi katika maamuzi yangu yote! Amen!
 
Bujibuji huenda mtoto Maurine alikuwa ni mwanao wa damu moja,
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…