Kwanza nianze kwa kusema sina hatimiliki na mtandao huu,na hivyo sina mamlaka ya kuanzisha ushindani wa aina yoyote ndani ya jukwaa hili na majukwaa mengine.Baadhi yetu ni vijana wadogo ndio tunaelekea kuitwa baba.Haina ubishi kuwa baba ni kiungo kikubwa katika familia,ni kichwa,wengine huenda mbali na kusema kuwa baba ni rais na mama pengine ndiye Makamu wa rais.Kwa sifa zote hizi bado ipo changamoto ya kumjua baba bora.Katika uzi huu ningependa tujadili kwa hoja ni kwa jinsi gani unavyomfahamu baba bora.Baba huyu aweza kuwa wewe mwenyewe,baba yako anayeishi au ambaye ametangulia mbele ya haki.Kuna mambo wewe kama baba,au babako mzazi umeyafanya,anayafanya au aliwahi kuyafanya,na mpaka sasa umekuwa msingi mkubwa na mweongozo wa maisha yako.Mfano mimi baba yangu ni mtu mwenye kujiamini na kujigamba kupita kiasi,lakini mimi nimechukua tabia ya kujiamini na kuona ndo inanifaa.Babu yangu ambaye ni baba wa baba yangu alikuwa ni mtu mpole na msikivu tabia hii pia nimeinyaka.Je wewe kama baba ukoje,babako yukoje au alikuwaje?Karibuni.
Katika maisha yangu yote sijawahi kuona baba bora kama Baba Yangu. Na hii ni Tanzania nzima, kusini mwa Jangwa la Sahara, Afrika Yote, Ulaya, Amerika, Asia, AUstralia na Dunia yote kwa ujumla.
Kinachonishangaza, hata vibinti vyangu vinanisifia kama mimi navyomsifia dingi angu. tena vinaongeza na kachumbari kabisa.
Sasa baba wa JF si ni asiyeonekana Invisible? Basi atakuwa ndo baba bora wa JF.
Konklushen: Kila mtu atamsifia baba yake
Topic Klozd!!
Mimi nimeshasema mengi sana hapa na ninajua ukimuuliza mhusika atakuambia hakunaga baba kama mimi.
Mimi nimeshasema mengi sana hapa na ninajua ukimuuliza mhusika atakuambia hakunaga baba kama mimi.
Hivi nimekusahauje?Hata wewe unaonekana ni baba mzuri, ila unaonekana utamdekeza sana matoto wa kike.
Hapana, huyu ambaye ninaye simdekezi bali ninampenda sana na ninamuonyesha kuwa ninampenda. Ninamfunza mbinu mbalimbali za kimaisha ili ikija kutokea sipo tena hapa duniani asije kushindwa ama kuhangaika sana na namna ya kukabiliana na changamoto za kimaisha.
Na kama shuleni anafanya vizuri na ni mtoto mwenye tabia nzuri basi nami ni jukumu langu kuhakikisha anapata mahitaji na matakwa yake yote ambayo yako ndani ya uwezo wangu.