Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo la biashara au kuweza kujiajiri

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,227
BAADHI YA NJIA UNAZOWEZA KUTUMIA KUPATA WAZO LA BIASHARA AU KUWEZA KUJIAJIRI PATA ELIMU YA BURE

1. TUMIA UJUZI ULIONAO
Ujuzi ulionao ndo sehemu ya kwanza kabisa ya kupata wazo la Biashara, Mfano kama wewe umejiliwa na ni Fundi wa kushona Nguo, why usianze na wewe kuwa na biashara ya aina hiyo? Kama wewe ni fundi magari why usianzishe gereji yako?

Ujuzi ulianao ndo hazina ya kwanza na ya kipekee ya kupata wazo na mara nyingi wajasirimali wengi waliofanikiwa waliacha kazi wanazo fanya na kwenda kuanzisha za aina hiyo na kuzimiliki wenyewe

2. BADILISHA HOBY YAKO KUWA PESA
Hobby ni moja ya maeneo ambayo watu huja kutajilikia, Kama unapenda gardening unaweza anza biashara ya kufanya landscape gardening

3. NUNUA BIASHARA AMBAYO TIYALI IPO
Ukishindwa kabisa kupa wazo mwanana unaweza nunua biashara ya mtu mwingine na kuindeleza, siku hizu kuna biashara kibao zinauzwa kwa sababu mbalimbali so unaweza nunua nu kuendelea nayo

4. FRANCHISE
Hii ni moja ya njia zinazotumika kwa sasa na sehemu nyingi sana, Unaweza nunua Popular Brand na kuifanyia kazi, Ingawa mara nyingi kuna mashariti ya kuambatana ikiwemo kuhakikisha unatoa huduma sawa na Brand yenyewe, na hii ni popular sana katika MAHOTELI/
MIGAHAWA, MASUPERMARKET NA MADUKA MENGINE
Na usijalibu kutumia Brand ya Kampuni Fulani bila kuwapa Taarifa maana inaweza kula kwako na ukajikuta unafilisiwa,
Na ilisha wahi kutokea kwa Kampuni ya Mabasi ya SABENA baada ya kutimia jina la Shirika la Ndege la Ubeligiji, Ila sijui walimalizana vipi, make jamaa bado wanalitumia

5. TUMIA PERSONALITY YAKO
Kuna watu unakuta either ni Mrembo sana, Handsome na kazalika, unaweza utumia huo urembo na uhendsaamu kufanya biashara, either za marketing na kazalika

6. NINI KINAKOSEKANA MTAANI?
Tazama ni kitu gani hakipo hapo mtaani and then geuza kuwa opportunity, inaweza isiwe ni mtaani ikawa ni kazini kwako, Kijijini kwenu au maeneo unayokwenda kustalehe

-Ni kitu gani huwa kinaleta usumbufu kwako na kukuchukulia muda mwingi na pesa nyingi?

- Ni huduma zipi hazipo kabisa mtaani kwako? Na ambazo ni za muhimu?

-Ni bidhaa zipi ambazo ni vigumu kuzipata mtaani kwenu?

-Ni kitu gani, wewe, Ndugu, Majirini huwa wanakilalamikia sana mtaani hapo?

7. UTALII KATIKA MAENEO YAKO
Hii nayo ni moja ya wazo, so unaweza angalia furusa za utalii kwenye maeneo uliyopo au hata kwingine na kuyafanyia kazi.

8. TUMIA TECHINOLOJIA MPYA KUANZISHA BIASHARA
Angalia mfumo wa maisha wa sasa ulivyo, vitu vinavyo tumika kwa sasa na vinavyo tumiwa na watu wengi, so mfumo wa maisha wa watu kwa sasa unaweza kukuongoza kuja na wazo la Biashara

9. ANGALIA MAKAMPUNI MAKUBWA NA TAASISI ZINGINE WANAHITAJI NINI
Unaweza tumia uwepo wa makampuni Fulani au taasisi Fulani maeneo yako kutengeneza wazo la biashara, taasisi kama Shule, vyuo, Hospitali, Makampuni kama Viwanda Migodi na kazalika, angalia ni kipi hawa watu wanaweza kuwa wanahitaji kwa wingi

10. UNAWEZA KUANGALIA KUHUSU KUUZA BIDHAA ZA WENGINE
Unaweza ukawa unauza bidhaa za watu wengine, unachukua na kuuza

11. ANGALIA NEWS NA MAKALA MBALIMBALI
Kuna channel huwa zina makala mazuri sana ya kiuchumi na biashara, so TV, radio na magazeti yanaweza toa mchango wakutosha kwa wewe kupata wazo la biashara, ila wabongo wengi wavivu kusoma

12. COPY BUSINESS IDEA AMBAYO IMEFANIKIWA KWINGINEKO
Hii ni moja ya njia zinazo tumika kwa sasa, unaweza copy idea kutoka hata India, China, na kwingineko na ukaja kuifanyia kazi huku kwa kufanya marekebisho madogo kulingana na mahitaji ya eneo husika

13. TUMIA NJIA ZOTE ZA KIUTAFITI KUPATA WAZO LA biashara

- Maonyesho ya biashara

- Magazeti,

- Kwenye taasisi za uma zinazo husika na biashara

- Kwa marafiki

14. UNAWEZA GUNDUA KITU?
Unaweza ukaja na ugunduzi wako kama walivyo fanya wakina Thomas Edson ,Michael Dell na wengineo, na ikawa ndo mwanzo wa mafanikoa kwako
Kikubwa tujitahidi kusoma wengi muda tunapoteza kusoma udaku na mambo ambayo hayatusaidii
 
Back
Top Bottom