jiamini360
Member
- Jan 26, 2016
- 35
- 19
- Je˛uwiano wa askari polisi na wananchi una kidhi mahitaji?
- Idadi ya polisi waliopo nchini haina uwiano na wingi wa watu na mahitaji halisi. Hivi sasa nchini Tanzania askari polisi mmoja anahudumia wastani wa wanachi 1,300 tofauti na viwango vya Umoja wa Mataifa ambapo askari polisi mmoja anatakiwa ahadumie wastani wa wananchi 450. Askari polisi wengiwanatumikakulindakundidogolawatumuhimu,aukatikautekelezaji wa shughuli za utawala na usalama barabarani. Hii inamaanisha kuwa kuna upungufu mkubwa wa askari polisi katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya jeshihilo.
- Je˛polisi wanaruhusiwa kutumia nguvu?
- Katika mazingira ya kawaida askari polisi haruhusiwi kutumia nguvu dhidi ya mtuhumiwa yeyote isipokuwa tu kama mtu huyo anakataa kukamatwa au anajaribu kutoroka. Ijapokuwa askari polisi anaweza kutumia nguvu, lakini hayuko juu ya sheria, na iwapo atatumia nguvu isivyohitajika atachukuliwa hatua za kinidhamu au kufunguliwa mashtaka kwa kosa la jinai.
- Kwanini Inspekta Jenerali wa polisi awajibike kwa Waziri?
- Kila serikali duniani inawajibu wa kuhakikisha kuwa kila mmoja wetu anakuwa huru na salama na hana wasiwasi juu ya maisha yake na mpendwa wake au mali yake. Serikali inatoa jukumu hili kwa polisi. Hivyo, polisi wanatakiwa kutoa taarifa serikalini kuhusu jinsi inavyotekeleza kazi zao. Vivyo hivyo, serikali pia inawajibu kwa umma kuhakikisha kuwa polisi ni wakweli, wanatenda haki, na wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi kulingana na sheria na siyo kwa matakwa yao.
- Je˛ni nani anayetoa fedha kwaajili ya shughuli za kipolisi?
- Polisi wanalipwa na walipa kodi ili kutoa huduma. Mishahara yao inatoka kwenye bajeti ya serikali kuu.Lakini,mwisho wa yote hayo inatoka mifukoni mwa walipa kodi. Yani Wewe Mwananchi. Kwa hiyo unamlipa mshahara Polisi.
- Je˛Jeshi la Polisi linapata wapi fedha zake?
- Nchi ina bajeti ambayo hutengwa kwa ajili ya utoaji wa huduma za polisi katika jamii. Jeshi la polisi hupata fedha kutoka kwenye bajeti hii na kutoka kwa wadau wa ndani na wa nje wa maendeleo ya nchi na ya Jeshi lapolisi.
- Nani hupitisha bajeti nakiasikikubwacha bajeti hiyo kinatumika kwa shughuliipi?
- Bajeti inapitishwa na Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kwa sababuulinzinausalamanisualalaMuungano.Rasimu ya kwanza ya bajeti hiyo inaandaliwa na kitengo cha mipango cha Jeshi la Polisi.Rasimu hii hupelekwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi kwa ajili ya kuridhiwa. Kutoka hapo hupelekwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi tayari kwa kupele kwa bungeni.Baada ya kujadiliwa bungeni,hatimaye bajeti ya polisi ya mwaka hupitishwa.Sehemu kubwa ya bajeti hii hutumiwa kulipa mishahara. Maeneo mengine ya matumizi ni mafunzo, upelelezi, miundombinu, ujenzi wa nyumba n.k.
- Je˛Jeshi la Polisi linaongozwa na sheria gani?
- Jeshi la Polisili linaongozwa na Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya 1977, Sheria ya Jeshi la Polisi na Wasaidizi wa Polisi (Sura ya 322 ya Sheria za Tanzania), ya Mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa mara kwa mara, Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai na Kanuni za Polisi (Police General Orders).
- Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai na Sheria ya Ushahidi na Kanuni za Adhabu˛ni nini?
- Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai inaeleza njia ambazo polisi na mahakama wanapaswa kufuata katika kuwashughulikia wahalifu. Hii ni pamoja na mamlaka ya polisi na taratibu wanazotakiwa polisi wazifuate. Kwa mfano, kitendo kimojawapo kinaelezea matumizi ya nguvu ya polisi pale anapomkamata mtuhumiwa na sehemu nyingine inaelezea nguvu na kazi za polisi anapofanya uchunguzi.
- Sheria ya Ushahidi
- inaeleza kwa undani kinachokubalika mahakamani kama ushahidi. Kwa mfano, sehemu moja ya sheria hiyo inasema kuwa ushahidi uliopatikana kwa kutumia nguvu hauwezi kutumika kama ushahidi halali,kamaikibainikanamahakamakuwaulipatikanakwanjiazisizohalali.
- Kanuni ya adhabu (Penal Code)
- inatoa ufafanuzi wa kila uhalifu unaosadikiwa kuwa ni matendo ya kihalifu nchini Tanzania. Pia inaelezea tabianamatendo,yanayoitwamakosa,yanafuatiwanaadhabukwakilakosa.
- Sheria ya Polisi inasemaje?
- Sheria ya polisi kwa kawaida inaeleza kuhusu uendeshaji wake, nidhamu, mamlaka na kazi za Polisi, Polisi wa Akiba na Polisi wasaidizi na mambo mengine yanayolihusu jeshi hilo. Inaeleza kwa kina njia mbalimbali zinazopaswa kuchukuliwa katika kuhakikisha haki na utendaji wa kulinda sheria na kanuni za nchi zinafanyika kwa haki na kwa uwazi.
- Nini maana ya“Utawala wa Sheria”?
- Hii ina maana kuwa sisi, sote, mkubwa au mdogo, tajiri au maskini, mwanaume au mwanamke, hata serikali na watumishi wa umma kama vile polisi, tunatakiwa kutii sheria na lazima tuishi kwa mujibu wa sheria zilizowekwa nchini mwetu chini ya Katiba yetu. Hakuna aliye juu ya sheria. Pia ina maana kuwa kila tendo linalofanywa na askari polisi lifanywe kulingana na sheria,na iwapo hatafanya hivyo askari polisi huyo atawajibika mbele ya sheria. Vilevile inamaanisha kuwa sheria zinazotungwa ni lazima ziwe za haki na usawa.
- Askari polisi anaweza kuadhibiwa akifanya makosa?
- Ndiyo. Askari polisi kama mtu mwingine yeyote iwapo atavunja sheria anaweza kuadhibiwa. Kwa kweli kwa kuwa yeye ni mtu aliyepewa dhamana yakusimamia utekelezaji wa sheria anatakiwa kupewa adhabu kali zaidi kwa kuvunja sheria.
- Askari polisi ana adhibiwaje?
- Kuna njia nyingi za kuwaadhibu askari polisi waliofanya makosa. Kama ametenda kosa la jinai hivyo anaweza kupelekwa mbele ya mahakama na akahukumiwa kama mtu mwingine yeyote au akapelekwa mahakama ya kijeshikutegemeananaukubwawakosalinalomkabili.Iwapoamekosaadabu, amekuwa na tabia mbaya au hakutekeleza majukumu yake inavyotakiwa, ataadhibiwa kulingana na taratibu na kanuni za Jeshi hilo.
- Askari polisi wanafanya kazi hatarishi.Je˛wanakinga ya bima?
- Hapana, askari polisi wa Tanzania hawana bima. Familia ya askari polisi aliyeuwawaaukufarikikaziniinapewafidianayulealiyeumiakazinianaweza akalipwa fidia au posho kulingana na matakwa ya waziri mwenyedhamana.
- Je˛askari polisi anatakiwa kukubali kila amri aliyopewa na mkuu wake wa kazi au mtu yeyote mwenye mamlaka ya kutoa amri kama vile Waziri˛Mkuu wa Mkoa˛Mkuu wa Wilaya˛Makamishna mbalimbali n.k?
- Hapana. Askari polisi lazima atii amri ikiwa tu ni halali.Anaweza akawajibika kwa chochote kibaya atakachokifanya kama ameamriwa kufanya hivyo. Kamwe hawezi kujitetea kwa kusema kuwa mkuu wake au mtu fulani mwenye mamlaka alimwamuru kutenda jambo baya na lililo kinyume cha sheria. Hilo halitamlinda.
- Je˛natakiwa kuzingatia kila agizo la askari polisi?
- Ndiyo, kama ni amri halali inayohusiana na kazi yake. Kiukweli kila mmoja ana wajibu wa kumsaidia askari polisi katika kutekeleza kazi yake; hasa iwapopolisianajaribukusimamishamapiganoaukuzuiauhalifuauanajaribu kumzuia mtu kutoroka katika ulinzi wake. Ki ukweli, iwapo unazo taarifa zinazohusu uhalifu ni wajibu wako kupeleka taarifa hizo kwa polisi. Pia ni wajibu wako kutomhifadhi mtu anayejulikana kuwa ni mhalifu. Vilevile una wajibu wa kutoa ushahidi mahakamani endapo unajua au umeona kitufulani kuhusiana na shauri lililoko mahakamani.
- Je˛naweza kuambatana na askari polisi iwapo ataniomba kufuatana naye mahalifulani?
- Hapana. Hata hivyo, iwapo askari polisi anakuomba ufuatane naye ili ukawe shahidi wa kitu anachokifanya kama sehemu ya kazi yake, kama vile kumkamata mtu, kutwaa mali, au kuchunguza eneo la uhalifu, hivyo unaweza kuambatana naye na kumsaidia. Kwa kawaida mtu huyo anaitwa shahidi anayeweza kuieleza mahakama alichokiona bila kuegemea upande wowote.
- Katika Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, watu walioko chini ya “kizuizi”–watuambaohawakukamatwanaaskaripolisi,lakiniaskaripolisi asingependa kuwaruhusu waondoke kwa vile wanaweza kuwa na taarifa kuhusiana na uhalifu–wanawezakushikiliwakwaajiliyakuhojiwanapolisi ndani ya masaa manne (4) tangu walipowekwa chini ya kizuizi. Ikiwa uko chini ya kizuizi unayo haki ya kuongea na mwanasheria au ndugu aurafiki.
- Ikitokea askari polisi ananiomba kwenda kituoni˛je naweza kwenda?
- Hapana. Ni vizuri kushirikiana na polisi lakini siyo muhimu kwenda kituo cha polisi isipokuwa kama askari polisi amekukamata rasmi kwa utaratibu unaotambuliwa.Vinginevyo,iwapoanatakakukuhojiauanafanyauchunguzi kuhusu uhalifu, anatakiwa kukuletea wito wa maandishi wa kukutaka ufike kituoni. Mpaka hilo lifanyike huwezi kulazimishwa kwendakituoni.
- Je˛nilazima nijibu maswali yote anayouliza askari polisi?
- Ni vizuri kujibu maswali yote kwa ukweli na uwazi na kuwaeleza askari polisi mambo yote yaliyotendeka unayoyajua kuhusiana na tukio husika. Iwapo hujui chochote, askari polisi hawezi kukulazimisha kutoa maelezo au kukusemea. Daima ni vizuri kuhakikisha kuwa mtu mwingine yuko pamoja nawe wakati unapohojiwa.
- Je˛askari polisi anawajibu wa kunisaidia wakati wa dharura?
- Ndiyo. Askari polisi anatakiwa kutoa msaada kwa kila mtu bila kujali utajiri nahaliyakimaishayamtu,aunafasiyamtukatikajamii.Kulingana na kanuni za maadili kazi kubwa ya polisi ni kutoa ulinzi kwa kila mtu bila woga au upendeleo ikiwa ni pamoja na kuwatuliza watu kiakili,kuhuzunika nao na kuwajali, kuwa tayari kutoa huduma na kuwa na uhusia nao
- Je˛nitafanyaje iwapo askari polisi hatakikunisaidia?
- Kuvunjwa kwa makusudi au kudharau wajibu wa kazi kwa askari polisi ni kosa linalostahili adhabu ya kifungo endapo itathibitika. Iwapo askari polisi hanamsaada,naweumedhurika,unawezakulalamikakuhusujambohilokwa afisa wa polisi wa ngazi ya juu. Katika hali hiyo askari polisi huyo anaweza kuonekana anahatia ya kushindwa kutimiza wajibu wake.
- Je˛askari polisi wanaweza kufanya chochote watakacho?
- Hapana hata kidogo. Wanaweza kufanya kile tu kinachokubalika kisheria. Kwa kweli wanatawaliwa na kanuni nyingi na kali. Hii ni pamoja na kanuni zao wenyewe, taratibu zilizowekwa kwa ajili ya uhalifu (criminal codes), amri zinazotolewa na mahakama ya rufaa, na miongozo kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
- Lakini iwapo askari polisi hawatii sheria hizo inakuwaje?
- Unaweza kulalamika kwa afisa wa polisi wa cheo cha juu yake, au mkuu wa kituo au kwa hakimu au Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kulingananauzitowasualalenyewe.Nivizurikulalamikakwamaandishina kupata uthibitisho wa maandishi wa kupokelewa kwa lalamikolako.
- Nikiwa natembea mtaani˛ je askari polisi anaweza kunisimamisha na kuniuliza chochote anachopenda?
- Hapana. Kwa ujumla askari polisi hawatakiwi kuwaingilia watuwanaofanya shughuli zao halali.Lakini iwapoatakudhania kuwa unazurura mtaani hususani wakati wa usiku anayo haki ya kukusimamisha na kukuuliza jina lako na shughuliunayofanya.Ikiwakunakituanachokitiliashakajuuyajambofulani unaweza kukamatwa. Askari polisi wanatumia mamlaka haya mara nyingi kama njia ya kuwakamata washukiwa na watu wenye mazoea ya kufanya uhalifu. Aidha, matumizi yaliyovuka mpaka ya mamlaka haya yamejadiliwa mara nyingi na kamati za maboresho na kulaaniwa.
- Je˛askari polisi anaweza kunizuia nisishiriki kwenye maandamano au mkutano wahadhara?
- Unayo haki ya kushiriki katika maandamano ya amani.Ibara ya 20 yaKatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa haki kwa kila mtanzania kushiriki katika mikusanyiko ya amani. Lakini taarifa ya maandishi lazima itolewe polisi saa 48 kabla ya kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano katika maeneo ya wazi. Taarifa hiyo lazima itolewe kwa kiongozi wa polisi wa eneo ambako mkusanyiko huo unapendekezwa kufanyika. Askari polisi
- anayepokea taarifa hiyo anaweza kusema kuwa mkutano unaopendekezwa hauwezikufanyikaiwapoanaaminikuwamkutanohuounawezakusababisha uvunjifu wa amani, usalama wa umma, kudumishwa kwa utulivu, kutumiwa kwa makusudi yaliyo kinyume cha sheria au iwapo matakwa ya utoaji wa taarifa ulioelezwa hapo juu haukutimizwa.
- Iwapo yanafanyika na baadaye yakageuka machafuko, polisi wanaweza kuyazuia yasiendelee, wakawataka wananchi waondoke na kuchukua hatua iwapo hawatawanyiki.
- Kwa upande mmoja askari polisi wana wajibu wa kuhakikisha kuwa amani inakuwepo. Kwa upande mwingine, askari polisi wana wajibu wa kuwawezeshawananchikutumiahakiyaoyamsingiyakufanyamikutanoya hadhara kwa amani na utulivu.
- Je˛polisi wanaweza kutumia nguvu kuvunja mkutano wa mtaa au maandamano?
- Ndiyo. Chochote polisi wakifanyacho kinatakiwa kuwa kwa kiasi. Hawapo kwa ajili ya kuwaadhibu watu, wapo pale kuhakikisha watu wapo salama na sheria na amani hazivunjwi. Hivyo kanuni ni kwamba katika kudhibiti mkusanyiko wa watu askari polisi watatumia nguvu kama suluhisho la mwishobaadayahatuanyinginezotekushindikana.Kamanguvuitalazimika kutumika basi iwe ya kadiri, inayoendana na mazingira na itumiwe kwa muda mfupi iwezekanavyo.
- Je˛askari polisi anaweza kutumia bunduki(nguvukubwa inayoweza kusababisha maangamizi?)
- Nguvu kubwa zitumike inapolazimika tu, wakati njia nyingine zote za udhibitizikiwazimejaribiwanakushindikana.Askaripolisianawezakutumia bunduki dhidi ya mtu anayetoroka, au anayefanya jaribio la kutoroka toka kizuizini au kutoroka asikamatwe - lakini pale tu askari polisi anapokuwa na sababu za msingi za kuamini kuwa hawezi kuzuia utoro huo kwa njia nyiasababuzamsingizakuaminikuwamtumwingine,au askari polisi wenyewe, wako hatarini kuumizwa vibaya.nginenaametoaonyokwamtuhuyokuwayukokaribukutumiabunduki, na mtu huyo hajali onyo lililotolewa.
- Pia askari polisi anaweza kutumia bunduki dhidi ya mtu ambaye anatumia nguvukumwondoamtumwinginekutokakizuizihalaliaukuzuiaukamatwaji halali wa mtu mwingine. Hata hivyo, katika suala hili, askari polisi anaweza tu kutumia bunduki iwapo hakuna njia nyingine ya kumzuia mtu huyo na iwapoaskaripolisian
- Je˛askari polisi afanye nini kamawatu ni wakaidi na wanarusha mawe au kuharibu mali?
- Askari polisi wana wajibu wa kulinda uhai na mali za watu. Lakini kuna utaratibu unaotakiwa kufuatwa katika utekelezaji wa jukumu hilo. Kwanza kutoa onyo mara tatu la kuwataka watu watawanyike na muda wa kutii amri hiyo lazima utolewe. Kama bado hawatawanyiki nguvu ya kadiri inaweza kutumika. Na aina ya nguvu hizo ni matumizi ya mikanda ya ngozi, virungu au silaha zinaweza kutumika pia kama vile risasi za mpira, maji ya kuwasha au mabomu ya machozi. Virungu visipigwe kichwani na mabegani bali vilengwe chini ya kiuno. Wakati wote polisi lazima wajitahidi kutumia njia yenye madhara kidogo na kutumia njia nyingine kama ile imeshindikana. Iwapopolisiwatatumiarisasizamotowafanyehivyokamanjiayakujihami, na lazima pawepo na maonyo ya wazi kuwa risasi zitatumika. Hapa pia kanuni ni kutumia nguvu kiasi. Hivyo, upigwaji wa risasi lazima ulenge chini na katika sehemu ya kundi inayoonekana kuwa tishio siyo kwa lengo la kusababisha mauaji bali kuwatawanya. Mara kundi hilo linapoonyesha dalili ya kutawanyika upigaji wa risasi lazima usimamishwe. Majeruhi lazima wasaidiwe kwa kupelekwa hospitali mara moja. Hata hivyo kila askari polisi anawajibika kuandika taarifa ya uhusika wake kwa ajili ya kumbukumbu. Lakini njia iliyobora ni ile ya kushauriana kwa mazungumzo na waandamanaji.
- Je˛askari polisi wanaweza kunishikilia mafichoni au wasimweleze mtu yeyote kuwa wananishikilia?
- Hapana. Baadhi ya askari polisi wamezoea kufanya hivyo mara kwa mara, lakini hii ni kinyume cha sheria. Mara askari polisi wanapokuweka rumande ni jukumu lao kuangalia afya yako na kuzilinda haki zako. Iwapo utapata madhara yoyote au haki zako hazitaheshimiwa bali zikavunjwa kwa namna yoyote ile polisi watawajibika. Hili ni jambo muhimu la kisheria la kukumbuka.
- Halafu, kutokana na ukweli kuwa askari polisi wana wajibu wa kuandika taarifazawatuwotewanaofikakituonikwenyekitabuchaochakumbukumbu za kila siku, kitaonesha muda ulioletwa hapo kituoni kwa mahojiano na wakati gani ulikamatwa.
- Mwisho, kwa kuwa unayo haki ya kuwa na mwanasheria wako wakati wa kuhojiwa, sehemu ya mahabusu lazima ijulikane na iweze kufikiwa na mwanasheria wako, marafiki, familia aujamaa.
- Je˛ askari polisi anaweza kunishikilia kituo cha polisi au naweza kuondoka nikitaka?
- Kama umekamatwa bila kufuata sheria, kanuni na taratibu zinazokubalika, huwezi kushikiliwa katika kizuizi kinyume cha matakwa yako. Iwapo polisi wamekuita kwa ajili ya mahojiano una wajibu wa kushirikiana nao na kuwasaidia katika uchunguzi wao. Lakini mahojiano yanapaswa kufanyika papohaponakwaufanisinayasiendeleekwamudamrefu.Kwaujumla,kama umeshikiliwa lakini hukukamatwa, polisi wanaweza kukuhoji kwa muda wa masaa manne na siyo zaidi. Katika mazingira maalumu wanaweza kuomba kuongeza muda wa mahojiano.
- Iwapo askari polisi haniachilii niondoke˛ nifanyeje?
- Kuwekwa mahabusu bila ridhaa yako hata kwa muda mfupi ikiwa hujakamatwa kwa kufuata taratibu ni kosa kubwa. Hii inaitwa kushikiliwa kinyume cha sheria na wewe au familia yako au rafiki wanawezakulalamika dhidi ya askari polisi huyo kwa mkubwa wake kimadaraka au kicheo aukwa hakimu. Kubwa zaidi, kupitia mwanasheria wako, familia, ndugu au rafiki unaweza kwenda moja kwa moja Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufaa kuomba kutolewa kwa amri ya kufikishwa kortini kuangalia uhalali wa kushikiliwakwakoiliuwezekuachiliwamaramoja.Aidha,malalamikoyako yanaweza kupelekwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi au Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
- Je˛askari polisi anaweza kunikamata bila kuniambia sababu?
- Hapana. Askari polisi anaweza kumkamata mtu ikiwa tu kuna sababu za kufanya hivyo. Mathalani, mtu amekamatwa papohapo akifanya uhalifu, au mazingira yote ya uchunguzi yanaonyesha kumtuhumu mtu huyo, au mtu huyo anaonekana akimsadia mtu mwingine kufanya uhalifu kabla, wakati au baada ya tukio kutokea, hivyo anaweza kukamatwa. Ni lazima kuwe na ‘sababu za msingi’ za kumkamata mtu. Mtu fulani kumtaja mtu mwingine katika taarifa ya awali ya upelelezi haiwezi kuwa sababu ya ukamataji. Lazima pawepo na kitu cha ziada chenye sura ya ushahidikitakachowezesha kukukamata. Kwa bahati mbaya kuna baadhi ya watu hukamatwa isivyo halali na pasipo sababu za msingi.
- Je˛ askari polisi anahitaji kuwa na kibali ili kunikamata mimi au mtumwingine?
- Inategemea aina ya kosa. Kuna makosa maalumu yaliyoorodheshwa katika Sheria ya Makosa ya Jinai yenye kuruhusu askari polisi kumkamata mtubila ya hati ya ukamataji, hata hivyo makosa mengine yote yanamtaka askari polisi kupata hati ya kukamata kutoka kwa hakimu, Katibu Kata au Katibu wa Baraza la Kijiji. Endapo askari polisi watamkamata mtu bila ya kuwa na kibali, ni lazima watoe taarifa kwa hakimu kuhusu ukamatajihuo.
- Kama polisi watanikamata bila ya kuwa na hati ya ukamataji˛ wanalazimika kumuarifu mtu yeyote kuwa nimekamatwa?Je˛ mtu huyo ataelezwa mahali nilipo?
- Ndiyo, kama polisi watakukamata bila hati ya ukamataji,lazimawatoetaarifakwahakimukuhusu ukamataji huo. Pia, pasipokujali umekamatwa kwa hati ya ukamataji au bila hati ya ukamataji, unayo haki ya kuwasiliana na mwanasheria, familia au rafiki yako mara baada ya kukamatwa. Unaweza kuwajulishasehemuuliponasababuzakukamatwa kwako.
- Iwapo askari polisi wananituhumu kuwa nimefanya uhalifu˛ je˛ wanawezapiakuwakamata wanafamilia yangu?
- Hapanahaiwezekani.Hakunahatiayakufungamanishwa.Mtukuwanahatia au kukosa hatia lazima kuamuliwe kwa kuangalia vitendo vya mtu binafsi na siyo kwa sababu mtu huyo yupo karibu na au anahusiana na mtu fulani ambayenimtuhumiwa.Uhuruwamtuyeyotehauweziukatwaliwaisipokuwa kwa sababu maalum ya sheria.
- Askari polisi hawawezi kuwatisha wanafamilia au marafiki au kuwafungia mahabusu kama njia ya kumbana mhalifu akiri kosa au kama amekimbia ajisalimishe polisi. Njia hii ya kuteka na kuwashikilia watu mateka ni kinyume cha sheria na ni kosa kubwa.
- Haijalishi kesi wanayoishughulikia ni ngumu kiasi gani, polisi hawawezi kutumia njia zisizo halali ili kumlazimisha mtuhumiwa kujisalimisha au kukiri kosa. Watu pekee wanaoweza kukamatwa ni wale ambao kunasababu za msingi dhidi yao za kufikiriwa kuwa wamefanyauhalifu.
- Je˛askari polisi wakinikamata˛wanaweza kunishikilia kwa muda wowote wanaopenda?
- Hapana!Ikiwaumekamatwanapolisinakuwekwamahabusubilakibali,basi askaripolisinilazimawakupelekemahakamanindaniyasaa24.Hatahivyo, iwapo umekamatwa kwa kibali kwa kosa ambalo adhabu yake ni kifo, au umekamatwakwakosanapolisihawanakibali,basipolisilazimawakupeleke mbele ya mahakama mapema iwezekanavyo. Ikiwa hujakamatwa, lakini umeletwa kituoni kwa ajili ya kuhojiwa, basi askari polisi lazima waliweke suala hilo katika kumbukumbu zao pia.
- Inakuwaje basi watu hukamatwa sikuya Ijumaa jioni na kuwekwa mahabusu mpaka siku ya Jumatatu?
- Haitakiwikuwahivyo.Inapokuwahaiwezekanikumpelekamtualiyekamatwa mahakamanindaniyasaa24kuanziaalipowekwamahabusu,afisamsimamizi wa kituo cha polisi ambako mtuhumiwa ameshikiliwa anawezakuichunguza kesi na, isipokuwa kama kosa linaonekana na afisa huyo kuwa ni kubwa, anaweza kumwachia mtu huyo baada ya kuweka dhamana kwa kiasi cha kutosha akiwa na wadhamini au bila ya wadhamini, na kumtaka kuhudhuria mbele ya mahakama katika muda na mahali palipotajwa kwenyedhamana.
- Nitawezaje kujua yotehaya?
- Kisheria, wakati unapokamatwa askari polisi anatakiwa kukujulisha haki zako zote. Pia kuna taasisi nyingi ambazo zinaweza kukusaidia kujua haki zako, kama vile Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Taasisi zinazotoa msaada wa huduma za kisheria pia zinaweza kukusaidia iwapo hujui haki zako za kisheria.
- Je˛askari polisi anaweza kunipiga niwapokizuizini?
- Hapana. Hawezi kukupiga, kukutisha au kukutia hofu. Kufanya hivyo ni kinyumechasheria,kanuninataratibuzakipolisi,naaskaripolisianayefanya hayo anaweza kuadhibiwa kwa kosa hilo.
- Sheria inasema kuwa mtu akiwa kizuizini,atatakiwa kutendwa kiubinadamu na kuheshimiwa na hatapaswa kutendewa ukatili, kinyume na ubinadamu au kudhalilishwa. Pia iwapo uko katika kizuizi cha polisi, unaweza kuomba kupatiwa matibabu au ushauri kuhusiana na ugonjwa au majeraha uliyonayo.
- Je˛askari polisi anaweza kunilazimisha kukirikosa?
- Hapana. Askari polisi anayo haki ya kukuhoji, lakini hawezi kukulazimisha kuongea kitu chochote ambacho huna habari nacho, kitu chochote ambacho hutaki kukisema au kukiri makosa ambayo hukuyafanya. Ungamo la kosa linalofanywa mbele ya askari polisi kwa namna yoyote ile halitakubalika mahakamani kama ushahidi.
- Je˛Tume ya Hakiza Binada muna Utawala Bora inajukumu la kufuatilia nguvu na mamlaka ya polisi?
- Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ni taasisi huru ya Serikali, iliyoanzishwa kama taasisi ya kitaifa iliyo kitovu cha kukuza na kulindahakizabinadamunawajibunautawalaboranchiniTanzania.THBUB ilianzishwa chini ya ibara ya 129(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaya1977nailianzakazitarehe1Julai,2001baadayakupitishwakwa SheriaNa.7yaTumeyaHakizaBinadamunaUtawalaBorayamwaka2001. Kulingana na kifungu cha 6(1) cha sheria hiyo pamoja na mambo mengine, Tume ina majukumu ya kupokea na kuchunguza malalamiko yanayohusu uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora na kutoa mapendekezo. Iwapo mapendekezo hayo hayakutekelezwa, inaweza ikapeleka masuala hayo mahakamani. Aidha, Tume hutoa mapendekezo kuhusu urekebishaji wa sheria iliyopo au inayotarajiwa kutungwa, kanuniau utaratibu wa kiutawala ili kutilia maanani masuala ya haki za binadamu na utawala bora
- Tume ya Haki za Binadamu na UtawalaBora
- S.L.P 2643, DAR ESSALAAM Simu: +255 22 2135747/8
- Barua Pepe: chragg@chragg.go.tz Tovuti:http://www.chragg.go.tz
- soma zaidi
- http://www.tanzania.go.tz/egov_uplo...uhusu_polisi_lakini_unaogopa_kuyauliza_sw.pdf
Attachments
-
upload_2016-1-26_22-39-52.png2 KB · Views: 132
-
upload_2016-1-26_22-43-26.png5.8 KB · Views: 122
-
upload_2016-1-26_22-44-59.png1.6 KB · Views: 146
-
upload_2016-1-26_22-45-40.png1.6 KB · Views: 131
-
upload_2016-1-26_22-58-45.png3.5 KB · Views: 117
-
upload_2016-1-26_23-0-30.png938 bytes · Views: 111
-
upload_2016-1-26_23-3-35.png3.7 KB · Views: 129
-
upload_2016-1-26_23-3-57.png3.7 KB · Views: 128
-
upload_2016-1-26_23-5-42.png721 bytes · Views: 126
-
upload_2016-1-26_23-7-48.png685 bytes · Views: 122
-
upload_2016-1-26_23-10-37.png621 bytes · Views: 131
-
upload_2016-1-26_23-11-23.png1.8 KB · Views: 124