Baada ya uhakiki wa watumishi,tunahitaji uhakiki wa Deni la Taifa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,684
149,887
Baada ya kuonekana mabilioni mengi ya serikali yalikuwa yanatumika kulipa watumishi hewa,je tuna uhakika gani matrilioni ya shilingi tunayotenga kila mwaka kulipa deni la Taifa yanalipa deni halali?

Kwanini nguvu kubwa inayoelekezwa kwenye kuokoa fedha zinazotokana na kulipa watumishi hewa hatuioni ikielekezwa kwenye kuhakiki hili deni la Taifa?!
 
Kweli kuna haja ya uhakiki kwa sababu JPM alisema hii nchi ilikuwa imegeuzwa shamba la bibi.Bahati mbaya hata bunge letu halinauwezo kuanzisha suala kama hili,maanzimio yote ESCROW hakuna hata moja labda kwa utashi wa kiongozi mkuu
 
ni kweli moja mkakati wa kufanya hapa kwanza ni wizara ya fedha iwaorodheshe wadeni wetu na kisha ni kuwauliza mabalozi nchi zao zinatudai kiasi gani? tena wakati unamuuliza balozi unakuwa umemfanyia ziara ya kushitukiza ofisini kwake
 
kila mtanzania anadaiwa milion afu bado hujaweka yale madeni ya kawaida unayodaiwa na watu unaweza ona hali ikoje
 
mwee
1. deni la taifa
2. mkopo wa benki
3. mkopo wa Bodi
4. mkopo wa vikoba
5. mkopo wa ndugu / ofisn
6. mkopo wa mahari maana weng hatumalizi

duuh tutapona kwel.......
 
Hivi nadaiwa million moja kwa kipi hasa..?

kila mwezi nnalipa kodi tsh..145,000/= PAYE...

bado kwenye Huduma za jamii...nalipa kodi.,

hivi hizo hazitoshi walipe hilo deni ....?

kwa nini tunadaiana madeni hewa......?

yaani wengine watumie,afu sisi ndo tulipe....sio fair
 
mwee
1. deni la taifa
2. mkopo wa benki
3. mkopo wa Bodi
4. mkopo wa vikoba
5. mkopo wa ndugu / ofisn
6. mkopo wa mahari maana weng hatumalizi

duuh tutapona kwel.......

Asante kwa kunisemea ndugu.....yote hayo yananihusu...isipokuwa hiyo no..6.... nshamalizana na ukweni.....

HAPA MADENI TU....
 
Asante kwa kunisemea ndugu.....yote hayo yananihusu...isipokuwa hiyo no..6.... nshamalizana na ukweni.....

HAPA MADENI TU....
dah hongera aisee nahis nikija kumaliza namba sita na thaman ya hela yetu hii sjui itakuaje?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom