Baada ya miaka minne, nani aliyefanikiwa kupokea kijiti cha Lady JayDee?

sinza pazuri

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
2,522
7,370

Ikiwa imepita miaka takriban mitano tangu isambazwe propaganda kwamba wakati wa Jide umeisha kwaio ilimbidi akabidhi kijiti kwa msanii mwingine wa kike.

Kwa mtazamo wako unadhani ni nani aliyeweza kuvaa viatu vya Jide mpaka sasa na vikamtosha kuwa malkia wa bongofleva?

Mwasiti? Lina? Rachel? Vanessa? Au Nandy?
 
Binti amekosa Mjegejo wa maana wa kumtuliza tu. Angeupata hakika angekuwa level zingine
 
Kusema kweli amebaki na sifa ya u legend ila kwasasa hakuna anachoimba nyimbo zake nyingi kwaya si kwaya melody zake hazivutii basi tu amebaki na heshima ya u legend na die hard fans.
Hata mnaomsifia si ajabu kwenye list za nyimbo zenu hakuna nyimbo zake mpya ila utakuta mna nyimbo za akina nandy lulu diva na madada wengine.
 
kwa sasa bila kupepesa macho....kijiti chake kinashikiliwa na nandy kama sio vanessa mdee
 
Mpaka sasa hamna msanii/ mwanamuziki wa kike ambaye ni nembo! Jide licha ya kuwa yupo kimya imebidi abaki na kijiti tu.
 
Kusema kweli amebaki na sifa ya u legend ila kwasasa hakuna anachoimba nyimbo zake nyingi kwaya si kwaya melody zake hazivutii basi tu amebaki na heshima ya u legend na die hard fans.
Hata mnaomsifia si ajabu kwenye list za nyimbo zenu hakuna nyimbo zake mpya ila utakuta mna nyimbo za akina nandy lulu diva na madada wengine.
Ni kweli ila waliopo wameshindwa kushindana hata na nyimbo zake za zamani.
 
Vanessa ni mara tano zaidi ya Jide!
Bora Nandy,maana nililazimika kumtafuta baada ya kunikonga moyo..sikuwa namfahamu kabisa.
Vanessa kuna tangazo la mtandao wa simu ndo lilinifanya nimjue na tena ni baada ya mpenzi wangu kuona wivu eti nalipenda tangazo kwa sababu ya Vanesa!Vinginevyo sielewi wimbo wake hata mmoja!!
 
Vijana wa siku hizi mna matatizo sana.
Huyu dada hana wa kufananishwa nae hapa bongo.
Huu wimbo wake tu huwezi kufananisha na nyimbo zote za Nandy.
Vijana fateni maudhui sio sura wala makeup.

Huyo nandy wenu anaweza kusimama bila promo kama huyu dada?
Mziki umechange huwezi fanya kitu chochote zama hizi ukakifanya vile vile kama kilivyofanyika miaka 10 iliyopita utafail.
Mziki bila promo now ni ngumu, kipindi jay d anaanza mziki nyimbo zilikuwa chache hata vituo vya redio vilikuwa vinapokea nyimbo chache na kulazimika kuzipiga zote yani zamani kuingia studio ukarekodi ndiyo ilikuwa kazi, ukisharekodi basi ujue umetoboa tu ndiyo maana hata watu kama akina dudu baya waliweza kutoboa.
Unaufahamu mziki flani jamaa anaimba lafudhi ya kichaga ambaye sasa hivi ni mmoja wa watengenezaji wa kipindi cha ubongo kids yule anaongea sauti ya yule twiga,
Aliimba mziki sijui ni jinsi gani ni namna gani tutawin maishani ....
Ile ilikuwa ni freestyle studio baada ya jamaa yake kufunga vifaa wakawa wanavijaribisha lakini kutokana na nyimbo kuwa chache wimbo ule ikaenda redioni.
Hata biashara now zinahitaji promo ndiyo maana sehemu kubwa ya muda kwenye tvs na redio utaona ni matangazo ya kibiashara tofauti na zamani.
In short kwasasa mziki unahitaji promo zama zimebadirika bila promo lazima ufail ndiyo maana kuna nyimbo nzuri hazijahit coz zimekosa promo kisa waimbaji ma underground hawana ela
 
Mkuu unajikanyaga mwenyewe.

Kuna watu wamejibu hapa kuwa kijiti chake kimeshikiliwa na nandy sijui na Vanessa.
Nikawauliza hao mnaowashindanisha naye wanaweza kukomaa wenyewe bila promo?
Maana yeye hadi leo yupo anaimba anasikika anapata tuzo na still hafanyi media tour za kulazimisha.
Hii ndio mada mkuu.
Ukianza kusema kuwa zamani wasanii walikuwa sijui wachache sijui media zilikuwa chache utakuwa hueleweki.

Jaydee anasikilizwa na watu wote kwa mood yyte ile tofauti na hao watu wenu.
Maudhui ya wimbo huu huwezi linganisha na maudhui ya nyimbo za Nandy au Vanessa.

Anapopita Vanessa now jide alishapita muda mrefu sana enzi hizo hata social media hazikuwepo.
Kama ni connection anazo za kutosha tu ambazo hizo hizo ndio Vanessa anajipachika huko sasa.
 
Vijana wa siku hizi mna matatizo sana. ?
Lady jay d kabaki na heshima ya ukongwe kwasasa hana mziki mzuri ana nyimbo hazina hata melody za kueleweka anaimba mziki kwaya si kwaya wala nini.
Sema tu ana ile fan base kubwa yan die hatd fans ambao wanabishana na kumtetea mitandaoni huku miziki yake mipya hawana na wala haiwasikilizi wamejaza nyimbo za akina vanessa na ndani kwenye music devices zao.
Kila zama na mfalme wake alikopita jide vanessa ndiko anapita leo kwakuwa hakuwepo kipindi kile na yeye kaenda mbele zaidi na kujaribu kufanya kilicho bora zaidi kwa zama hizi.
Jide kabaki tu na sifa ya u legend ila kwa sasa hata yeye mwenyewe anashindwa kuimba mziki mzuri kama aliokuwa akiimba awali ndiyo maana miziki yake mipya inachuja haraka sijui kazeeka
 
Uzungu unawamaliza wadada wa siku hizi!
Muziki wa sasa umewarahisishia vitu vingi sana wasanii waliopo lakini bado wanashindwa kufika kule walipofikia wenzao kipindi ambacho hakukuwa na vyote hivi.
Wadada wa zamani wengi sana waliliwa uroda na waandaaji wa muziki kwa ahadi za kurekodi na bado wakakosa nafasi ya kurekodi.
Ila kwa sasa huwezi ukamdanganya kwa ahadi za kitambo hiko, lakini bado hakuna anayefanya vizuri! Jide atabaki kuwa Jide, kama mtabisha muwaulize wenzie kina Rah P, Sister P, Zay B, Ray C na wengineo kama ilikuwa ni kazi rahisi kuwa alipo Jide.
Mambo yalikuwa magumu kwao mpaka wameususia mziki kabisaa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom