Makanyaga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2007
- 10,810
- 7,090
WASOMI na wanaharakati nchini wamempongeza Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, kwa kuandika kitabu na kuelezea maisha yake binafsi pamoja na mambo mazuri na mabaya aliyowafanya wakati wa uongozi wake.
Wamesema kitabu hicho kitakuwa mwongozo kwa viongozi waliopo na watakaoingia madarakani kwa maslahi mapana ya taifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga, alisema Mkapa amelitendea haki taifa kwa kueleza vizuri uzoefu wake kwa mambo mazuri na mabaya aliyofanya na yanayofanyika.
Alisema kitabu hicho kitasaidia kupunguza makosa ambayo yangefanywa na viongozi wajao na kuwa darasa kwa serikali katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali.
“Nampongeza sana Rais Mkapa kwa kuandika kitabu hiki, amelitendea haki taifa. Uongozi wa juu alioshika ni uzoefu mkubwa aliotengeneza, hivyo kupitia kitabu hiki kinachoelezea mema na mabaya aliyofanya, itasaidia kupunguza makosa ambayo yangefanywa na viongozi wanaokuja," alisema.
Mkurugenzi huyo alisema Mkapa anastahili pongezi kwa kuwa ndani ya kitabu chake hicho amekuwa wazi na mkweli katika kuelezea maisha yake hata kwa mambo ambayo ni mabaya kwake.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. George Kahangwa, alimpongeza Mkapa kwa kuandika kitabu hicho, akieleza kuwa uamuzi huo unapaswa kuigwa na viongozi wengine na watu mashuhuri nchini kwa manufaa ya taifa.
Alisema kuna haja viongozi wa serikali kukisoma kitabu hicho ili kufanyia kazi baadhi ya mambo yaliyoandikwa na kiongozi huyo wa ngazi ya juu.
“Wananchi wanaweza kununua kwa ajili ya kujisomea, lakini serikali inapaswa kukisoma ili kufanyia kazi mambo mbalimbali katika uongozi na kuondoa ajenda za kulaumu na kunyoosheana vidole," alishauri Dk. Kahangwa.
Alisema baada ya kuzinduliwa kitabu hicho juzi, kumeibuka mijadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kiongozi huyo kutoyaongelea hadharani baadhi ya mambo hadi amesubiri kuyazungumzia kwenye kitabu.
Dk. Kahangwa alisema kuibuka kwa mijadala hiyo kunaonyesha kuwa kitabu hicho kitaisaidia serikali kuchukua hatua juu ya mambo mbalimbali yanayotokea.
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Dk. Rugemeleza Nshala, pia alimpongeza Mkapa kwa kuandika kitabu hicho na kusema ni jambo linalowatia watu moyo.
Alisema ndani ya kitabu hicho, Mkapa anaeleza makosa yaliyowahi kufanyika na majuto yake, hivyo ni funzo kwa jamii kuwa watu wanakosea na wajifunze kutorudia makosa.
WABUNGE WAMPONGEZA
Bungeni jijini Dodoma, baadhi ya wabunge wamempongeza Mkapa kutoa kitabu kinachohusu maisha yake, wabunge wamemmiminia sifa kiongozi huyo kwa kusema amefanya jambo la ujasiri.
Wakizungumza na Nipashe kwenye viwanja vya Bunge jana, watunga sheria hao walimwelezea Mkapa kuwa ni shujaa na jasiri kwa uamuzi wake wa kuweka wazi mambo yaliyojificha, ambayo Watanzania wengi walikuwa hawayajui.
Mbunge wa Bumbuli, January Makamba (CCM), alisema Rais Mkapa ameandika historia ambayo itabaki kwa vizazi na vizazi.
“Ninampongeza kwa uamuzi wa kuandika kitabu, viongozi wengi wa Afrika wanapomaliza muda wao wa madaraka, huwa hawana utaratibu wa kuandika kitabu," alisema Makamba.
“Amekuwa mkweli, nampongeza kwa kuwa ameamua kufanya jambo la ujasiri litakazoanzisha mjadala, kuamua maoni yake yajadiliwe. Nina imani hata Mzee (Ali Hassan) Mwinyi na (Jakaya) Kikwete wataiga mfano huu."
Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), alisema: "Kitabu cha Mkapa kimechukua falsafa ya 'Dunia ni kijiji' na Tanzania ni tone ndani ya Dunia, mabadiliko ya kasi ya Dunia tangu ilipoumbwa ni makubwa, kila kilichokuwa kwenye giza, kesho kitakuwa kwenye nuru."
Mbatia alisema kikubwa cha kujifunza kupitia kitabu hicho cha Mpaka ni unyenyekevu na kuwa na tahadhari katika kufanya uamuzi, akieleza kuwa kiongozi huyo amewafundisha Watanzania kuwa makosa yaliyotokea katika utawala wake, hatarajii yatokee katika utawala wa sasa na ujao.
“Mkapa anatuambia ni lazima tujirudi, hisia, kunuia, kunena kwetu kufanane na matendo yetu, anatufanya tuwe chanya kuliko 'negative' (hasi)," alisema Mbatia.
Aliongeza kuwa kupitia kitabu hicho, Mkapa ameonyesha hisia kwamba nafsi yake inamsuta kutokana na uamuzi aliowahi kuuchukua wakati akiwa madarakani, akitolea mfano machafuko ya Zanzibar.
“Nampongeza kwa unyenyekevu wake akiwa hai, matendo mema aliyoyafanya, yamekuwa sauti huru akiwa hai na akiwa hayupo duniani. Ninamtakia kila la heri ya kuishi maisha mengi zaidi ya miaka 81 aliyotimiza sasa," alisema Mbatia.
Mbunge wa Busokelo, Atupele Mwakibete (CCM), alisema Rais Mkapa amefanya jambo la kiungwana na kizalendo kwa kuandika kitabu hicho. Alisema viongozi wengine wanapaswa kumuiga.
"Inatufundisha viongozi waliopo na waliostaafu kufanya hivyo, ni wakati mwafaka kwani itaacha alama kwa vizazi vya baadaye kufahamu mambo yaliyofanywa, ni njia sahihi ya kuhifadhi matukio," alisema.
Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) alisema: “Mambo mengi aliyoyaandika yamekuwa ni mafunzo kwa kizazi kijacho, ni mafundisho kwa viongozi na namna ya kufanya mambo yetu. Jambo lililonifurahisha ni kukiri kuwa kulikuwa na upungufu katika utawala wake."
Mbunge wa Ndada, Cecil Mwambe (Chadema), alisema Mkapa amefanya jambo la busara, lakini amechelewa.
Alisema Mkapa alikuwa Rais wa Tanzania miaka 15 iliyopita, hivyo alipaswa kuandika mapema zaidi ili viongozi waliompokea madaraka, wawe na tahadhari kuhusu mambo aliyoyaandika katika kitabu chake hicho.
Mbunge wa Viti Maalum, Hawa Mwaifunga (Chadema), alisema: “Nampongeza kwa uamuzi wake, ni jambo la ujasiri, limeshtua wengi kwa uamuzi wa kuweka wazi maisha yake, suala la EPA limenishtua hata mimi."
Juzi, Mkapa alizindua kitabu chake hicho alichokiita 'My Life, My Purpose' (Maisha Yangu, Kusudi Langu), akieleza mambo mbalimbali hasi na chanya yaliyotokea katika maisha yake pamoja na alipokuwa madarakani kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.
*Imeandikwa na Gwamaka Alipipi (DODOMA) na Mary Geofrey (DAR).
Chanzo: Nipashe