japanese
Member
- Jul 28, 2015
- 13
- 16
Imepita kama wiki moja hivi na ushehe baada ya ccm kutoka na kilichoitwa utafiti na baadae tukaambiwa ccm itashinda kwa asilimia zaidi ya sitini.Mimi binafsi nilishangaa sana kwa nini utafiti wafanye mwenyewe na hatimaye wajipe asilimia ndogo kiasi hicho.
Leo tena watu wale wale safari hii wakijiita twaweza wameibuka na matokeo mengine wanadai eti mgombea wa ccm atashinda kwa asilimia 68, na wamesema wamezunguka nchi nzima yenye idadi wa watu zaidi ya milioni 45,kati ya hao watu zaidi ya milioni 25, wameandikishwa na tume kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu mapema mwezi octoba mwaka huu lakini watafiti hawa kanjanja wametuambia eti waliweza kuwafikia watu 1848 pekee na ndipo wakaja na haya matokeo ya Leo.
lakini bado wamempa mgombea wao asilimia karibu zilezile, Mimi nilidhani wangempa walau asilimia 80 ili wafanikiwe kuwapumbaza wanamabadiliko.
Lakini pia unaweza kugundua jambo lingine kwenye tafiti hizi za ccm, wote wamekuja na kauli eti kama uchaguzi ungefanyika Leo, lakini hawasemi chochote kuhusu maoni na mtazamo mpana wa wapiga kura kuelekea uchaguzi mkuu, huu ni mkakati wa kitoto, wao wanafanya jambo hili kama komedi wakati hili ni jambo linalokwenda kutokea.
Siku chache kuelekea uchaguzi mkuu yawezekana zikiwa zimebakia siku hata kumi tutegemee matokeo mengine kama haya ya kinachoitwa utafiti,huu utaletwa na redet kwa malengo yaleyale ya kupumbaza wanamabadiliko lakini tofauti na tafiti mbili zilizopita hawa wanaweza kuja na hadaa za kujifanya mgombea wa ukawa amepanda kidogo ukilinganisha na tafiti zilizopita.
Haya kimsingi yanaashiria nini kuelekea uchaguzi mkuu,moja ccm kupitia hawa mawakala kama twaweza na baadae redet kwa kujua au kutokujua wanaongeza hamasa zaidi kwa wapenda mageuzi nchini,kwani wengi wanaona matarajio yao na shauku waliyonayo ya kutaka kuiondoa ccm madarakani haiwezi kudhoofishwa na mambo ya mizaha kama wanavyofanya hawa mawakala na badala yake wataunganisha nguvu kwenda kupiga kura kuiondoa ccm octoba 25.
Mbili ari ya mabadiliko miongoni mwa watanzania walio wengi iliongezeka baada ya uchaguzi wa mwaka 2010, ambapo ccm ni kama ili kwenda likizo na kuacha kuisimamia serikali yao ,matukio kama kutoroshwa kwa wanyama hai,operesheni iliyowaumiza wananchi,tokomeza.
wizi wa kutisha wa fedha za umma kwenye akaunti ya escrow na wafaidika wa hizo fedha kuachwa wakitamba na kuwakejeli wananchi eti mil 10 ni sawa na hela ya mboga huku wananchi wakitaabika kwa kukosa huduma muhimu, kushindikana kupatikana kwa katiba mpya ya wananchi ili hali fedha zao nyingi ziliteketea na mengine mengi ni mambo ambayo yamewatia wananchi hasira za kutaka kuuondoa mfumo kandamizi uliopo.
Tatu mchakato wa kuondoa mfumo kandamizi kimsingi ulishaanza tokea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka Jana na kinachokwenda kufanyika mwezi oktoba ni kuuhitimisha tu.
wengi wa waccm wahafidhina wanadhani hii ni mihemuko tu ya kisiasa na huu ni upepo mbaya tu kwao mwaka huu lakini baada ya muda mambo yatatulia.
Wengine wanadhani hamasa hii inatokana na wanaccm wenzao kama lowassa na sumaye kujiunga na upinzani mwaka huu,na wanajipofusha ili wasione mbali kwa kusema hata mrema aliondoka ccm na mambo waliwanyookea mwaka ule, wamesahau kuwa nyakati na mazingira vimebadilika uchaguzi wa mwaka huu.
Ccm na wanaccm lazima wajiandae kisaikolojia mwaka huu, kama mwenyekiti wao alivyowaasa kuwa tukifanya makosa tunaweza kushindwa uchaguzi.