Leo hapa JF kumekuwa na mijadala mingi kuhusu kushuka kwa thamani ya TZS kwa dola(depreciation of Tanzania shilings against US dollar).
Kabla sijachangia niliamua kugoogle latest published audited financial statements za BOT nikakuta ya May 2014. Lakini cha ajabu kwenye financial position hakuna gold wala tanzanite ambazo sisi watanzania tunazo kwenye ardhi yetu.
Maana Mimi naamini moja ya fastest stabilisation ya home current(Tz) ni BOT intervention in a currency market na nyingine ni kuuza gold outside ili kupata dollar kwa haraka sana maana gold ni pesa.
Sasa swali langu ni kweli BOT haina gold reserve au macho yangu yameshindwa kuona.
Sababu kuu ya TZS kuwa dhaifu mbele ya USD ni kuadimika kwa USD (ama mahitaji ya USD kuwa makubwa, angali ni chache). Vyanzo vikuu vitatu vya USD (kama fedha za kigeni) kwa Tanzania ni Misaada ya Kihisani (Donor's Aid), Mauzo ya dhahabu, na Utalii. Kati ya vyanzo hivyo vikuu, kimoja tu (utalii) ndio kinafanya vizuri.
Wahisani wamesitisha (ama kupunguza) misaada kutokana na sababu mbali-mbali (ikiwemo rushwa ilokithiri, mf. TGT Escrow scandal). Hii ina maana kwamba mapokezi ya USD yamepungua kwa kiasi kikubwa hasa kwenye zile akauti za misaada. ungekuwa unafanya kazi benki zinazotunza akaunti za namna hiyo ungeliona dhahiri.
Bei ya dhahabu imekuwa ikiporomoka sana kwa kipindi cha robo ya mwisho ya mwaka 2014 na mwanzoni mwa 2015, ila kwa sasa imeanza kuimarika. Inamaanisha kiasi ya USD zilizoingia kutokana na mauzo ya dhahabu zilipungua.
source: NASDAQ (soko la hisa la pili kwa ukubwa duniani)
Utalii umeendelea kuimarika, na hii inatokana na hali ya usalama nchini Kenya kudorora.
Kwa hiyo sasa tunaona uhaba wa USD kwenye hifadhi ya fedha za kigeni kupungua na kusababisha uhaba kwenye soko.