Eti king'amuzi kimeisha na nimeongeza pesa na kuonekana imelipwa lakini ni siku ya sita sasa stesheni hazionekani. Nimejaribu kupiga hizo namba zao za Voda na Airtel (nadhani) zinaita tu na kukatika kwa siku zote hizi. Sasa leo wakati naendelea kujaribu nakadhani nimepata bahati kumbe ni sauti imerekodiwa!!
Unajua ni nini hiyo sauti inasema!!??? ....eti; "samahani leo ni sikukuu, tupigie kesho".
Ndio nikajiuliza kama kweli media house iliyosajiliwa to deliver 27/7 services wanajibu hivi ni sahihi!???
Hawa jamaa watabaki kuwapata watu wa aina fulani tu wasioelewa wanachokitaka!