Zanzibar Spices
Nyuzi zinazohusu azam TV lazima uwepo..
Hahahah,mkuu unajua chanzo cha mie kukubali Azam,ni pale Nilipohama Simba Rasmi na kuwa AZAM FC.
Baada ya blaablaa za simba na AZAM kufanya vizuri nikawa shabiki mkubwa saana wa AZAM Team yenye malengo.
Hata hapa home nina jezi almost matoleo yoote ya AZAM TEAM,tena huwa nikija Dar naenda kununua pale AZAM COMPLEX.
So,kuanzia muda huo,nimekuwa nafuatilia kila wanachofanya kwenye products zao za TEAM na TV.
Mie nina Startime na pia ZANZIBAR CABLE,ila nimeviweka chini nimepandisha AZAM tangu walipoanza huduma,wiki ya mwanzo tu mie nikawa nimenunua Dekoda yao,hadi sasa sijuti kuwa na AZAM Dekoda.
Napendelea saana kufuata kitu chenye mabadiliko yanayoonekana na sio yanayoandikwa kwenye Magazeti.
Mfano ni kama AZAM Team inafanya yao bila kuwa na ushabiki wa magazeti,Simba na Yanga wao kila siku ni kuletea wachina wa Kilosa eti wapima uwanja,ebbo
Ukienda kwenye AZAM Tv kule unakuta almsot kila Mwezi ni sapraiz za ajabu na maendeleo ya kasi sana kwenye tasnia ya habari.
Sasa Mabadiliko haya ndio mie nataka kuyaona na sio ya kuandika magazetini kila siku wakati uhalisia hakuna.
Ndio maana mkuu unaniona saana kwenye nyuzi za AZAM,maana ni shabiki wa AZAM Team na AZAM TV kwa ujumla.