Ta Kamugisha
JF-Expert Member
- May 17, 2011
- 3,550
- 2,199
Mimi ni Mmiliki wa kisimbuzi cha Azam, nimelipia package ya Sports. Cha kushangaza napata Azam Sport HD, Man Utd, Liverpool TV na Madrid TV.
Naomba kuuliza, hivi Fox Sport siyo channel ya michezo au Kombat Sport, MCS International Sport, hizi channel si za sports?
Kwanini hamziweki kwenye package ya sports?
Acheni kutuibia, kama mmeshasema channel za sports ni elfu 15, basi tuwekeeni channel zote za sports, na sio kutupiga changa la macho na hiyo Azam HD pekee. Au nyie hizi channel mnaziitaje kama sio za sports?
Acheni utapeli wa mchana kweupe tuwekeeni hizo channel kwenye package ya sports.
Au mmeanza kulewa Sifa kama DSTV?
Karibu Dstv mkuu hautojuta kamwe
wewe ulitaka vipi labda manake zinapatikana still
Upo sahihi Ta Kamugisha. Mie nina tatizo kama lako.
Mimi receiver yangu iliungua lkn cha ajabu eti hazitengenezeki na wala hawauzi mbadala kama Dstv,badilikeni bwana
wewe ulitaka vipi labda manake zinapatikana still
Mkuu chukua like yangu jamaa umemjibu vzr,We utakuwa unatumia tv ya jirani,labda hata hujawahi kumiliki tv ya 14'' achilia mbali kisimbuzi cha 1k+ kwa hiyo nyamaza tu,hujui lolote
Karibu Dstv mkuu hautojuta kamwe
Hao ndio matapeli papa nchi hii.
Bora uwaambie mkuu kwa sababu na mimi hapa nilikuwa najiandaa kulipia hiyo azam sport kumbe ovyo tu!?
Kila kitu Tanzania ni uamuzi tuu wa mtoa huduma, anawaibia wananchi na serikali kuu inaona lakini hakuna usimamizi.