Azam na changamoto ya Simba na Yanga

Hatimaye dau la SSB la mrejesha kocha Azam kweli si kweli?
 
Unaona sasa unavyojichanganya, kama unadhan hao Toto ni wazuri wakiwa CCM Kirumba wala hata wasingekuwa nafasi ya pili toka mwisho, timu imeshinda mechi moja tu halafu unaona ni timu nzuri? Unazidi kujichanganya unaposema hawajacheza hata gemu moja halafu unataka kocha angewaingiza siku ya mechi na Simba hutaki kujiuliza kwa nini hizo mechi zingine nane hawakupangwa, siku ya Ruvu Shooting Bocco hakucheza kabisa kama wana washambuliaji wengine kwa nini hawakuchezeshwa na kama walichezeshwa mbona hawakuweza kuifungia timu magoli, fowadi ya Azam ina matatizo baada ya kuondokewa na Ngasa na kiungo kama Chombo ambaye alikuwa akipenyeza pasi nzuri sana za mwisho na kama unataka uamini hilo omba siku moja wakutane hata na polisi Morogoro bila ya Kipre Tchetche na Bocco kama Mwaikimba atafanya la maana. Some more questions please, Hivi ulifanikiwa kuona Mwaikimba alivyokuwa anageuzwa na wale madogo wa Simba wa U20 kwenye nusu fainali ya super8? Na kama uliona kwa nini unadhani angekuwa msaada kwa timu yake dhidi ya magwiji wa ligi kuu kama Kiemba, Chollo na Kapombe? Na unajua Owino hajacheza toka lini tangu ajiunge na Azam?
 

Mkuu Masuke kwa jinsi unavyoichukulia soka na kwa kuwa juzi mliifunga team iliyokuwa inashika nafasi ya pili 3 kwa mahesabu yako leo mnapocheza na team inayoshika mkia bila shaka mtashinda 10, au siyo?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Masuke kwa jinsi unavyoichukulia soka na kwa kuwa juzi mliifunga team iliyokuwa inashika nafasi ya pili 3 kwa mahesabu yako leo mnapocheza na team inayoshika mkia bila shaka mtashinda 10, au siyo?

Mimi siichukulia kihivyo unavyosema lakini nakushangaa wewe kuona Azam kufungwa goli tatu ni kitu cha ajabu hadi unaanzisha na thread kuona kwamba Azam walifungwa magoli rahisi hadi unasema Azam imeanzishwa kuitengenezea njia Simba, hicho ndo mimi sikitaki, Tatizo washabiki wengi wa Yanga mnachojua ni kwamba timu yenu ndo pekee inayoshinda kihalali na zingine hususani Simba, Mtibwa na Azam zinashinda kimagumashi kitu ambacho sio kweli.

Sawa kama shabiki wa upande wa pili kuna muda mwingine unaweza ukaamua kusema kama utani fulani lakini wewe kwenye mabandiko yako hakuna chembe ya utani unachoandika unakusudia kabisa kuandika na kupotosha ukweli.

Wadau wa soka letu la bongo lazima tukubali kwamba mpira una matokeo matatu, kushinda, sare na kufungwa na sio timu inapofungwa unaona ni kitu cha ajabu utafikiri kuna baadhi ya timu zina haki ya kushinda tu, tuache mpira uchezwe na timu yenye uwezo ionekane kwa kandanda safi na kupata ushindi.
 
Unaona sasa unavyojichanganya, kama unadhan hao Toto ni wazuri wakiwa CCM Kirumba wala hata wasingekuwa nafasi ya pili toka mwisho, timu imeshinda mechi moja tu halafu unaona ni timu nzuri?.......................................


Mkuu ulivyokuwa unadharau team za mwisho nilijua leo mtavuna gunia la lumbesa la magoli kule Morogoro, ulikuwa unawabeza Azam waliotoka droo na Toto iliyoshinda mchezo mmoja na inayoshika nafasi ya 2 kutoka mkiani, team yako leo imeponea chupuchupu kwa team ambayo haijawahi kushinda hata mchezo mmoja na inaburuza mkia,umeona jinsi soka ilivyo Rafiki?
 
Katika post zangu zote sikuidharau Toto nilichosema ni kukushangaa wewe jinsi ulivyokuwa unashangaa kwa nini Simba iliifunga Azam na mimi nikakuuliza kwa nini hukushangaa iliporuhusu magoli mawili na Toto, mimi najua soka ndo ilivyo ndo maana sikushangaa timu yangu kuifunga Azam na wala sijashangaa leo kuruhusu goli moja dhidi ya polisi, mimi kinachonikera katika post zako ni kushadadia kila Simba inaposhinda unaona kwamba haijashinda kwa haki hata leo baada ya kusawazisha ukaanza tena eti viongozi wa Simba wameongea na Polisi ndo maana Simba wameweza kupata goli; wapo wengi wanaosema hivyo lakini wengine post zao ukizisoma zimekaa kiutani utani lakini zako ni serious mno hadi zinakera utafikiri viongozi wa Simba huwa wanakutuma kwenda kuandaa mazingira ya ushindi kwa hiyo unachosema una uhakika nacho.

Timu zetu tunazipenda sawa lakini yanini utoke mapovu kila Simba inaposhinda mara wameenda Zanzibar kwa mganga mara wanapendelewa na marefa mara wachezaji wengine wanaendekeza unazi kwa timu ya Simba hivyo hawajitumi wanapocheza nayo.

Kwa mtu wa mpira yeyote anaamini mchezo wa mpira una matokeo ya aina tatu, kushinda, sare na kufungwa na mchezo huu pia kuna vitu viwili huchangia ushindi, uwezo pamoja na bahati, ukiamka siku hiyo unavyote unashinda kirahisi lakini ukikosa vyote unafungwa kirahisi na ukiwa na kimoja na kingine ukakosa ndo unashinda kwa taabu au unadroo au kufungwa kabisa. Nitatolea mfano kwenye mechi kama tatu tulizotoa droo, mechi ya Kagera tulikosa uwezo ingawa bahati tulikuwa nayo tulifanya uzembe kuruhusu yale magoli, Mgambo JKT tulikosa bahati lakini uwezo tulikuwa nao maana takribani shots tatu ziligonga mwamba, mechi hii ya leo pia tumekosa bahati kwa sababu mipira mingi sana imepigwa kuelekea lango lango la Polisi.

Mwisho kabisa hongereni kwa kutufikia kwa idadi ya pointi na kama wadau wa mpira tutaniane lakini sio kuwa na wivu uliopitiliza timu ambayo huishabikii inaposhinda na kutafuta visingizio visivyokuwa na kichwa wala miguu kuhalalisha kwamba timu hiyo haikushinda kihalali.
 

Mtani sipendagi kutumia huu msamiati wa "POVU" lkn leo ninalazimika kuutumia.....mtani kwanini unatoka mapovu namna hii? imekuwaje?
Yote ninayoandika hapa ni utani ingawaje in most cases kunakuwa na ukweli ndani yake,wewe fatilia utagundua yale yote watu wa mlengo wa Msimbazi mnayoyalalamikiaga kuwa sijui napotosha watu mara nyingi huja kuthibitika yalikuwa na ukweli anyway all in all ni utani tu ambao hata nyie mnautoaga sana,mara ngapi mmesema baadhi ya ushindi wetu haukuwa halali,unakumbuka mechi yetu na Toto mlichokuwa mnakisema humu jukwaani? au ndo yale masuala ya Nyani haoni..........
By the way Mtani issue nyingine unanisingizia mtani kama issue ya Viongozi wa Simba kuongea na Polisi halftime mkaingia 2nd half mkasawazisha sikuileta mimi Kaka embu fatilia utaona...kuna issue nyingine zina ukweli ambao mara nyingi unaowahusu huwa hamtaki kuukubali...nawenyewe unataka tusiuseme ksbb tutakuwa tunaonekana kuwa kila ushindi wenu tunauletea zengwe?
 
Kipande hiki umenitumia leo Mtani.......

Katika post zangu zote sikuidharau Toto................................

Ukiwa umesahau kabisa kuwa jana ulinitumia kipande hiki.....

................... kama unadhan hao Toto ni wazuri wakiwa CCM Kirumba wala hata wasingekuwa nafasi ya pili toka mwisho, timu imeshinda mechi moja tu halafu unaona ni timu nzuri?........................ ................

Kusahau ni ugonjwa mbaya sana Mkuu!
 
Kipande hiki umenitumia leo Mtani.......



Ukiwa umesahau kabisa kuwa jana ulinitumia kipande hiki.....



Kusahau ni ugonjwa mbaya sana Mkuu!

Nilichosema ni ukweli Toto imeshinda mechi moja na ni kweli si wazuri, nimesema ukweli na sio kwamba nimewadharau, hata polisi Moro nao sio wazuri ndo maana hawajashinda mechi hata moja na kutoa sare na Simba haina maana kwamba ni wazuri wangekuwa wazuri wasingekuwa huko waliko. kuna tofauti ya kudharau na kusema ukweli.

Mfano kama wewe ni Andunje na unataka kuifikia sehemu ambayo iko juu na ukashindwa kufika nikikwambia wewe ni mfupi tafuta ngazi upande ili uifikie sehemu hiyo sio kwamba nimekudharau nitakuwa nimesema ukweli na kukupa solution ya kutatatua tatizo lako.
 

Basi Mtani yamekwisha,umeshinda wewe!
 
Tumejadiliana, kukosoana na kutaniana vya kutosha mkuu, tukutane kwenye thread nyingine.
 
Basi Mtani yamekwisha,umeshinda wewe!

Hapa hatushindani mtani, tulikuwa tunajadiliana, kukosoana na kutaniana. ngoja kwanza nifuatilie habari za fao la kujitoa kwenye jukwaa la sports litakuwa hot wikend.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…